NACTE mlichowafanyia watoto wa kimasikini sio Haki

kimaus

JF-Expert Member
May 10, 2011
565
652
Kuna kijana wangu anasoma katika moja ya vyuo vya afya vinavyosimamiwa na NACTE.

Baada ya mitihani ya mwaka wa pili kuvuja mwaka jana na kurudiwa, matokeo yametoka.

Sasa kitu ambacho naona si cha kiungwana ni uamuzi wa wa NACTE kutowapa watoto waliofail baadhi ya masomo mitihani ya Supplementary ili waweze ku clear na kuendelea mwaka wa tatu na wa mwisho, badala yake wale wote ambao either amefeli somo moja au mawili, wametakiwa KURUDI NYUMBANI mpaka mwezi wa nane (August) mwaka huu ndipo waje wafanye mitihani waliyofail pamoja na wanafunzi wa mwaka wa pili wa mwaka huu. Maana yake watoto hawa wanapoteza mwaka mzima kwa kufeli somo moja au mawili?

Sijajua kama ndio sheria yao NACTE au ni utaratibu tu, lkn vyovyote vile utaratibu huu sio MZURI.

NACTE haiwezi kutunga mitihani ya marudio?

Watoto wapoteze mwaka nyumbani kwa kufeli somo moja?

Mzazi unajua mtoto wako anamaliza mwaka huu, lkn mtoto anarudi nyumbani kukaa miezi 8 kusubiri mtihani mmoja, then ndiyo aendelee.

This is not right. Kama kuna mahali nimekosea NACTE watoe ufafanuzi, lkn kwa kweli huu utaratibu sio mzuri.
 
NACTE hawatungi mitihani bali ni Wizara ya Afya. Sheria za mitihani zinatungwa na mtoa mitihani. Hivyo NACTE hahusiki kwa lolote
 
Mitihani ya vyuo ukifeli pale ulipo utapiga gwaride usubirie wanaokuja nyuma yako utahiniwe nao mwaka unaokuja
 
NACTE hawatungi mitihani bali ni Wizara ya Afya. Sheria za mitihani zinatungwa na mtoa mitihani. Hivyo NACTE hahusiki kwa lolote
Asante kwa kunirekebisha.
Lkn bado wizara ya Afya hawafanyi haki
 
Ukiona hivyo ujue mtihani wa supp ndo ulokuwa plan B(huo walio urudia)
Hapo la msingi ni kukomaa ili kumaliza!
Pole sana mtoto wa maskini
 
Sasa mwanao kam ni kilaza siumtafutie shamba mpe mtaji ajiajir usilazimishe aendelee tu kusoma wakat kichwan hamnazo, kwann afeli kwanza na utake upate mlango wa pili wa kutokea?
 
Mbona wameruhusiwa boss kufanya mtihani 2 March 2022..na kuendelea na masomo.Cheki barua hiyo ila wizara wana mambo ya hovyo hawaeleweki kabisa mambo yao.
 
Attachments

  • BARUA, MATOKEO RASMI YA MITIHANI YA DISEMBA,2021.pdf
    297.1 KB · Views: 20
Asante kwa kunirekebisha.
Lkn bado wizara ya Afya hawafanyi haki
Hawatendi haki nakubaliana na wewe. Na shida kubwa ni Hivi vyuo vya private kukubali kuburuzwa na wizara ambayo ilihusika katika uvujaji wa mitihani hiyo
 
Hawatendi haki nakubaliana na wewe. Na shida kubwa ni Hivi vyuo vya private kukubali kuburuzwa na wizara ambayo ilihusika katika uvujaji wa mitihani hiyo
Vyuo vya private ndo vimeharibu hii kozi kwakweli...imefanya kuwe na wanafunzi wa ajabu wenye ufauli hafifu sana na pia wao ni kufanya biashara baada ya kutoa elimu stahiki...kwa sasa C.O haina thamani hata huku mtaani kwa sababu ya mlundikano wa vyuo vya private mbaya zaidi vijana wanamaliza shule hata kuchoma tu sindano hawajui,history taking mtihani
 
Acha uongo wewe! Vyuo vya Serikali vipo hoi! Vya private vinajitahidi. Best students wanatoka private. Acha akili za kitoto za kuwepo na Wanafunzi wachache. After all mitihani wanafanya huo huo na wasimamizi wanateuliwa na wizara ya Afya. Je mitihani iliyovuja si ilivuja katika vyuo vya Serikali? Acha ujinga
 
Mzee hakuna nilipokutukana..toa maoni kiistarabu ukweli utabaki hivyo hivyo hata hizo pepa kuvuja zimetoka huko huko private wao hawaangalii ubora wao ni kufaulisha na GPA za kubumba wanafunzi vilaza.
 
Kweli mkuu watu wanapiga GPA za 5 Huko, wakati huku hata ya 3.5 inatafutwa kwa jasho
 
Mzee hakuna nilipokutukana..toa maoni kiistarabu ukweli utabaki hivyo hivyo hata hizo pepa kuvuja zimetoka huko huko private wao hawaangalii ubora wao ni kufaulisha na GPA za kubumba wanafunzi vilaza.
Unaeneza uongo. Nilete uthibitisho hapa kuwa Wizarani kuna mtu aliiba marking Scheme na kuituma kwa wanafunzi wa NTA level 5 katika chuo cha serikali!!!!!!!! Acha uongo
 
Back
Top Bottom