Sijamshabikia Magufuli kwa bahati mbaya.
Nilimshabikia kwa imani kubwa juu yake.
Nilimshabikia kwa kuwa nilijua ni mteule na ni mteule wa kweli mwenye kusimamama katika kweli.
Nilimshabikia kama mzalendo Mtanzania bila kulipwa chochote na asiyetegemea kulipwa chochote.
Nilimshabikia kwa kuwa yuko genuine!
Nilimshabikia SANA ili nchi yetuisitumbukie kwenye mikono ya mafisadi.
Kamwe sitajutia kumshabikia Magufuli kwa kuwa watanzania wa hali ya chini kama mimi watafaidika.
Nilikubali kejeli na matusi yote ili tu watanzania wapate kilicho bora.
Niliuvaa ujinga ili tu watoto na vijana wetu wanielewe.
Niliuvaa utoto na ujana kwa maslahi ya mama Tanzania!
Watanzania watakuwa wananielewa sasa kile nilichokishabikia kwa ukweli au propaganda ni kipi hasa.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA