Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,465
- 13,080
Katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 124,286 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 86 vilivyoidhinishwa kudahili wanafunzi katika Shahada ya Kwanza. Aidha, jumla ya programu 856 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 809 mwaka 2023/2024, ikiwa ni ongezeko la programu 47 za masomo.
Vilevile kwa upande wa nafasi za udahili, mwaka huu kuna jumla ya nafasi 198,986 ikilinganishwa na nafasi 186,289 mwaka uliopita. Hili ni ongezeko la nafasi 12,697 sawa na asilimia 6.8 katika programu za Shahada ya Kwanza.
Pia katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 98,890 sawa na asilimia 79.6 ya waombaji wote walioomba udahili, wamepata udahili kwenye vyuo walivyoomba. Idadi ya waombaji wa udahili na watakaodahiliwa inatarajia kuongezeka katika Awamu ya Pili ya udahili.
Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia leo tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2024. Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.
Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.
wakati wa kuomba udahili. Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majina ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja inapatikana kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).
Tume inatangaza kuwa Awamu ya Pili ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2024/2025 imeanza leo tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2024. Tume inawaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Kwanza kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.
Aidha, Tume inaelekeza Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kutangaza programu ambazo bado zina nafasi. Waombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili wa Awamu ya Pili kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya udahili iliyoko katika tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).
WITO KWA WAOMBAJI UDAHILI
Waombaji udahili wa Shahada ya Kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika. Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.
Imetolewa na
Prof. Charles D. Kihampa
KATIBU MTENDAJI
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA
Pia soma:Prof. Charles D. Kihampa
KATIBU MTENDAJI
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA
~ TCU yafungua dirisha la udahili kwa waombaji wa vyuo vikuu kwa Mwaka 2024/25
~ Matokeo Kidato cha Sita 2024 yatoka. Ufaulu wapanda kwa asilimia 0.26
~ 𝗧𝗖U Admission Guide Book 𝟮𝟬𝟮𝟰/𝟮𝟬𝟮𝟱