Naacha rasmi kusaidia wenye uhitaji

Naacha rasmi kusaidia wenye uhitaji

Zekidon

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2013
Posts
1,903
Reaction score
569
Ubinadamu kazi wakuu,

Vitendo ninavyopata toka kwa ninaowasaidia kutoka ni vya kukatisha tamaa kwa kweli.

Huyu ni mtu wa nne sasa; anahitaji ajira unampa shavu anakua na life lake lakini akishatoa matongotongo tu anaanza visa vyake.Unaonekana mjinga na mshamba tu.

Yeye ndio anajua kila kitu anajifanya kama hakujui vile kumbe wewe ndio umempa hiyo nafasi.Sasa hata nikiona nafasi mahali bora nikae kimya tu maana napata dharau toka wema wangu.

Wakuu binadamu watu hatari mno,nimekuja jua maana kama ingekua ni huyu tu nisingekua na wazo tofauti ila huyu ni wa nne kwahiyo hii ndio tabia halisi ta binadamu kwamba akishatoka anasahau kua kuna jamaa walihenyeka kumpa support mpaka kufikia hapo alipo.

Watu wabaya
 
Endelea kuwasaidi mkuu.. watakukumbuka tu hao wajinga..tena watakubebea na mazawadi kibao na kukutangaza kwenye vyombo vya habari wakitoa shukrani za kipekee kwao..ipo siku ujinga utawatoka..
 
mkuu umemshika mtu mtu mkono akiweza kutembe mwache aende na si kutegemea shukrani kwa hao watu.. kukudharau ni kosa kubwa.. ila inategemea maana ya dharau unaichukuliaje wewe.. yawezekeana wapo kawaida ila we ndiyo unaona dharau
 
Acha kuwasaidia. Bora ule hiyo hela na familia yako. Hao ndugu hawana msaada wowote.

hua napiga mapande ya ajira mkuu; wakishapata sasa huwaoni mkuu na wanageuka wajuaji. inauma sana kuona mtu umempa pande then anakugeuka baada ya kua mambo safi. kama binadamu you expect walau hata kuona ukikumbukwa kidogo inaleta faraja ila hakuna. wabongo si watu.
 
kama unaona unaumia mkuu ni bora uache kusaidia tu aisee
 
Kutafutiwa ajira sometime is a curse. Maana unashindwa kujua ni wakati gani ulipe fadhila kwa aliyekutafutia. Sa kwa watu wengine kama sisi ambao hatupendi interaction unaweza kuonekana unamdharau mtu kumbe ndo maisha yako yalivokuwa. Mi ndo maana nimeapa sitaki Kutafutiwa kazi na mtu Wakaribu maana ukipata atahic unamdharau tu.
 
hua napiga mapande ya ajira mkuu; wakishapata sasa huwaoni mkuu na wanageuka wajuaji. inauma sana kuona mtu umempa pande then anakugeuka baada ya kua mambo safi. kama binadamu you expect walau hata kuona ukikumbukwa kidogo inaleta faraja ila hakuna. wabongo si watu.

Endelea kusaidia tena kwa moyo wote...wala usitegemee chochote kutoka kwa umsaidiaye...
 
Loh kwani huwa unategemea wakufanyie nini haswa
 
unalipwa indirect ila huwezi kujua, inawezekana malipo ni kuepushwa na maradhi, ajali, kufukuzwa n.k.

Mungu mkubwa, allah akbar

we endelea kuwapa mashavu na usitegemee malipo toka kwao, hata wana wa israel walisahau kama Mungu aliyewatoa israel bado yupo na anawaona wakaamua kutengeza sanamu ya ng'ombe ndama.

waache waabudu ndama mkuu, we chapa mwendo watusulie tu.

Tumsifu Yesu kristu
 
Usiache kusaidia watu endelea hivyo hivyo,unapomsaidia mtu usitarajie atakulipa,wema unaofanya hauendi bure,atakayekulipa ni Mungu,na si leo wala kesho,inaweza kuja kutokea kwa ndugu zako au watoto wako wakaja kupata mafanikio makubwa sana ktk maisha yao,kumbe ni reflection ya wema uliowatendea wengine,unavyowasaidia watu unapanda mbegu ambayo mwisho wa siku utavuna ulichopanda,si kwamba utasaidiwa na hao unaowasaidia ila Mungu atakubariki kizazi chako chote hadi cha tano,usiumizwe na unaowasaidia then wanakubeza,malipo yako yapo kwa Mungu ambaye fedha na dhahabu ni mali yake na si binadamu ambaye ni udongo tu.
 
unalipwa indirect ila huwezi kujua, inawezekana malipo ni kuepushwa na maradhi, ajali, kufukuzwa n.k.

Mungu mkubwa, allah akbar

we endelea kuwapa mashavu na usitegemee malipo toka kwao, hata wana wa israel walisahau kama Mungu aliyewatoa israel bado yupo na anawaona wakaamua kutengeza sanamu ya ng'ombe ndama.

waache waabudu ndama mkuu, we chapa mwendo watusulie tu.

Tumsifu Yesu kristu

Ushauri mzuri sana umempa. Ubarikiwe.
 
hua napiga mapande ya ajira mkuu; wakishapata sasa huwaoni mkuu na wanageuka wajuaji. inauma sana kuona mtu umempa pande then anakugeuka baada ya kua mambo safi. kama binadamu you expect walau hata kuona ukikumbukwa kidogo inaleta faraja ila hakuna. wabongo si watu.

Post yako ya mwanzo nilielewa vizuri kwamba baada yakumsaidia amekutenga labda hata salam hakuna
Ila hii ya pili ndio nimepata picha kwamba Kumbe unataka kauli iwe Tenda wema usubiri chochote.

Hii inanipa picha kwa wewe ndio mtata,na hao watu karibia wanne unaosema unawasaidia na hakuna anaekukumba sio kweli.

Kwa maelezo yako tu ni kwamba jamaa wewe mtata saaana,yaani unampa mtu mchongo kisha yeye ndio aendeshe maisha yako?

Watu wa namna hii mpo wengi sana,na unapompa mtu mchongo sio kwamba ndio umeunda ajira mpya,au msaada wa kukusaidia majukum yako,mtu kukusaidia ni hiari yake.

Na ndio maana hao woote wanne umesema umewasaidia na kila mmoja hakukumbuki,mi nawaunga mkono kabisaaaa.
Huwezi kuchuniwa na wote wanne lazima utakuwa na mapungufu makubwa sana na kitengo chako cha MIZINGA kipo Acvtive sana,ila wewe ni MTATA
 
Kama wewe ni muamini wa hizi dini zetu...ni wapi umeahidiwa kuwa ukimsaidia mtu basi utalipwa na mtu/watu?
Mimi nadhani utarajie kulipwa na MUNGU kupitia watu ambao si lazima wawe hao uliowasaidia.

Maana hao uliowasaidia wakikulipa sasa wewe utakuwa umewafanyia wema au imewauzia wema?

Wema haulipwi na biandamu aliyefanyiwa bana
 
Wasaidie na usitarajie kitu kutoka kwao. Utakuwa na raha hata kama hawajakushukuru.
 
hua napiga mapande ya ajira mkuu; wakishapata sasa huwaoni mkuu na wanageuka wajuaji. inauma sana kuona mtu umempa pande then anakugeuka baada ya kua mambo safi. kama binadamu you expect walau hata kuona ukikumbukwa kidogo inaleta faraja ila hakuna. wabongo si watu.

Kwani Mkuu unataka wakufanyie nini? Na dharau gani wanaonyesha?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom