Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
Wakati wetu huu ni kipindi ambacho watanzania tunahitaji mawazo ya kuujenga utaifa wetu ambao unatishiwa na wanasiasa wa CCM. Katika mazingira haya wasomaji wa Tanzania Daima tulitegemea makala zinazotoa mawazo na hoja za kuujenga umoja wetu na kuipenda nchi yetu kwa dhati zinapewa kipaumbele kikubwa. Moja ya makala hizo ni ile ya Mwanakijiji – Njozi ya Mwanakiji iliyokuwa inatoka katika gazeti la Tanzania Daima kila Jumatano. Makala hii ilikuwa imefikia sehemu nzuri, hasa maelezo kuhusu akina Abdalah ambao Mwalimu Nyerere amewahi kufanya nao kazi. Walikuwa wameshatajwa wachache, mmoja wapo Abdallah Fundikila, Abdallah Twalipo na nilikuwa nategemea kusoma akina Abdalla wengine. Kinachosikitisha ni kuwa makala ya namna hii imesitishwa kutolewa na Tanzania Daima. Ni jambo la ajabu kama wahariri wa Tanzania Daima hawakuona umuhimu wa Makala ile. Ama huwa hawasomi na kuona umuhimu wake. Sasa jina Tanzania Daima lina maana gani ikiwa makala zinazojenga mawazo ya U-Tanzania wanazitupa kapuni?. Tayari wasomaji wametoa malalamiko yao juu ya hilo lakini hakuna marekebisho. Somo moja ninawapa Tanzaia Daima ni kuwa katika dunia ya sasa vyombo vya habari ambavyo haviwasikilizi wasomaji na wasikilizaji wake vinakosa soko. Ndiyo maana vyombo kama BBC vimebadilika badala ya wasikilizaji kusikia tu nao wanatoa michango yao na inasikika. Na kwa njia hii ndiyo maana chombo kama Jamiiforums kinawapenzi wengi kwa kuwa mawazo yao yanasikilizwa. Kwa kusikitishwa na kitendo cha Tanzania Daima kuacha kuchapisha makala inayojenga utaifa wa nchi yetu bila sababu zinazoeleweka kwa wasomaji, kuanzia Jumatano ijayo sitanunua na kusoma tena Tanzania Daima hadi mwendelezo wa habari ya Njozi ya Mwanakijiji uendelee. Uamuzi huu ni tofauti na ule nilioufanya miaka mingi iliyopita wa kuacha kusoma Uhuru, na sasa Habati Leo, Majira nalo naelekea kulitosa. Sababu za kuacha kununua na kusoma magazeti ya Uhuru, Habari Leo na Majira ni kukithiri kwao kushiriki siasa chafu za kuliangamiza taifa letu katika misingi ya ubaguzi