NACTE : Udahili na uchaguzi 2017/18 wa Astashahada na Stashahada utafanyika moja kwa moja vyuoni

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,386
73,978
Udahili utafanyika vyuoni moja kwa moja isipokuwa vyuo vya afya na ualimu vya serikali.

In a nutshell!
Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.

Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

==========
upload_2017-5-10_20-35-15.png

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.

Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

Aidha vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.

Baraza linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017. Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Septemba, 2017.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 10/05/2017
 
Udahili kwa ngazi ya cheti na diploma umefunguliwa leo
May 10 saa 1 na dk 26 na sek 49 usiku
d43b3ddfc60ecee56a2d0a18742aeb66.jpg
863d12fbc01c7fce0b09ab609f73a9af.jpg
8552ff7e88c95231412f27612eef4035.jpg

INGIA NACTE KWA MAELEKEZO ZAIDI
 
Je mmekwisha gundua ya kuwa agizo la raisi la kuua CAS limeanzwa kutekelezwa au nimekosea?. Hii naona itakuwa ile vurugu mechi isiyo na coordination. Maombi ni moja kwa moja vyuoni.
Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.
 
Je mmekwisha gundua ya kuwa agizo la raisi la kuua CAS limeanzwa kutekelezwa au nimekosea?. Hii naona itakuwa ile vurugu mechi isiyo na coordination. Maombi ni moja kwa moja vyuoni.
Sure!
 
Yaani hapa badala ya kusonga mbele tunarudi nyuma.
 
Hapa naona wanafunzi wenye sifa wakipangwa kwingine na walio na sifa pungufu kuonekana bora
Na naona Gharama ndo zimeongezeka mara dufu zaidi..
 
Back
Top Bottom