Naacha buku 15 daily nakuta ugali na dagaa

Naacha buku 15 daily nakuta ugali na dagaa

Oyaa -unatuaibisha wnaume wenzio mkuu.
Chakufanya jizoeshe kila unaporudi kazini au kibaruani kama ni mapema pitia sokoni chukua mazagazaga yoote yanayohitajika home kwako.
Hizo dagaa anazopenda yeye,makoroti,nyanya bamia,hoho,maharagwe,samaki mbogmbogan na matunda vinavyohitajika kukaa kwenye friji viweke vyoote.alafu mwachie pesa ndogo kwa emergence tuu,buku tano inafaa sana.
Mii brother angu ndo zake hizo,mpaka mwanamke huwa anakasirika kisa haachiwi pesa.Manake kila kitu kipo mpaka hiriki.
ukifanya hivyoo mkuu tuletee feedback
lazima akakutangaze huyo.
 
Sionagi haja ya mwanamme kwenda sokoni kabisa. Huyo si mke wako, wakati wewe unajenga Roma mwenzio anajenga Babylon.

Naamini katika uwazi baina ya wanandoa, kama haupo ni tatizo la kudumu. Hizi ndio aina ya familia mke anajenga kwa siri bila mume kujua.
 
15elfu ni pesa ya matumizi kwa siku mbili,tatizo ulilonalo ndugu ni hujajua kua huyo sio mke ni mpita njia tu,au ni mtu anaetaka kuishi kitamthilia akizania yale anayoyaona kwenye tamthilia na movies ndio maisha halisi na kumbe ni usanii tu,wadada wa mjini sijui wamekuaje hawana maana hata kidogo! Kwa ushauli wangu huyo mtu piga chini tafuta mke mwema weka ndani
 
mambo mengine haya hitaji ushauri MKUU. achana na hao wanaokwambia uoe kwanza hiyo ni point nyingine kbs .

MKUU hiyo 15 nikubwa sana mm nakulaum sana kwakushindwa kumhoji na inaonekana ww huyo mwanamke ww ndio umependa kwa sana/ kakushika tawala ndio maana hupumui kwake.
huo sio uwanaume hata kidogo.
kama hufanyi kazi mpaka week end siku moja ongozana nae mpaka sokoni chukua ile ile 15 nunua vitu vyakupika utakavyo mf samaki mbogamajani viungo mchele kilo 1 na matunda uone mtatumia kiasi gani??

nunua unga kiroba mchele debe mafuta ya kupikia Lita 5 maharage hata kilo 10 samaki wakutosha wiki nzima vitunguu kisado karoti zakutosha wiki bamia nyanya n.k then kila unapotoka asubuhi mwachie 5 elf.

ujue unaweza ukawa unamraum mkeo kumbe ww mwenyewe ndio mwenye matatizo au ndio ulijitengenezea hilo bom ww kila Siku unaacha 15 kwaajili ya msosi then ukirudi unakutana na matapu tapu ya ajaabu ajabu hata huulizi ww unakandamiza 2 kesho tena unatoa 15 lazima mwanamke akuone na kukufanya msukule.
mwisho wa siku unakuja kulalamika na kulialia hapa JF tena kwakusema eti naogopa kumuuliza hivi kweli ww nimwanaume timamu kweli??
ukiambiwa nunua vitu ooo atakuona mbahili.
sasa unataka ushauri gani??
nenda basi kamsemee kwa mama yako au kwa mama yake ili amseme..

hivi ukichapiwa utalalamika?? wanawake wanapenda wanaume wenye msimamo na wenye maamuzi imara yaliyo nyooka sio legelege kama mlenda.
kashakuona hueleweki mwanaume suruali huna msimamo hujitambui ndio maana kila siku anakulisha ugali dagaaa na tembele.
yote maisha mkuu ushauri na matusi humohumo nimekuelewa lakini ila kumbuka sijamuoa
 
15elfu ni pesa ya matumizi kwa siku mbili,tatizo ulilonalo ndugu ni hujajua kua huyo sio mke ni mpita njia tu,au ni mtu anaetaka kuishi kitamthilia akizania yale anayoyaona kwenye tamthilia na movies ndio maisha halisi na kumbe ni usanii tu,wadada wa mjini sijui wamekuaje hawana maana hata kidogo! Kwa ushauli wangu huyo mtu piga chini tafuta mke mwema weka ndani
nimekuelewa asante
 
Point taken,Hapo ukute ana vikoba,finca rejesho,mchezo 10000 kila baada ya siku kumi na bado hajamodoa madera kwa fundi issa,hao ndo wanawake wa daslam bwana!

Hata kama ana michezo anaweza ana weza weka mezani chakula cha kueleweka huyo dada hajui budget na jinsi ya kubadili menu
 
Oyaa -unatuaibisha wnaume wenzio mkuu.
Chakufanya jizoeshe kila unaporudi kazini au kibaruani kama ni mapema pitia sokoni chukua mazagazaga yoote yanayohitajika home kwako.
Hizo dagaa anazopenda yeye,makoroti,nyanya bamia,hoho,maharagwe,samaki mbogmbogan na matunda vinavyohitajika kukaa kwenye friji viweke vyoote.alafu mwachie pesa ndogo kwa emergence tuu,buku tano inafaa sana.
Mii brother angu ndo zake hizo,mpaka mwanamke huwa anakasirika kisa haachiwi pesa.Manake kila kitu kipo mpaka hiriki.
ukifanya hivyoo mkuu tuletee feedback
lazima akakutangaze huyo.
nimekusoma
 
1.Chungulia uvunguni mwa kitanda utakuta kibubu.
2.Ukihoji majirani lazima atakuwa anacheza mchezo wa buku 5 kwa siku (Upatu).
3.Kuna mahali anawekeza huyo.

Nini chakufanya.
1.Ingia sokoni nunua kila kitu kwa matumizi ya wiki au mwezi mzima.
Yaani Mchele, Unga, Maharage, Samaki wakavu kwa wabichi, Viungo vyote jaza kwenye friji, Nyama na Samaki wabichi unaweza ukawa unaleta jioni ukiwa unatoka kazini. Matunda Kwa Dar sio shida unaweza kuleta mwenyewe.
Ratiba ya chakula kwamba leo tule nini inabidi mupange asubuhi kabla hujaondoka na ikitokea umesahau mwambie kabla hajapika akujulishe au akuulize leo unakula nini. Bajeti ya chakula musichanganye na bajeti ya mavazi na mengineyo. Kama kila kitu kitakuwa ndani maisha yanakuwa rahisi sana. Kila kitu kikiwa ndani unaweza kuacha 5000 na ukakuta haijatumika. vitu kama juices jijengeeni tabia yakujitengezea wenyewe za matunda kuliko kununua hizi za supermarket. Jaribu kufanya hayo kisha ulete feedback.

kuna watu mnatoa ushauri wa maana sana humu..mbarikiwe!!
 
Ulitaka ufaidi nini zaidi?
mkuu hayo mahesabu nilishapiga kitambo nilikuwa nikimpa hiyo pesa ili kumvutia asinione bahili sasa nimechoka natoa pesa nyingi alafu sifaidiki na chochote tatumia diplomatic gan
 
kuna watu mnatoa ushauri wa maana sana humu..mbarikiwe!!

Mimi kwangu HG alikuwa anapiga cha juu sasa. Sasa hivi hata nikiacha 2,000 tu anashindwa anunue nini jioni naikuta kama ilivyo. Yaani sanasana akienda gengeni labda anunue chumvi tu ingawa nayenyewe kwasasa ipo ndani nyingi mpaka anachanganyikiwa aombe pesa yakazi gani.
 
Kwangu bajeti ilifikia laki sita kwa mwezi kwa hesabu ya 20,000 kwa siku. Lakini kwasasa tangu nianze utaratibu wakujaza vitu ndani nimefanikiwa kupunguza 50% ya bajeti. Nanunua mchele 30kg. Unga 20kg. Maharage 10kg. Gesi ya 58,000. Mafuta yakula lita 5, Mkaa natokanao site hivyo nakujaga na gunia ambazo nakaanazo mpaka nasau yaani hadi miezi minne kwagunia tatu na bei ya mkaa mikoani elfu 10-13. Kama ukiwa na network na madereva wamalori wanasaidia sana kukuletea mkaa. Ila kama umepanga chumba ni bora utumie Gesi mkaa unahitaji nafasi kubwa katika matumizi yake. Vitu vyakuharibika mapema hasahasa viungo vinanuliwa kwa wiki au kila baada siku chache.

Wakati mwingine mkuu ukiona mfuko umetoboka unaforce tu watu kula maharage asietaka akalete yeye Sato.
 
tajaribu kufanya hivyo hawa wake zetu nimegundua hawana huruma kabisa wanapenda kunyonya mtu sana
 
Aisee ata Kama ningekuwa mm ningefanya the same. Kwanza hujamuoa so apo Ana buy time tu asepe so lazima ajiwekee akiba yake. Pili evi we na akili zako unaacha 15 daily ushafanya calculations kwa mwezi unampa bei gani? Kama bado basi inakutoka 450,000! Naomba nikufundishe ewe mwanaume, mwanzo Wa mwezi chukua iyo 450,000 nenda mwenyewe kafanye shopping ya vyakula nyumbani kwako, beba kila upendacho then mpelekee home uyo mchumba then daily muachie buku 5 tu ya emergency! Nakuhakikishia iyo 450,000 hautaimaliza unaeza kutumia 300,000 apo ndo umenunua hadi vitunguu!! Ebu jaribu hii

Umemaliza kila kitu mkuu asipokuelewa basi tena
 
Huyo hakupendi hata kidogooo,wanaopendwa hawafanyiwi mambo ya ajabuajabu kama hayo,KWA USALAMA WAKO MPE RED CARD MAPEMAAA KABLA HAJALAZA WANAO NJAA!
 
Back
Top Bottom