Je ikitokea likaja wazo kuwa uchague kati ya kubinafsisha ardhi, bandari, mbuga, kwa uchukuaji uitwao uwekezaji na ikulu, utachagua kipi?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,720

1687385126297.png

Rais Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe kutoka Kampuni ya DP World uliongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo kutoka Falme za Kiarabu (UAE)Bw. Sultan Ahmed Bin Sulayem, wakati Ujumbe huo ulipofika Ikulu Dar es Salaam leo tarehe 17 Nov 2021 (pichani ikulu Dar).

1687385323452.png

Tangu tuanze sheria za uwekezaji aka uchukuaji, Tanzania imegeuka shamba la bibi tena linalosimamiwa na kipofu. Miaka mingi kidogo niliwahi kusoma makala moja ya mtu mmoja aliyeficha jina lake halisi lakini akaijiita Mpayukaji Msemahovyo kwenye gazeti la Tanzania Daima kwenye safu ya Kijiwe.

Siku hizi sioni makala zake nilizotokea kupenda sana. Katika uandishi wa kiutani utani aliwahi kupendekeza jeshi aliloiita geshi la Polish libinafsishwe kwa FBI. Baada ya kuisoma ile makala nilimuandikia email ambayo hakujibu nikitaka aandike makala nyingine inayotaka na Ikulu ibinafishwe ili tugawane kila mtu atafute pa kwenda na la kufanya. Mwanzoni, niliona mwandishi huyu kama chizi na asiyetumia akili.

Niliposoma between the lines, nikagundua alikuwa anachamba serikali kwa lugha ya kihuni ili kuepuka kupatilizwa au gazeti kufungiwa. Baada ya kuibuka hili sakata la bandari na waarabu, nimekumbuka sana makala hizi.

Je, tuanze na kufikiri kubinafisha ikulu maana inaonekana ni kama ka mzigo fulani? Je hawa wanaobinafsisha bandari kwa masharti ya kihuni watashindwa kubinafsisha ikulu siku moja? Naomba kutoa hoja.
 
Siku nilipoona Samia amekuwa Raisi sauti ilisikika moyoni ikisema"Hakuna mwarabu anayeweza kuaminika kwa mtu mweusi Nchi yenu imeuzwa". Samia haamini kuwa yeye ni mtu mweusi kutokana na utumwa wa fikra waolijengewa Wazanzibar hasa wapemba kuwa na wao ni waarabu eti! Huyu mtu anajua kujipendekeza arabuni kwa kutumia ardhi yetu. Tutairudisha
 
Back
Top Bottom