Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,151
- 137,136
- Thread starter
- #101
Umesema sana lakini it is all about your Signature; Miafrika ndivyo tulivyo.
Hata nawe umeandika sana ujue....
Na hii ni kwa sababu tumelishwa kasumba mbaya na nchi za magharibi zikihesabiwa sambamba na USA.
Nchi za Mashariki hazijatulisha hiyo kasumba mbaya?
Tunaamini katika hizo tu.
Ni wazi si wote mnaoziamini.
Lakini naomba uwasaidie wanajukwaa kufahamu ni kwa nini usiku na mchana SK na USA hawapumui wanapoilinda Military Demarcation line kati ya hawa blood related Nk & SK.
North Korea wao wanapumua? Kwa taarifa yako nao hawapumui kwa kujua kuwa taifa kubwa lipo karibu kuilinda South Korea endapo huyo mwehu ataleta chokochoko na ndo maana kila siku hao NK hawaishi kuwatukana viongozi wa Marekani.
Muulize Japan pamoja na kwamba vita kati yake na NK iliicha NK hohe hahe na bado NK karudi kuwa tishio katika ukanda wao.
Zaidi ya mikwara huyo NK kaifanya nini Japan? Aivamie basi tuone kama kweli yeye ni gangwe.
Muulize USA alijibu nini wakati NK alipomuhakikishia kuwa pamoja kuipiga SK ana uwezo wa kutandika nuke moja kwa moja katika ardhi ya USA.
Alihakikisha kwa vitendo ama kwa maneno? Aliivamia hiyo South Korea? My dad always told me that 'well done is always better than well said'. So until actually they do it their bark remains to be worse than their bite.
Ni wazi nchi zote zinapiga propaganda sana japokuwa ni wazi nchi za Magharibi ukihesabu na USA kwa kutumia media zao zimetufanya "Miafrika kuwa kama tulivyo" . Hatuambiwi wala hatusikii kuhusu "wakubwa" hawa. And we don't argue.
Mbona hapa mpo mnao-'argue'....?
Mataifa kama Russia, China, Irani, North Korea and the like; wanaiambia USA waziwazi kuwa wanauwezo wa kupambana nae kwa kujua kuwa pamoja na kwamba watashusha nuke katika ardhi yake pia wana uwezo wa kutandika katika ardhi ya swaiba zake hasa watakao host upuuzi wowote wa USA.
Well done is always better than well said. Hata Saddam Hussein aliyasema yote hayo but where is he now?
Na hii ni kwa sababu moja kubwa kwamba na wao wanahitaji resources zao na nyinginezo ziwasaidie wao kwa maendeleo yao kama apendavyo USA katika maendeleo yake.
And......?
So, kwa hilo mataifa hayo yanpofikia hapo hayana utani na ardhi yao hata kama angekuja "kiranja" USA.
USA haanzishi vita tu bila sababu.
Hebu niambie ni nchi gani katika Afrika itamtunishia msuli USA?
Zimbabwe.
North Korea ilimwambia ataitazama kama "kuku anavyomtazama na kumtamani mende aliyeko kwenye kioo kigumu kabisa..."
Ilimwambia lini? Na tayari nishasema hapa kuwa NK haina mpinzani kwenye propaganda na fiery rhetoric (mikwara). Na ndicho kitu pekee wanachokiweza.
Katika google utapata habari za NK lakini kwa uhondo na mapana zaidi pitia kwa uchache vitabu vya the Great Leader Kim IL Sung...viko vingi sana and Do that home work. Ukimaliza rudi hapa tuendelee kwa pamoja.
Oh please! I have better things to do than read fictional narratives about the Hermit Kingdom.