Kwa kuongezea, kidini za Abraham kumchukua MTU utumwani ambaye sio ndugu yako sio dhambi na Mungu anabariki.
UONGO.
Utumwa kwenye BIBLIA.
Utumwa kwenye Biblia
sio utumwa huu tunaojua wa kukandamiza na kuonea watu.
Utumwa kwenye Biblia hauna tofauti na
ajira leo hii, ndomaana mnaitwa
Watumishi.
1) Mtu hakupaswa kuchukuliwa
kinguvu na kufanywa mtumwa. Adhabu ya mtu anayefanya hivi ni
kifo. Kwahiyo mpaka hapa tuna uhakika
MUNGU hakuunga mkono utumwa tunaoujua.
"Yeyote anayemteka nyara mwingine akamuuza au akamweka kwake, akikamatwa ni lazima auawe."
Kutoka.21.16.NENO
2) MUNGU alikataza
kuonea na kudhulumu watu, hata wageni /
watumwa.
i)
"Usimwonee mtu maskini na mhitaji ambaye umemwajiri, akiwa ni nduguyo Mwisraeli au mgeni anayeishi katika mojawapo ya miji yenu.
Mlipe ujira wake kila siku kabla ya jua kutua, kwa sababu yeye ni maskini na anautegemea ujira huo. La sivyo, anaweza kumlilia Bwana dhidi yako, nawe ukapata hatia ya dhambi."
Kumbukumbu.24.14-15.NENO
ii)
"Usimtendee mgeni vibaya au kumdhulumu, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.
“Usimdhulumu mjane wala yatima.
Ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao.
Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima."
Kutoka.22.21-24.NENO
3) Utumwa ulikuwa
makubaliano, hasa ili kulipa deni.
Watumwa wa kiyahudi wamepewa muongozo kabisa wa muda wa kazi.
Watumwa wa kigeni ni wazi ingekuwa makubaliano yao na mabosi zao maana ni
kosa kuwalazimisha.
i)
“Ukimnunua mtumwa Mwebrania, atakutumikia kwa miaka sita. Lakini katika mwaka wa saba, atakuwa huru naye ataenda zake pasipo kulipa chochote."
Kutoka.21.2-3.NENO
ii)
"Kama Mwebrania mwenzako, mwanaume au mwanamke, akijiuza kwako na kukutumikia miaka sita, katika mwaka wa saba ni lazima umwache aende zake akiwa huru.
Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu."
Kumbukumbu.15.12-13.NENO
4) Watumwa waliokimbia kutoka nchi zingine walipaswa
kupokelewa vuzuri na waisraeli. Labda walikuwa wanateswa huko. Wakija Israeli wanakuja nyumbani.
"Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake.
Mwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimdhulumu."
Kumbukumbu.23.15-16.NENO
5)
Atakayempiga akamuumiza mtumwa, mtumwa anakuwa
huru kutoka hapo hata kama muda wa kuondoka haujafika.
“Mtu akimpiga mtumwa wa kiume au wa kike kwenye jicho na kuliharibu, ni lazima amwache huru yule mtumwa kama fidia ya hilo jicho.
Akimvunja jino mtumwa wa kiume au wa kike, ni lazima amwache huru huyo mtumwa kwa kufidia hilo jino."
Kutoka. 21.26-27.NENO
6)
Atakayeua mtumwa wake ataadhibiwa.
Damu kwa kwa damu. Mtumwa asipokufa hatoadhibiwa, lakini tumeona mtumwa anakuwa
huru kuondoka akitaka.
"Mtu akimpiga mtumwa wake wa kiume au wa kike kwa fimbo na mtumwa huyo akafa papo hapo, ni lazima aadhibiwe,
lakini ikiwa mtumwa ataamka baada ya siku moja au mbili, hataadhibiwa, kwa sababu yule mtumwa ni mali yake."
Kutoka.21.20-21.NENO
7) Mabosi wakristo wanaagizwa watendee
watumwa wao / wafanyakazi wao / watumishi kwa
haki.
"Ninyi mabwana, watendeeni watumwa wenu yaliyo haki na yanayostahili, mkitambua kwamba ninyi pia mnaye Bwana mbinguni."
Wakolosai.4.1.NENO
8) Utumwa kwenye biblia hauna
ubaguzi wa rangi, taifa, kabila. Wote
waisraeli na
wasio wasiraeli walikuwa watumwa. Utumwa wa kutesa tunaojua ulikuwa ni ubaguzi kwa binadamu wengine.
Mzungu alisema: Little knowledge is a dangerous thing.
1) Demokrasia kwenye Ukristo.
YESU alikuja kuwainua wanawake wakati jamii nyingi zilikuwa haziheshimu wanawake.
"Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu."
Wagalatia.3.28.NENO
2) Mauaji ya kimbari.
Jamii zilizouawa hadi wanyama na watoto ni jamii zenye damu ya kinefili, pamoja na jamii zenye tamaduni ovu kabisa kama kutoa kafara...