Naanza kuamini wafanyabiashara wa mafuta wana nguvu sana

Mwenye wizara ametetea kwa kusema bei imepanda kulingana vita ya Ukraine halafu akasema huko ulaya pia nao wamepandisha bei kwa hiyo bei imepanda kihalali
Yani hawa wauza mafuta wanajua kupandisha tu sio kushusha hii bidhaa na hapo wakisema ishuke utakuwa mzozo.
 
... katikati ya jiji la Dar kwa siku 4 kuanzia Ijumaa hadi J4 kabla bei hazijatangazwa almost sheli zote za Total, Puma, na Oryx waliweka utepe mwekundu mafuta yameisha. Sekunde ileile baada ya bei mpya zote zilianza kuuza mafuta kwa fujo!

Unajiuliza mbona nchi inachezewa sana kana kwamba hakuna Serikali hupati jibu! Angekuwa Jiwe angetoa mfano ambao wasingerudia tena!
Tatizo jiwe wakati anatoa show zake watz mlilalamika tena kuwa ni mshamba..sasa tuendelee na wajanja tu hamna namna
 
Moda msiunganishe huu uzi.

Kwa kweli hawa watu nadhani wana nguvu ya ziada na nnaamini kuna vigogo wengi wanadeal na hii biashara maana ni kama Serikali inawabeba sana.

Fikiria akiba ya mafuta ni ya miezi miwili nyuma ila bei imepata matuta yamepandishwa hapo hapo ndani ya muda huo huo, mafuta yakishuka yanashuka kwa pesa ndogo sana ila yakipanda yanapanda kwa speed ya umeme kwa nini?

Serikali imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta kwa mfano diesel mwaka jana ilikuwa inacheza kwenye 2200 sasa 3200.

Serikali imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta na wenye sheli wamepandisha mda huo huo ila wenye vyombo vya usafiri wamepewa siku 14 wasubiri kupandisha nauli ila wenye sheli ni mda huo huo huwa hawapewi hata siku 2 ni hapo hapo yanapanda , sasa kuna mtu anaweza kuamini hii biashara haina mkono wa wakubwa kweli?
Wanasiasa wengi walioko madarakani na wastaafu ndio wamiliki wa makampuni makubwa ya mafuta na wanaimiliki serikali pia
 
Mama si alishasema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake

Acha watu wapige walibanwa kwa muda wa miaka 5
 
Yoote hayo tunayataka wenyewe watanzania, hatma ya nchi hii na maisha bora kwa vizazi vyetu ipo mikononi mwetu, wazee wetu walikosea tumefika hapa, nasi tunaboronga sijui vijana wetu wataishi namna gani huko.
 
Mbona malalamiko?

Ulipiga kura?

Ulichagua viongozi?

Wewe ni mlaji TU..

Utakula kila utachowekewa mezani..

 
Walishajua bei zinapanda kiasi kikubwa hata kabla ya kutangazwa.
.... in other words walishajipangia bei. Ilikuwa inasubiriwa siku ambayo imetamkwa na sheria kutangaza bei mpya; J4 ya mwanzo wa mwezi. Nchi itachezewa sana Samia na timu yake wasipokuwa makini.
 
Manake inashangaza kuona Viongozi kuwahi kuwaelewa hao oligopoly wa mafuta kirahisi na kwa haraka hivyo!

Yani Viongozi badala ya kustuka na kuhoji kwa kuonesha kuwiwa na concern kubwa badala yake wanaonesha kuwaelewa kirahisi hivyo kweli?

Mmnh huenda iko namna!
 
January akapewa airtime ya dk 15 bungeni akaongea utumbo ambao hata mwanafunz wa OLevel hawez changia hoja kitoto kias kile...
 
Back
Top Bottom