....... Akawatolea mfano mwingine, akisema, ufalme wa mbinguni umefanana
na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu
walipolala akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano,
akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa,
yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda
wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako?
Limepata wapi basi magugu? Akawaambia adui ndiye aliyetenda hivi.
Watumwa wakamwambia, basi wataka twende tuyakusanye? Akasema la;
msije mkakusanya magugu na kuzingoa ngano pamoja nayo. Viacheni
vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia
wavunao, yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita
mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. (Math.13:24-30)
Tafakari ya leo usiku wapendwa.
Usiku mwemani.