Nabii Frank Kilawah acha kudanganya watu

Nabii Frank Kilawah acha kudanganya watu

Mkuu, ile haijatokea bahati mbaya. Yule kipofu feki siyo muigizaji. Kuigiza ni kipaji hata watu wakiku-train kuna sehemu inabidi uwe normal ufanye vile ulivyozoea ndio maana kwenye kuigiza kuna (cut, take one, action). Hii inafanywa ili pale ulipo-act normal waparudie. Sasa ile ilikuwa live audience, wasingeweza kumwambia arudie tena kuwa kipofu halafu akiponywa aanze kushangilia.

Hahhaaaaa
 
wakweli wapo lakini sio Frank namjua enzi akijiita mchungaji,kama unabii unapatikana ghafla baada ya kumuaibisha Yesu kwa kujiita mchungaji na kutenda maovu hadi jamii ikamfukuza kwa tabia zake basi sio YESU ninayemwabudu.

Duuh,mkuu unamchana kinoma[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyu Frank kilawah anayoyafanya yote Mungu anamuona

Alikuja mbeya hapa hotel ya mbeya forest akawaombewa watu kwa tshs 200,000 bila hela hiyo umuoni yana mwisho
Hivi ni kweli ana upako wa kutoa laki 2 bola nienda sinza vatican kwa mwamposa
 
huyu Frank huo unabii kautoa wapi, namjua vizuri sana enzi anajiita mchungaji na kuja kufungua kanisa eneo mkimbizi F iringa.muulizeni aliondoka kwa staili gani na kukimbia kanisa lake bila hata kuaga,nashtuka namuona kwenye TV akijiita nabii na miujiza kibao.Hakika kwa kupitia huyu nabii ninayemfahamu nimeamini manabii wa uongo wapo.
Alipotoka iringa alienda tanga uko nako sijui nini kaalibu sasa hivi yupo dar
 
Acha woga wewe, Wazazi wako hawakwenda shule ndio waliopokea hiyo dini halafu wakakurithisha wewe, wewe wamekupeleka shule ili uelimike uwasaidie. Sasa kama na wewe bado unamwogopa yesu kwa sababu za kuambiwa na wazazi wako baada ya kutishwa na wamisionari, elimu uliyopata itakuwa haijakusaidia siyo wewe tu, pamoja na wazazi wako na watu waliokuzunguka.

Mbona zamani hata kupita tu kwenye makaburi mlikuwa mnaogopa, kunyooshea kidole kaburi ilikuwa hatari, mbona siku hizi mambo yenu ya kishenzi na machangudoa mnaenda kufanyia pale makaburini kinondoni? nini kimebadilika?

Hata huko kwenye dini tumia akili hiyo hiyo itakusaidia.
Bado sana ,sijakuelewa mkuu labda jina lingine ila sio la Yesu
 
Acha woga wewe, Wazazi wako hawakwenda shule ndio waliopokea hiyo dini halafu wakakurithisha wewe, wewe wamekupeleka shule ili uelimike uwasaidie. Sasa kama na wewe bado unamwogopa yesu kwa sababu za kuambiwa na wazazi wako baada ya kutishwa na wamisionari, elimu uliyopata itakuwa haijakusaidia siyo wewe tu, pamoja na wazazi wako na watu waliokuzunguka.

Mbona zamani hata kupita tu kwenye makaburi mlikuwa mnaogopa, kunyooshea kidole kaburi ilikuwa hatari, mbona siku hizi mambo yenu ya kishenzi na machangudoa mnaenda kufanyia pale makaburini kinondoni? nini kimebadilika?

Hata huko kwenye dini tumia akili hiyo hiyo itakusaidia.
Dogo kauli zako zinavuka mipaka
 
kwa kweli sijui nikujisahau au ndio kamba zenyewe..jamaa kasema alifaulu form four kwa div 1point 12 na form six div 1ya point 19....nilichoka ...nilizima TV nikaendelea na mambo yangu
 
Bado sana ,sijakuelewa mkuu labda jina lingine ila sio la Yesu

Ni kweli hujanielewa, na mi sikuandika ili wewe unielewe kwa sababu najua akili zako kuna mtu kazishika, wewe kunielewa ni mpaka upate hisani ya kurudishiwa akili zako na huyo yesu. Nimeandika ili wengine wenye akili zao wanielewe.

BTW wewe umejazwa roho mtaka-tifu? Unanena kwa lugha? Nijibu tafadhali.
 
Kwanini akili zako zote umeziwekeza huko? Hivi wote wanaokwambia kuna utapeli wa kufa mtu kwenye haya madhehebu, wote kwako ni waongo?
Ndugu yako alipona,sawa. Lakini isiwe passport ya kuaminisha watu kuwa kwenye madhehebu hayo pako shwari 100%.
Vinginevyo yaweza nawe kuwa ndiye walewale.
Nadhan kama umesoma maelezo yangu vizur hukupaswa kusema nimeamini asilimia Mia. Kwanzaa mm sio muumini wa madhehebu hayo kabisa na nilikuwa mpondaji mzuri sana katika maswala hayo ya miujiza nilikuwa sihudhurii mkutano wowote zaid ya mwakasege. Ila nilipoona mtu kapona wakaribu yangu na hajahama dhehebu amebaki anaamini aliemponya Ni kristo kupitia huyo nabii. Siwezi kunena mabaya tena juu ya hao manabiii Mungu aliesirini ndo anawajua vyema waliowake. Madam aliomba kwajina la yesu Hilo ndilo nililoamini kama yeye anayesu mwingine mm niliamini yule naemwamini.

Ushauri. Endapo unaona huendani na iman nyingine simama kwenye iman yako ila mwili wako akili yako na chochote kinachomilikiwa na wewe kisitumike kuksmashifu iman ya mwingine. Hiyo ndo point yangu.
 
kwa kweli sijui nikujisahau au ndio kamba zenyewe..jamaa kasema alifaulu form four kwa div 1point 12 na form six div 1ya point 19....nilichoka ...nilizima TV nikaendelea na mambo yangu

Mkuu wewe ndio hukuelewa, wenzako mle ndani wanaelewana wanasaidiwa na roho mtaka-tifu. Unaweza kuta hiyo div 1 ya pt 19 ni grade za mbinguni! Madai yao ni kuwa roho mtaka-tifu ni mwalimu pia!
 
Mkuu wewe ndio hukuelewa, wenzako mle ndani wanaelewana wanasaidiwa na roho mtaka-tifu. Unaweza kuta hiyo div 1 ya pt 19 ni grade za mbinguni! Madai yao ni kuwa roho mtaka-tifu ni mwalimu pia!
Hakuna binadamu aliyekamilika, ukilijua hilo hupati shida saana! Na Roho Mtakatifu yupo pale pale!!
 
Kinachotutatiza ss watu ni kosa kumjua Mungu wa kweli!!! Na watu wanataka kumjua Mungu wa kweli kupita watu na sio nelo la Mungu (bibilia) kila binadamu anamapungufu yake ila Mungu anatusaidi tunaweza kuvumiliana, wachaji wa Mungu wapo na manabii na watumishi wa uongo wako pia!!! Na hapa tunahitaji kulijua neno haswa (bibilia) na kujaa Roho Mtakatifu na sio kujazwa roho mtakavitu( ambae roho huyo huwajaza watumishi wa shetani na wanafavitu ili kuzidi kufanya wale watu wasio mwamini Yesu wapinge na kusema hakuna wokovu au walokole ni waongo) lakini Yesu alisha toa ole kwao!!!
 
Dah poleni sana makanisani kwenu, sisi hakuna ujinga kama huu, Kwanza tungemtandika bakora Kuanzia Nabii mwenyewe mpaka mgonjwa na mama yake pia
These are self ordained prophets. Wanaombatana nao wanafanana nao.
 
Tupien ka photo nimfahamu, mdogo wangu alipigwa laki mbili Na nusu Na huyu nabii bila hata risiti weken ka photo wakuu.
 
Hivi hamna namna serikali inaweza dhibiti utapeli unaoendelea kwenye haya baadhi ya makanisa?
Hilo ni swala la imani ni ngumu sana serikali kuliingilia......ni swala la mtu binafsi kutambua huo utapeli.
 
Huyu nabii juzi kafanya kitu ambacho kimenishtua sana kwenye kipindi chake, katokea mtu anadai ni kipofu kaja na mama yake mzazi, yule mama kaulizwa kadai huyo mtoto wake kazaliwa hana macho kabisa, kabla hajamuombea kamera zilikuwa zinamuonyesha yule kijana akiwa amefumba macho, na ukimwangalia yule kijana alikuwa kama anainama chini muda mwingi.

kuinamisha kichwa chini ni hulka ya binadamu inayoambatana na kuona aibu. Basi nabii akasema huyu mtu tokea kuzaliwa hajawahi kuwa na macho, sasa mungu akimrudishia hata jicho moja si itakuwa safi, basi akachukua maji ya chupa na kummwagia huku akiweka mikono yake kwenye yale macho, eti yule jamaa akafungua jicho moja linaona.

Cha ajabu eti yule kipofu ambaye hajawahi kuona tokea kuzaliwa akapata jicho moja na ye akawa katulia tu kama hamna kilichotokea, yaani fresh tu. Mtu ambaye hajawahi kuona tokea amezaliwa hawezi kuwa vile akiona.

Halafu huu usanii anaofanya nabii anashirikisha hadi wamama watu wazima kuongea uongo mbele ya kadamnasi. Toka lini mungu akamponya mtu nusu kwa kumrudishia jicho moja? Ningekuwepo siku hiyo haki ya mungu ningeomba urudie kuomba ili jicho la pili nalo lirudi.

USHAURI: Katika miujiza ambayo haina longolongo ni upofu, namshauri huyo nabii asiigize tena kuponya mtu kipofu maana kuna siku itamtokea puani. kuna watu kama sisi tukiwa eneo la tukio tutataka tuhakikishe kama huyo kipofu kweli ni kipofu kabla hujamuombea halafu tutakuumbua.

Yeye aendelee na miujiza iliyozoeleka ambayo hatuwezi kuthibitisha kama sijui nilikuwa naumwa ukimwi, tumbo, nilikuwa sizai,mapepo, kichwa kuuma, kutokwa na damu, BP n.k ila asicheze kabisa na kumponya kipofu ambaye hana macho, huo muujiza hata yesu ukimwambia arudie te na hawezi.

Nikupongeze ndugu yangu kwa kuhoji mambo yanayopaswa kuhojiwa ikiwa ni kweli ama la! Biblia ya Wakristo imekamilika sana katika jambo hili. "Wapendwa msiziamini kila roho. Zijaribuni Kama zimetoka kwa Mungu; kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani." 1Yoh 4:1. Biblia inatoa tahadhari ya kutosha juu ya matendo ya miujiza. Miujiza sharti ipambanuliwe. Uponyaji nao sharti upambanuliwe kama ni kutoka kwa Mungu ama la (1 Wakorintho 14: 26 - 29). Katika karama za roho zilizoainishwa katika 1Kor 12: 1 - 10) ipo karama ya kupambanua roho. Hivyo nakupongeza kwa kulifahamu hilo.
 
Back
Top Bottom