Bunge latatua mgogoro kati ya Wizara ya Afya na Wamiliki wa Vyuo vya Afya Nchini kuhusu Vigezo vya Udahili

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
855
1,224
Tarehe 18 Oktoba 2024 ilikuwa siku ya kihistoria baada ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia kwa Waziri wake Prof Adolph F. Mkenda kuwasilisha taarifa kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kwa namna Serikali ilivyoshughulikia malalamiko ya wamiliki wa Vyuo vya kati vya kada za Afya kuhusu vigezo vipya vya udahili wa wanafunzi wa Vyuo hivyo.

Katika taarifa yake yenye kurasa kumi na tatu (13) iliyosainiwa na Mhe. Waziri , pamoja na masuala mengine imeainisha malalamiko ya wadau yaliyowasilishwa mbele ya Kamati za Bunge na Spika wa Bunge kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya vigezo vya udahili; Kwamba mchakato ulikuwa na dosari kwa;​
  • Kutokuzingatiwa kwa miongozo na taratibu zilizowekwa kuhusu mabadiliko ya vigezo vya udahili.​
  • Wadau muhimu kutokushirikishwa kikamilifu katika mchakato wa mabadiliko ya vigezo vya udahili​
Malalamiko haya yalipelekea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia A kuelekeza Kamati zake za kudumu za Elimu, Utamaduni na Michezo na ile ya Afya na Masuala ya Ukimwi kuwaita wadau na kusikiliza hoja zao, ambapo Kamati hizo zilipendekeza yafuatayo;​

I. Uelimishwaji na Ushirikishwaji wa Wadau katika mabadiliko ya mitaala:
Ilishauriwa kuwa; Wadau washirikishwe na wapewe elimu ya kutosha kuhusu vigezo vipya vya udahili kabla ya kuanza kutumika katika mwaka mpya wa masomo 2025/2026.​
II. Utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Ilishauriwa kuwa:
  • NACTVET ihakikishe inatekeleza majukumu iliyopewa kwa mujibu wa Sheria Sura namba 129 ikiwemo majukumu iliyoyakasimu kwa Wizara ya Afya.​
  • Serikali ianzishe chombo mahususi cha usimamizi na uendeshaji wa Vyuo vya Kati vya Afya vilivyo chini ya Wizara ya Afya ili kuwezesha uendeshaji bora wa mafunzo ya fani za Kada ya Afya.​
Katika taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge, Waziri wa Elimu ameishauri Wizara ya Afya kufanya mapitio upya ( curriculum review) ya mitaala iliyolalamikiwa kabla ya kuanza kutumika, na kwamba;

Soma Pia: Serikali kuburuzwa mahakamani kuhusu wizara ya afya kubadili mitaala ya vyuo vya afya vya kati bila kufuata utaratibu
  1. Kwakuwa mitaala ya Famasia na Uuguzi na Ukunga ilitakiwa kuanza kutumika katika mwaka wa masomo 2022/2023 hivyo haitakuwa imetumika kwa miaka mitatu na kwakuwa uhai wa mtaala ni miaka mitano, basi Wizara ya Afya itaelekezwa kuifanyia mapitio ili kuhuisha baadhi ya maudhui na kuhakikisha kwamba wadau husika wameshirikishwa ipasavyo.​
  2. Kadhalika kwa mtaala wa Fiziotherapia ambao ulitakiwa kuanza kutumika katika mwaka wa masomo 2023/2024 na kwakuwa wadau hawakushirikishwa ipasavyo, Wizara ya Afya itaelekezwa kupitia na kufanya marekebisho madogo (minor review) kwa kuwashirikisha wadau hasa katika hatua ya Mkutano wa Wadau (Stakeholders Consultative Meeting) ili kutoa maoni yao zaidi.​
Maamuzi haya ni hatua muhimu katika kumaliza mgogoro uliodumu kwa takribani miaka nane (8), ambapo ni matarajio ya wadau kwamba Wizara ya Afya itatekeleza ushauri wa Wizara ya Elimu , na Bunge kwa kuhakikisha mchakato wa kufanya mapitio ya mitaala unazingatia kanuni na taratibu ikiwa ni pamoja na kushirikisha wadau kikamilifu.

Mbali na suala la vigezo vya udahili pia Wizara ya Afya imetakiwa kurudisha majukumu ya utunzi na uratibu wa masuala ya mitihani kwenda NACTVET , mamlaka ambayo walikasimishwa kwa muda. Kurudishwa kwa mitihani NACTVET ni hatua muhimu sana ambayo itasaidia kuboresha ufanisi wa taaluma ya mafunzo, na kupunguza gharama ya fedha za mitihani.​
 

Attachments

  • TAARIFA YA VIGEZO VIPYA VYA UDAHILI VYUO VYA KATI VYA KADA YA AFYA VILIVYOSHUGHULIKIWA.pdf
    398.7 KB · Views: 21
Back
Top Bottom