Serikali haijapata Mwekezaji wa Mwenge wa Uhuru?

Serikali haijapata Mwekezaji wa Mwenge wa Uhuru?

Mizega

Senior Member
Joined
Feb 10, 2021
Posts
161
Reaction score
339
Ama kuhusu gharama za uendeshaji wa Mwenge wa uhuru ni kubwa.

1. Kila mkoa hutumia wastani wa lita 5000_ 6000 za Diesel wakati wa raking na wakati wa kukagua miradi na kuukimbiza. Mikoa iko 31.

2. Kila halmashauri hutenga bajeti ya posho,viburudisho,sare na zawadi kwa wakimbiza mwenge kitaifa si chini ya milioni 60 kwa halmashauri zote( makadirio) kulingana na kila halmashauri.

3. Wakati wa kuupokea kuingia mkoan na kuutoa nje ya mkoa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hutumia si chini ya milioni 30 kwa ajili ya sare za kamat ya sherehe mkoa, kamati ya usalama, ccm, posho na vyakula.

4. Gharama za dharula, jeshi la polisi, mgambo na suma jkt napo hela zinaenda.

Upi hasa mchango wa mwenge wa uhuru katika karne hii ambayo tuna viongozi kila ngazi wenye uwezo wa kukagua miradi ya maendeleo? Kuna wakati miradi iliyokwisha kuwekewa majiwe ya msingi na wakuu wa mikoa wilaya mawe yenye maandishi huondolewa ili kuweka mapya kwa ajili ya mwenge. Kama mkuu wa mkoa au wilaya au RAS angeweka jiwe la msingi au kuzindua angetumia mamilioni yote haya?

Nawaza kwamba, badala ya kuweka wawekezaji kwenye bandari kwa miaka isiyotajwa, hebu tuanzeni kuwapa kwanza Mwenge wa Uhuru. Na kwakuwa wao wana teknolojia basi tuukimbize mpaka Dubai, tukaangaze huko na penye giza pawe nuru.

Wasalaam
 
Unawalazimisha wachawi wa CCM wakabidhi tunguli kwa Pastor?
Una RC, DC, takukuru,usalama,rpc,ded,das..wote hawa wanangoja moto uje kukagua mradi kwa gharama kubwa,..hizo nafasi zina umuhimu gani kuwepo? Mwenge una faida gani zaidi ya matambiko? Hebu aje mtu mwenye andiko kuhusu tija za mwenge
 
Kuna ofisi ya CAG kila mwaka makosa hayapungui , wangetupia jicho la kuongezewa trchnologia pia
 
Huwa najiuliza wale wakimbiza mwenge kitaifa huwa wanalala muda gani.. unakuta saa kumi na moja mwenge umetinga mkoani au wilayani sàsa huko walikotoka wametoka saa ngapi!!??
 
Huwa najiuliza wale wakimbiza mwenge kitaifa huwa wanalala muda gani.. unakuta saa kumi na moja mwenge umetinga mkoani au wilayani sàsa huko walikotoka wametoka saa ngapi!!??
Wewe ukilipwa vizuri mfano milioni kwa siku ukaambiwa upunguze masaa ya kulala utakataa? Na ukiahidiwa u dc baada ya kumaliza kukimbiza utalala ama utakagua barabara ya lami kwa nyundo?
 
Sijawai kuelewa huu mwenge ingawa niliwai kukimbiza nao mwenyewe nikiwa chipukizi.
 
DP World wapo, wakipewa mchongo watawekeza na huko
 
Back
Top Bottom