Kwangu bajeti ilifikia laki sita kwa mwezi kwa hesabu ya 20,000 kwa siku. Lakini kwasasa tangu nianze utaratibu wakujaza vitu ndani nimefanikiwa kupunguza 50% ya bajeti. Nanunua mchele 30kg. Unga 20kg. Maharage 10kg. Gesi ya 58,000. Mafuta yakula lita 5, Mkaa natokanao site hivyo nakujaga na gunia ambazo nakaanazo mpaka nasau yaani hadi miezi minne kwagunia tatu na bei ya mkaa mikoani elfu 10-13. Kama ukiwa na network na madereva wamalori wanasaidia sana kukuletea mkaa. Ila kama umepanga chumba ni bora utumie Gesi mkaa unahitaji nafasi kubwa katika matumizi yake. Vitu vyakuharibika mapema hasahasa viungo vinanuliwa kwa wiki au kila baada siku chache.
Wakati mwingine mkuu ukiona mfuko umetoboka unaforce tu watu kula maharage asietaka akalete yeye Sato.