Naanza kuamini kuna hujuma dhidi ya Rais Samia

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
7,526
2,000
Kuna mambo yamenifanya nianze kuamini kuwa Kuna hujuma dhidi ya Rais Samia ingawa nilikuwa nikisikia tu na kutoamini huko mwanzoni. Mambo haya ni

1. Tanesco kukata Umeme hovyo nchini- Na hii ni nchi nzima, hata muda huu, umeme umekatika maeneo mengi nchini. Kalemani yuko kimya, Wizara ya Nishati wapo kimya


2. Yanayoendelea CCM. Kwa sasa huko Ccm kuna defectors , wanajulikana na motive yao inajulikana. Yaliyoandikwa kwenye gazeti la uhuru mpaka likafungiwa hayakuandikwa kwa bahati mbaya

Ushauri kwa Mama
1. Fanya kazi na loyalist wako, wanaokusikiliza na kukuheshimu. Fanyia kazi kundi linalotaka kukuhujumu. Anzia na Tanesco na Wizara ya Nishati

2. Kuna Loyalist wa Mtangulizi wako hawako tayari kufanya kazi na wewe. Piga chini weka wengine.

3. Itumie idara vizuri na wajipange vizuri dhidi ya hawa watu
 

keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,863
2,000
Yaani Mama naona anazidiwa mpaka anaenda Rwanda afu anasema tununue v8 huko.
Ni kwa Nini majeshi yake yawe msumbiji jamaa sio mtu poa kabisa
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
4,033
2,000
Ushauri wa raisi Kenyatta kwenye kuaga mwili wa hayati “raisi Samia njia umeonyeshwa na mtangulizi wako, usibadili kitu shikilia hapo hapo”.

Ametaka kuleta ubunifu wake na team mpya ngoja tuone.

She has only her self to blame huu mwanzo tu.
 

Mightier

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
5,755
2,000
Hebu tumpuzisheni Mama ( Rais ) Samia kwa kila Mtu tu Kukurupuka na Kumshauri. Alionao wa Kumshauri wanamtosha sana tu.
 

Aisha j

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
1,646
2,000
Samia kayataka mwenyewe,ilitakiwa avunje baraza lote la mawaziri,aweke watu wake,yaani wanamuhujumu kwakweli, umeme sasaivi karibia kila siku unakatika
 

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,196
2,000
Ugomvi wa kijinga na upinzani hautamsiadia Mama angeacha kufuata nyayo za hayati kwenye hili
Masoud.png

Halafu anatafutwa mchawi...maajabu haya!​
 

Rick Rick

New Member
Jul 24, 2021
3
45
Mama kisha toka kwenye natali mda tyu ni bola angefuata nyayo za mtangulizi wake jpm kwani alifanya mengi mazuri ila akija na mbinu zake kuonesha yuko tofauti nchi itamshinda zaidi hata walio andika gazeti la UHURU hawajakosea wana akili timamu itakuwa wamepata hizo tarifa sehem husika hawajakurupuka mama anataman hata ajiuzuru anavo pata lawama kila siku me kwa ushauli wangu kwa mama apumzike tu 2025 hii nchi awaachie kina MAJALIWA wanaume watuvushe
 

IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,105
2,000
Royalist indeed! Mwendakuzimu kweli alliiharibu hii nchi...yaani mtu hujui lugha lakini unalazimisha na wewe uonekane upo. Eti royalist...yale yale ya fenti ford!
Mwendakuzimu wako akikutandika akiwa hai na bado anakutandika akiwa mfu!
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,415
2,000
Kuna mambo yamenifanya nianze kuamini kuwa Kuna hujuma dhidi ya Rais Samia ingawa nilikuwa nikisikia tu na kutoamini huko mwanzoni. Mambo haya ni

1. Tanesco kukata Umeme hovyo nchini- Na hii ni nchi nzima, hata muda huu, umeme umekatika maeneo mengi nchini. Kalemani yuko kimya, Wizara ya Nishati wapo kimya


2. Yanayoendelea CCM. Kwa sasa huko Ccm kuna defectors , wanajulikana na motive yao inajulikana. Yaliyoandikwa kwenye gazeti la uhuru mpaka likafungiwa hayakuandikwa kwa bahati mbaya

Ushauri kwa Mama
1. Fanya kazi na royalist wako, wanaokusikiliza na kukuheshimu. Fanyia kazi kundi linalotaka kukuhujumu. Anzia na Tanesco na Wizara ya Nishati

2. Kuna Royalist wa Mtangulizi wako hawako tayari kufanya kazi na wewe. Piga chini weka wengine.

3. Itumie idara vizuri na wajipange vizuri dhidi ya hawa watu
Mpwa, CCM wana wimbo wao "CCM ni ile ile"!!! Hata huyu ni hao hao, huyu si ndio alisema kuwa Lissu hakupigwa risasi na Polisi, maana kwa mafunzo waliyonayo wasingemkosa
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,415
2,000
Upumbavu tu!

Kodi kwenye mafuta, mama anahujumiwa!
.
Kodi kwenye miamala, mama anahujumiwa!

Umeme kukatika, mama anahujumiwa!

Huyu mama yenu basi atakuwa ni wa hovyo sana!
Hahahaah CCM huwa hawakosi pa kutokea wakibanwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom