Na mimi ni banker yamenikuta

Na mimi ni banker yamenikuta

Pole sana ndugu. Ila "Bankers" wengi ni kweli hawana hela, wanaunga unga sana. Mimi siyo "Banker" ila ilishanikutaga. Niliombwa pesa na msichana mmoja niliyemotokea ili akafanyie biashara. Aliniomba Milioni1. Sikubishana nae, sikuonesha kushtushwa, wala sikumuliza maswali mengi, baada ya siku mbili nikampa. Akashukuru sana. Baada ya wiki mbili akanirudishia hela yangu yote na kuniambia hakuwa na shida nayo alikuwa ananipima tu.
 
Pole sana ndugu. Ila "Bankers" wengi ni kweli hawana hela, wanaunga unga sana. Mimi siyo "Banker" ila ilishanikutaga. Niliombwa pesa na msichana mmoja niliyemotokea ili akafanyie biashara. Aliniomba Milioni1. Sikubishana nae, sikuonesha kushtushwa, wala sikumuliza maswali mengi, baada ya siku mbili nikampa. Akashukuru sana. Baada ya wiki mbili akanirudishia hela yangu yote na kuniambia hakuwa na shida nayo alikuwa ananipima tu.

Hii nayo stori nzuri ya kujifunza inawezekana nayeye anajaribiwa....avunje tu kibubu
 
mambo ya kuombana hela kwakweli hayafai basi tu hawa dada zetu hawajielewi, yaani unakuta mtu hata kazi hafanyi, kutwa kujipodoa, yaani k ndo kitega uchumi chake
 
Habari wana JF,

Waswahili wanasema ukiona mwenzako ananyolewa tia maji nywele zako. Kuna mdau mmoja (banker) aliwahi leta topic kuhusu masikitiko yake jinsi alivyotendwa na bint wa IFM pale Kilimanjaro Hotel.

Wadau nami yamenikuta, nami pia ni banker tena junior officer tu hapa jijini Mwanza. Hii ni ajira yangu ya kwanza na ni miezi michache tu imepita tangu nipate hiki kibarua. Here is my story.

Mimi ni mtulivu na nisiye na makuu na ni mwezi mmoja sasa tangu nifahamiane na bint mmoja mwenye asili ya bara la Asia. Amenivutia naye anaonekana kuvutiwa nami.

Kwa kuwa nimetengana na aliyekuwa mwandani wangu mwezi May nikaona sasa ni muda muafaka wa kupata mbadala wake. Tofauti na yule mdau mwingine ambaye alikua anachepuka, mimi nilikua single mpaka nilipokutana na huyo binti.

Jumamosi iliyopita yani tarehe 1 August, nilimuita Mayi Hotel nikamwaga sera zangu. Kiukweli nimempenda. Ni mpole, na ana aibu na bashasha fulani hivi ya kike. Akaniambia nisiwe na wasi wasi kama Mungu amepanga tuwe pamoja basi itakuwa.

Leo tarehe 7, nikiwa kwenye morning meeting pale job nikapokea msg ya salam mapema isivyo kawaida. Mazungumzo yakafikia baby nina shida ya pesa.Nikauliza kiasi gani, to my surprise "laki 2 na nusu". Haki ya Mungu nilihis mikono yanitetemeka na smu nikaidondosha kwenye kiti.

Hata branch manager alihisi kitu uso wangu ulivyobadlka ghafla maana tulikaa opposite na nilikua nasoma kinyemela. Nikahs labda kakosea huyu.

Anyway, 250k sometimes can not be a big deal, but within 7 days of relationship na maisha yetu yenyewe haya? Vijana wenzangu hapa mmh, hii kali.

Sikujibu mpaka kikao kilipoisha nikajitetea nilikua kikaoni. Hata hivyo niliruka hicho kibom. Nikaulizwa sasa ntatoa ngapi, to be honest niliruka tena mara ya pili. Akajifanya kunielewa.

Mpaka sasa najiuliza, hivi hawa wadada wanadhani sisi bankers tunalipwa mamilioni kama ya Escrow? Anyway, hivi ndani ya wiki moja unanipiga mzinga mkubwa hivyo? Aah kuweni fair bwana, msione bankers wana vigari, ni vya mkopo hivyo.

Nikitazama geto langu halijapendeza kiasi nipendavyo, namna hii si tunarudishana nyuma. Nitaanzisha biashara zangu kweli, ntafikia plan zangu za kutokua mwajiriwa miaka kadhaa ijayo?

Cha ajabu huyu Muasia wangu anauza duka ambalo anadai wanamiliki yeye na dada yake. Kiasi fulani ni miss independent, lakin kwanini vibom hivi. Au ndio kujaribiwa huku?

Mpaka usiku huu hatujawasiliana, tulikua na appointment kuonana jioni ya leo imefail nilibanwa na majukum lakini hata hivyo simu yangu pendwa ilipata majanga siku nzima.

Worse enough namba yangu nyingine hana nami namba zake sijakariri. Nimekuta msg zake kadhaa za hasira akijua labda ndio nimepotea mazima tangu niruke vibom vyake. Akiamka asubuhi sijui itakuaje?

Mmmh! Naomba asubuhi ifike haraka nijue mwisho wa sinema yetu. Ila kama tutawasiliana vizuri asubuhi nimepanga nimuite nimweleze hali halisi ya life langu na mambo yangu kiujumla, lazima tudefine life-mbivu na mbichi.

Nijue moja kama amekuja kwangu kuchuma bora ajitoe kabisa nami nikae chonjo. Na kama kweli ananipenda she has to agree with reality. Siwezi kuishi maisha ya kuigiza kisa mwanamke, huo ndio msimamo wangu.

Sijui kapata wapi akili za kujaribiana wakati mimi sijawahi kufanya show offs za aina yoyote kwake.

Yaani kelele zote hizi ni kwaajili ya 250k tu? Usione vyaelea kaka...tafuta wa saiz zako
 
Mm kuna demu alikuwa anajua tunalipwa mamilion sijui kusikia nafanya kaz kampuni kubwa ya simu ...nikamletea salary slip...akaona deduction ya mkopo wa nyumba naokatwa....akachoka....nilimwambia mm take home laki 4 tu
 
Sukari Yenu

ahaaaaaaa uko bank gani? Mmm hapa mwanza bank yenye wakaka wa njaa ni access bank.hongera sana.

Wadada wenzangu kuweni makini na wakaka wa benk! Ukishaamua kujitoa mwanga basi hata meneja ila hawa muwaacha kwanza watafte maisha.

Bi dada kawai sana binafsi siwezi omba hela natengeneza mazingira ya kupewa kiroho swafi.

Ushauri, wewe mpe afu msikilizie kama atarudia tena.
Sipo Access dada yangu, nipo na benki moja yenye asili ya Kenya. Kwa wiki moja simpi. Kesho atakuja nyegez ninapoishi lazima nimsort
 
Last edited by a moderator:
Movie inaendelea, asubuhi aligoma kabisa kupokea smu yangu wala kujibu msg. Mida ya mchana akaanza kunijibisha, kesho atakuja nyumbani kwangu nitazungumza nae kwa kirefu.
 
Waarabu na waasia wanapenda sana huo mchezo wajaribu sana na kukusema kwa watu wa karibu Ombi langu kwako tafuta mdada wa mbali asiejua kazuli yako halisi fanya nae mahusiano taratibu bila kujua kama wewe ni banker.
Unatafutaje MTU Wa mbali mkuu? Unaweza kumuamini? Naona ugumu kweli! Nile somo briefly.
 
Kuombwa pesa ooh mapema oooh just 7 days of a relationship, mbona papuchi ukipewa huoni kama ni mapema wajipakulia tu jamani....pole lakini

Evelyn Salt
Wewe binafsi waweza fanya kama hivyo? Mimi papuchi kwenye uhusiano mpya siombi, atatoa mwenyewe. Nitamtengenezea mazingira ya kunipa bila kuomba. I have the techniques.
 
Waarabu na waasia wanapenda sana huo mchezo wajaribu sana na kukusema kwa watu wa karibu Ombi langu kwako tafuta mdada wa mbali asiejua kazuli yako halisi fanya nae mahusiano taratibu bila kujua kama wewe ni banker.

Achaar, mapenzi ya mbali yalinishinda na ndio kisa cha kuachana na aliyekua mwandani wangu wa mwanzo.
Mimi siwezi kumficha mwanmke life yangu. Atanyooka tu kama kweli ananipenda.
 
Back
Top Bottom