Naacha rasmi kununua na kulisoma Tanzania Daima hadi wazidishe uzalendo wao kwa Tanzania

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Wakati wetu huu ni kipindi ambacho watanzania tunahitaji mawazo ya kuujenga utaifa wetu ambao unatishiwa na wanasiasa wa CCM. Katika mazingira haya wasomaji wa Tanzania Daima tulitegemea makala zinazotoa mawazo na hoja za kuujenga umoja wetu na kuipenda nchi yetu kwa dhati zinapewa kipaumbele kikubwa. Moja ya makala hizo ni ile ya Mwanakijiji – Njozi ya Mwanakiji iliyokuwa inatoka katika gazeti la Tanzania Daima kila Jumatano. Makala hii ilikuwa imefikia sehemu nzuri, hasa maelezo kuhusu akina Abdalah ambao Mwalimu Nyerere amewahi kufanya nao kazi. Walikuwa wameshatajwa wachache, mmoja wapo Abdallah Fundikila, Abdallah Twalipo na nilikuwa nategemea kusoma akina Abdalla wengine. Kinachosikitisha ni kuwa makala ya namna hii imesitishwa kutolewa na Tanzania Daima. Ni jambo la ajabu kama wahariri wa Tanzania Daima hawakuona umuhimu wa Makala ile. Ama huwa hawasomi na kuona umuhimu wake. Sasa jina Tanzania Daima lina maana gani ikiwa makala zinazojenga mawazo ya U-Tanzania wanazitupa kapuni?. Tayari wasomaji wametoa malalamiko yao juu ya hilo lakini hakuna marekebisho. Somo moja ninawapa Tanzaia Daima ni kuwa katika dunia ya sasa vyombo vya habari ambavyo haviwasikilizi wasomaji na wasikilizaji wake vinakosa soko. Ndiyo maana vyombo kama BBC vimebadilika badala ya wasikilizaji kusikia tu nao wanatoa michango yao na inasikika. Na kwa njia hii ndiyo maana chombo kama Jamiiforums kinawapenzi wengi kwa kuwa mawazo yao yanasikilizwa. Kwa kusikitishwa na kitendo cha Tanzania Daima kuacha kuchapisha makala inayojenga utaifa wa nchi yetu bila sababu zinazoeleweka kwa wasomaji, kuanzia Jumatano ijayo sitanunua na kusoma tena Tanzania Daima hadi mwendelezo wa habari ya Njozi ya Mwanakijiji uendelee. Uamuzi huu ni tofauti na ule nilioufanya miaka mingi iliyopita wa kuacha kusoma Uhuru, na sasa Habati Leo, Majira nalo naelekea kulitosa. Sababu za kuacha kununua na kusoma magazeti ya Uhuru, Habari Leo na Majira ni kukithiri kwao kushiriki siasa chafu za kuliangamiza taifa letu katika misingi ya ubaguzi
 

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Umemuuliza Mwanakijiji akupe sababu za hiyo makala yake kuacha kutoka? Pengine mwenyewe kaacha kupeleka.
 

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
bila kulinunua na kulisoma utajuaje kama limezidisha huo unaouita uzalendo?
Makala husika ilikuwa inaonekana ukurusa wa mbele hivyo ni rahisi kujua ipo au haipo. Njia nyingine ni kuwapigia simu wauzaji kama hiyo makala ipo au la.
 

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Umemuuliza Mwanakijiji akupe sababu za hiyo makala yake kuacha kutoka? Pengine mwenyewe kaacha kupeleka.
Ameshajibu kuwa haelewi kwa nini makala haitoki. Ameshasema kuwa yeye ameshafika mbali sana na Njozi yake lakini Tanzania Daima wamezikalia tu.
 

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Soma uhuru, mzalendo na jambo leo.
Haya ni magazeti hovyo kabisa, ndiyo haya yanayosambaza siasa chafu za kuwagawa Watanzania kibaguzi. Hayafai yalipaswa kuwa yamefungiwa na wizara hisika siku nyingi. Lakini kwa kuwa wizara ni CCM na CCM ndiyo inayoongoza kubomoa misingi ya nchi yetu ndiyo maana yanaachwa tu.
 

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
nyie ndo mnajinyonga mkiwashika ugoni wake zenu!
Hapana ndugu, inabidi watu tuishi kwa kuongozwa na misingi fulani. Wakati huu ni wakati wa Wazalendo kuuonyesha uzalendo wao hata kama ni kwenda kinyume na mke au mume. Ulimsikia Amina Chifupa enzi za uhai wake? hakujali ndoa yake kwa maslahi ya kutetea vijana wanaoangamia kwa madawa ya kulevya
 

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
523
Mimi nlidhani njozi za Mwanakijiji kwenye TDaima zimeisha kumbe kuna jambo nyuma ya pazia! So sad.
 

BBJ

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
1,181
159
We nawe usituletee vi command vyako kama uko kwa mke wako.Hiyo sio sababu ya kuacha kulisoma Tanzania Daima, basi uwe unasoma MZALENDO, MTANZANIA etc
 

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,691
477
mkuu jaribu kuzungumza na pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi wa haraka hivyo!
 

buyegiboseba

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
535
145
Let mwanakijiji say something here to make the topic thinkerble, la sivyo tutaingia,kwenye mjadala tusio ujua kiini chake. mwanakijiji please
 

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Let mwanakijiji say something here to make the topic thinkerble, la sivyo tutaingia,kwenye mjadala tusio ujua kiini chake. mwanakijiji please

Ndugu huu siyo muda wa utani, ni wakati wa kurejesha utaifa unapokwa na CCM. Nilichosema ndicho sahihi, Mwanakijiji alishasema amefika mbali sana na Njozi yake bali hajui kwa nini haitoki. Hakuna sababu ya kudanganya ili kiwe nini?
 

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
mkuu jaribu kuzungumza na pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi wa haraka hivyo!
Nilisoma Njozi zake kuanzia mwanzo hadi mwisho, nikaridhika kuwa ilikuwa na mawazo mazuri sana na hoja za kupambana na wanaoharibu utaifa wetu. Nishasema awali mwanakijiji alishasema wazi kuwa yeye ameendelea kuandika njozi yake kama kawaida lakini Tanzania Daima hawazichapishi.
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom