Na mimi ni banker yamenikuta

Na mimi ni banker yamenikuta

bila shaka upo access 🙂

Hapana sipo Access, kwetu tuna session za vikao kila asbh kabla hatujaanza kuwahudumia wateja. Ni ktu cha kawaida, nadhani ofisi nyingi zinafanya
 
Mang'ana Mura, Nimeupokea ushauri wako kaka. Hilo jina linafanana na mteja wangu mmoja akija lazima anitafute nimhudumie ndio maana nimekupa salaam yako stahili.

Maisha ya bankers yanakuaga ya stress,
Na sijui kwanini wadada huwa wanahisi mna mihela
Hahahaa umenikumbusha jambo...
 
Hivi wafanyakazi wote wa benki hata ma teller nao ni Bankers? Mi nilidhani owners wa hayo mabenki ndo bankers e.g kina Morgan (as in J.P. Morgan) etc. Anyway hongera banker kwa kupata kazi hivi karibuni!
 
Ungempeleka SAUT kwa mama rey wewe ukampeleka mayi hotel akajua unazo
 
Habari wana JF,

Waswahili wanasema ukiona mwenzako ananyolewa tia maji nywele zako. Kuna mdau mmoja (banker) aliwahi leta topic kuhusu masikitiko yake jinsi alivyotendwa na bint wa IFM pale Kilimanjaro Hotel.

Wadau nami yamenikuta, nami pia ni banker tena junior officer tu hapa jijini Mwanza. Hii ni ajira yangu ya kwanza na ni miezi michache tu imepita tangu nipate hiki kibarua. Here is my story.

Mimi ni mtulivu na nisiye na makuu na ni mwezi mmoja sasa tangu nifahamiane na bint mmoja mwenye asili ya bara la Asia. Amenivutia naye anaonekana kuvutiwa nami.
Kwa kuwa nimetengana na aliyekuwa mwandani wangu mwezi May nikaona sasa ni muda muafaka wa kupata mbadala wake. Tofauti na yule mdau mwingine ambaye alikua anachepuka, mimi nilikua single mpaka nilipokutana na huyo binti.

Jumamosi iliyopita yani tarehe 1 August, nilimuita Mayi Hotel nikamwaga sera zangu. Kiukweli nimempenda. Ni mpole, na ana aibu na bashasha fulani hivi ya kike. Akaniambia nisiwe na wasi wasi kama Mungu amepanga tuwe pamoja basi itakuwa.

Leo tarehe 7, nikiwa kwenye morning meeting pale job nikapokea msg ya salam mapema isivyo kawaida. Mazungumzo yakafikia baby nina shida ya pesa.Nikauliza kiasi gani, to my surprise "laki 2 na nusu". Haki ya Mungu nilihis mikono yanitetemeka na smu nikaidondosha kwenye kiti.

Hata branch manager alihisi kitu uso wangu ulivyobadlka ghafla maana tulikaa opposite na nilikua nasoma kinyemela. Nikahs labda kakosea huyu.

Anyway, 250k sometimes can not be a big deal, but within 7 days of relationship na maisha yetu yenyewe haya? Vijana wenzangu hapa mmh, hii kali.

Sikujibu mpaka kikao kilipoisha nikajitetea nilikua kikaoni. Hata hivyo niliruka hicho kibom. Nikaulizwa sasa ntatoa ngapi, to be honest niliruka tena mara ya pili. Akajifanya kunielewa.

Mpaka sasa najiuliza, hivi hawa wadada wanadhani sisi bankers tunalipwa mamilioni kama ya Escrow? Anyway, hivi ndani ya wiki moja unanipiga mzinga mkubwa hivyo? Aah kuweni fair bwana, msione bankers wana vigari, ni vya mkopo hivyo.

Nikitazama geto langu halijapendeza kiasi nipendavyo, namna hii si tunarudishana nyuma. Nitaanzisha biashara zangu kweli, ntafikia plan zangu za kutokua mwajiriwa miaka kadhaa ijayo?

Cha ajabu huyu Muasia wangu anauza duka ambalo anadai wanamiliki yeye na dada yake. Kiasi fulani ni miss independent, lakin kwanini vibom hivi. Au ndio kujaribiwa huku?

Mpaka usiku huu hatujawasiliana, tulikua na appointment kuonana jioni ya leo imefail nilibanwa na majukum lakini hata hivyo simu yangu pendwa ilipata majanga siku nzima.

Worse enough namba yangu nyingine hana nami namba zake sijakariri. Nimekuta msg zake kadhaa za hasira akijua labda ndio nimepotea mazima tangu niruke vibom vyake. Akiamka asubuhi sijui itakuaje?

Mmmh! Naomba asubuhi ifike haraka nijue mwisho wa sinema yetu. Ila kama tutawasiliana vizuri asubuhi nimepanga nimuite nimweleze hali halisi ya life langu na mambo yangu kiujumla, lazima tudefine life-mbivu na mbichi.

Nijue moja kama amekuja kwangu kuchuma bora ajitoe kabisa nami nikae chonjo. Na kama kweli ananipenda she has to agree with reality. Siwezi kuishi maisha ya kuigiza kisa mwanamke, huo ndio msimamo wangu.

Sijui kapata wapi akili za kujaribiana wakati mimi sijawahi kufanya show offs za aina yoyote kwake.
Mkuu si umchukulie mkopo tu hapo banque?maana yeye anajua zipo na mnavyojua kuoga ninyi watu wa bank,muko kama ndugu zangu wakongo man kwa kuoga na kujipodoa tu hamjambo
 
Sio kila mtu wa Asia kwao kuna mabasi,wengine njaa tuu
 
Sipo Access dada yangu, nipo na benki moja yenye asili ya Kenya. Kwa wiki moja simpi. Kesho atakuja nyegez ninapoishi lazima nimsort

ahaaaa KCB Aahaaaa jirani na nmb kenyata ok siku moja mtakubamba hapo nilinganishe maneno yako. Umesema unaitwa nani vile???
 
Muda si mrefu atatua nilipo, ntaleta mrejesho hapa.

Mmmmh!! Huo utakuwa umbea sasa, mwanaume amepewa kifua atiiii!!! Sasa wavulana wa siku hizi kila kitu cha ndani mnaanika!!
 
huyo ni mfano wa wale wajipangao usiku,na itakuwa ivo,fuatilia utabaini.
 
Back
Top Bottom