NACHINGWEA: Mwenge wa uhuru wazindua, kutembelea na kuzindua miradi sita (6) wilayani Nachingwea

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
3,134
2,470
Tarehe 25.8.2021 Mwenge wa Uhuru umetembelea, kuzindua na kuweka jiwe la msingi jumla ya miradi sita katika wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi.

Miradi iliyozinduliwa ni pamoja na mradi wa maji katika kijiji cha Namikango, mradi wa wodi ya wazazi ya kisasa katika hospitali ya wilaya na mradi wa mashine ya kusaga ya walemavu katika kijiji cha Naipanga uliotolewa kupitia mikopo ya halmashauri pamoja na kukabidhi hundi ya mikopo kwa vijana.

Aidha Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Lut Josephine Mwambashi ametembelea mradi wa shule ya sekondari ya wavulana katika kijiji cha Chiumbati mradi ambao unatarajiwa kuchukua wanafunzi 1600 kuanzia kidato cha 1 hadi cha 6 baada ya kukamilika ambapo kiongozi wa mbio za mwenge amesifu juhudi zilizofanywa na wananchi katika ujenzi wa shule hiyo.

Pia Lut Mwambashi ametembelea mfano wa miradi ya shamba darasa la mbogamboga katika kata ya Nachingwea mjini.

Pia Lut Mwambashi ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Muungano.

Mbio za Mwenge wa uhuru katika wilaya ya Nachingwea zilifanyika tar 25.8.2021 baada ya kuupokea mwenge huo katika kijiji cha Lionja kutoka wilaya ya Liwale ambapo Mh Mkuu wa wilaya ya Nachingwea ndg Hashim Komba aliukabidhi mwenge wa uhuru kwa Mh Hassani Ngoma mkuu wa Wilaya ya Ruangwa tar 26.8.2021.

Mkesha wa mwenge katika wilaya ya Nachingwea ulifanyika katika kijiji cha Namatula kata ya Namatula.

Mh mkuu wa wilaya ya Nachingwea akipokea mwenge wa uhuru kutoka wilaya ya Liwale
Screenshot_20210827-200247.jpg

Screenshot_20210825-213704.jpg


IMG_20210825_192402_170.jpg

IMG_20210827_105207_544.jpg

20210825_213934.png

Screenshot_20210827-200144.jpg

Screenshot_20210827-200213.jpg

Screenshot_20210825-101523.jpg

IMG_20210827_105207_481.jpg

Mh Mkuu wa wilaya ya Nachingwea akikabidhi mwenge kwa Mh Mkuu wa wilaya ya Ruangwa
Screenshot_20210827-200103.jpg
 
Hiyo mikesha sio hatarishi kwa korona? Ila hii nchi tumepigwa pakubwa sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom