Nabii Frank Kilawah acha kudanganya watu

Nabii Frank Kilawah acha kudanganya watu

Hapana usiseme hivo....kuna shehe alitoa tangazo chanel 10 kuwa anaponya na kutoa pepo kwa watoto wakike na akina mama...aliita wote waende kuombewa..tangazo lilikuwa kwa style ya wachungaji....
Anajiita shekhe shariff majini mpk insta yupo full kujitangaza
 
Naskia uyo nabii frank bila lak mbili sijui tatu hakuombei
 
Nilipita mkutanon kwake nikakuta wadada wasaidizi wake wamevaa skin jeans (kabanamsuli) nilichoka
 
Huyu nabii juzi kafanya kitu ambacho kimenishtua sana kwenye kipindi chake, katokea mtu anadai ni kipofu kaja na mama yake mzazi, yule mama kaulizwa kadai huyo mtoto wake kazaliwa hana macho kabisa, kabla hajamuombea kamera zilikuwa zinamuonyesha yule kijana akiwa amefumba macho, na ukimwangalia yule kijana alikuwa kama anainama chini muda mwingi.

kuinamisha kichwa chini ni hulka ya binadamu inayoambatana na kuona aibu. Basi nabii akasema huyu mtu tokea kuzaliwa hajawahi kuwa na macho, sasa mungu akimrudishia hata jicho moja si itakuwa safi, basi akachukua maji ya chupa na kummwagia huku akiweka mikono yake kwenye yale macho, eti yule jamaa akafungua jicho moja linaona.

Cha ajabu eti yule kipofu ambaye hajawahi kuona tokea kuzaliwa akapata jicho moja na ye akawa katulia tu kama hamna kilichotokea, yaani fresh tu. Mtu ambaye hajawahi kuona tokea amezaliwa hawezi kuwa vile akiona.

Halafu huu usanii anaofanya nabii anashirikisha hadi wamama watu wazima kuongea uongo mbele ya kadamnasi. Toka lini mungu akamponya mtu nusu kwa kumrudishia jicho moja? Ningekuwepo siku hiyo haki ya mungu ningeomba urudie kuomba ili jicho la pili nalo lirudi.

USHAURI: Katika miujiza ambayo haina longolongo ni upofu, namshauri huyo nabii asiigize tena kuponya mtu kipofu maana kuna siku itamtokea puani. kuna watu kama sisi tukiwa eneo la tukio tutataka tuhakikishe kama huyo kipofu kweli ni kipofu kabla hujamuombea halafu tutakuumbua.

Yeye aendelee na miujiza iliyozoeleka ambayo hatuwezi kuthibitisha kama sijui nilikuwa naumwa ukimwi, tumbo, nilikuwa sizai,mapepo, kichwa kuuma, kutokwa na damu, BP n.k ila asicheze kabisa na kumponya kipofu ambaye hana macho, huo muujiza hata yesu ukimwambia arudie te na hawezi.
Wewe utakuwa sio shirika nasi umeenza vizuri sana, ila hapo pa Jesu hakika umehajaribu,na naomba niikemee imani yako mbovu juu ya Yesu
Ambaye kila dini wanaamini atashuka kwa parapanda, mkuu kuwa makini na Jina la Simba wa kabila la Yuda.
 
Yeye aendelee na miujiza iliyozoeleka ambayo hatuwezi kuthibitisha kama sijui nilikuwa naumwa ukimwi, tumbo, nilikuwa sizai,mapepo, kichwa kuuma, kutokwa na damu, BP n.k ila asicheze kabisa na kumponya kipofu ambaye hana macho, huo muujiza hata yesu ukimwambia arudie te na hawezi.

hapo sasa umeuvuka mpaka[/QUOTE]
kwani yesu ndo anaponya au mungu labda tuanzie hapo kwanza
 
Msilitaje Jina La Bwana Yesu bure. Kwa kukuelewesha katika Jina Hili la Yesu vitu vinavyoonekana na visvyoonekana viliumbwa. Pili. Kila goti litapigwa mbele yake na kila ulimi utakiri kwamba Yesu Ni Bwana ukiwepo wewe uliyesema hata Yesu hawezi kufanya miujiza. Wewe endelea kuchezea Jina Hili maana hakika siku moja utalia na kuomboleza utakapmwona akishuka na mawingu. Kusema kwamba Yesu hawezi kutenda miujiza ndugu yangu umeenda mbali sana. Aliyeumba vitu vyote hatashindwajwe kutenda miujiza. Tatu. Yesu yu hai siku zote maana yeye nimwanzo na mwisho. Yeye na Mungu ni wamoja.
Imeandikwa wap Yesu aliumba vitu vyote? Yesu si Mungu . kasome bibkia vzur acha kupotosha
 
Huyu Frank kilawah anayoyafanya yote Mungu anamuona

Alikuja mbeya hapa hotel ya mbeya forest akawaombewa watu kwa tshs 200,000 bila hela hiyo umuoni yana mwisho
 
huyu Frank huo unabii kautoa wapi, namjua vizuri sana enzi anajiita mchungaji na kuja kufungua kanisa eneo mkimbizi F iringa.muulizeni aliondoka kwa staili gani na kukimbia kanisa lake bila hata kuaga,nashtuka namuona kwenye TV akijiita nabii na miujiza kibao.Hakika kwa kupitia huyu nabii ninayemfahamu nimeamini manabii wa uongo wapo.
 
Tangu ulipoanzisha bandiko lako tumekwenda pamoja, conclusion yako ndo umechemka mbaya na ime-ruin credibility yote ya bandiko lako ovu. Nikukumbushe kama umesahau, au nikufahamishe kama hujui...YESU NI YEYE YULE JANA, LEO NA HATA MILELE. Kama alifufua wafu Jana, atafufua wafu leo na atafufua wafu kesho. Kama aliponya Kipofu, anaponya hata sasa na ataponya hata baada ya miaka 500.

Uwe na adabu unapotema pumba zako kwa kumshirikisha YESU

Eeh! Na wewe hapa ndio unaona umetema facts? Kweli waliotuletea dini walimaliza kila kitu! Yaani linapokuja swala la dini watu wa aina yako huwa akili zote wanashikiwa na YESU, wanakuwa mazezeta. No wonder ndio maana utapeli kama ule wa nabii frank unafanyika hadharani mpaka tunaoangalia kwenye TV tunauona lakini waliopo kwenye eneo la tukio hawaoni, kisa eti "YESU NI YEYE YULE JANA, LEO NA HATA MILELE.
 
Kuhusu uponyaji isikupe shida Yesu aliponya sana ukisoma mathayo 15:29-31, utajionea!!! Na manabii wa uongo wapo na wakweli pia wapo!!!!
wakweli wapo lakini sio Frank namjua enzi akijiita mchungaji,kama unabii unapatikana ghafla baada ya kumuaibisha Yesu kwa kujiita mchungaji na kutenda maovu hadi jamii ikamfukuza kwa tabia zake basi sio YESU ninayemwabudu.
 
kama aliweza wakati ule kwanini ashindwe sasa? acha dhihaka ni vyema ukamuongelea huyo frank unayemuona na sio Yesu

Acha woga wewe, Wazazi wako hawakwenda shule ndio waliopokea hiyo dini halafu wakakurithisha wewe, wewe wamekupeleka shule ili uelimike uwasaidie. Sasa kama na wewe bado unamwogopa yesu kwa sababu za kuambiwa na wazazi wako baada ya kutishwa na wamisionari, elimu uliyopata itakuwa haijakusaidia siyo wewe tu, pamoja na wazazi wako na watu waliokuzunguka.

Mbona zamani hata kupita tu kwenye makaburi mlikuwa mnaogopa, kunyooshea kidole kaburi ilikuwa hatari, mbona siku hizi mambo yenu ya kishenzi na machangudoa mnaenda kufanyia pale makaburini kinondoni? nini kimebadilika?

Hata huko kwenye dini tumia akili hiyo hiyo itakusaidia.
 
Niliona kile kipindi aisee ila kuhusu ukweli wa tukio wanajua wahusika wenyewe ila nlitegemea jamaa aruke ruke na kukimbia huku na kule.

Mkuu, ile haijatokea bahati mbaya. Yule kipofu feki siyo muigizaji. Kuigiza ni kipaji hata watu wakiku-train kuna sehemu inabidi uwe normal ufanye vile ulivyozoea ndio maana kwenye kuigiza kuna (cut, take one, action). Hii inafanywa ili pale ulipo-act normal waparudie. Sasa ile ilikuwa live audience, wasingeweza kumwambia arudie tena kuwa kipofu halafu akiponywa aanze kushangilia.
 
Back
Top Bottom