The same old primitive discussion,this proves that there is lack of relevant knowledge about international politics.Watu wanazungumza kwa kasumba na ushabiki bila hata kujijua.Ubongo wao umefungwa kujua ukweli ulivyo kuhusu siasa za dunia.Mimi sipingi watu kufahamu taarifa kama hizi,ila nashauri watu wajitahidi kupanua mawazo yao mbali zaidi nje ya maistream media,hapo ndipo mtakapojua ukweli.
-Ushabiki wa kwamba nani ana nguvu za kijeshi zaidi ya mwingine utatusaidia nini?
Hebu ngoja tuone na wewe umeandika nini.
-Kuna watu wanasema NK inaongozwa kidikteta,je hawa watu wanajua kwamba marekani ni dikteta na gaidi namba moja duniani?
Nitajie dikteta mmoja wa Marekani, tafadhali. Na katika kufanya hivyo weka kabisa na fasili ya neno 'dikteta' ili tuweze kupata msingi mzuri wa hoja.
Hakuna nchi hata moja duniani inayoongozwa kwa demokrasia,kama kweli mnajua maana ya demokrasia.
Wewe unaijua maana ya demokrasia? Kama unaijua tueleze basi na si wengine ambao umedokeza kuwa hatuijui.
-Kuna watu wanasema kwamba watu wa NK hawapigi kura kuchagua kiongozi wao,je watu hawa wanajua kwamba raisi wa marekani hachaguliwi na wananchi wa marekani bali anawekwa na matajiri ambao hasa ndio wanaoongoza marekani ili kutimiza agenda zao?
Hao matajiri ni akina nani [wataje majina yao] na agenda zao ni zipi[ziorodheshe ukiambatanisha na vyanzo]?
Na una ushahidi gani kuwa rais wa Marekani "hachaguliwi na wananchi wa marekani bali anawekwa na matajiri ambao hasa ndio wanaoongoza marekani"?
Na kama raisi hafuati maagizo ya matajiri hao anaondolewa madarakani
Madai makubwa kama haya huhitaji ushahidi mkubwa na madhubuti. Lete vyanzo na ushahidi wa haya madai yako.
au anauawa,remmember JF kennedy?
Kennedy aliuwawa na hao matajiri kwa sababu hakufuata maagizo yao? Okay, sawa, lete ithibati ya madai yako hapa.
-Kuna mtu anasema NK inaongozwa na familia moja tu,je huyu mtu anajua marekani anayoishabikia kama inaongozwa na familia za watu wasiozidi saba na maraisi wa marekani kama vile Obama ni watumwa tu wa hizo familia?
Zitaje hizo familia saba ukiambatanisha na ithibati madhubuti.
-Kuna watu wanasema NK inafanya wananchi wake kama watumwa,je hawa watu wanajua kama marekani wanafanya watu karibu wa dunia nzima kuwa watumwa hasa nchi zetu za kiafrika?
Kabla ya kwenda mbali, tuanze na fasili ya neno 'utumwa'. 'Utumwa' ni nini? Baada ya hapo lete ushahidi wa Marekani kuifanya dunia nzima kuwa watumwa hasa hizi nchi zetu za Kiafrika.
-Hivi watu wanafahamu vizuri kweli historia ya NK na SK na kwa nini ziko katika hali hii tunayoiona leo?
Wewe unaifahamu? Kama unaifahamu na unaona siye wengine hatuifahamu, tufahamishe basi kile ambacho wewe unakifahamu ambacho siye hatukifahamu.
Au tunaongea kwa ushabiki tu?
Kama kuna aliyeandika kishabiki tu basi wewe ndo unaongoza kwani hujatoa ithibati, ki/vidhibiti, wala ushahidi wowote ule kuambatana na madai yako ya kipuuzi kabisa uliyoyatoa.
-Hayo maswali ni sehemu ndogo tu ya mambo ambayo watu wanatakiwa kuyajua na si propaganda za vyombo vya habari vya magharibi ambavyo hurubuni akili za watu kila kukicha.
Nchi za Mashariki zenyewe hazina propaganda zinazorubuni watu wenye akili kama zako? Manake kama kuna mhanga wa propaganda basi wewe utakuwa juu kwenye orodha ya watu hao.
-Nashauri tupende kutafuta habari nje ya mainstream ambapo ndio mambo yaliyojificha hufunuliwa.
Wapi huko? Kwenye mitovuti ya ma conspiracy theorists, birthers, truthers, holocaust deniers, na kadhalika? Huko ndiko ulipoyatoa hayo ma conspiracy theory yako uliyoyatapika humu? Unachekesha!
Tuache ushabiki usio na tija kwa kuwa ipo siku mtu ataathirika kwa kukosa taarifa sahihi.
Tatizo la washabiki ni kuona watu wengine kuwa ni washabiki na wao kutokujiona kuwa ni washabiki. Mambo ya projection hayo!!
Mfano:Kwa uelewa huu niliuona hapa watu wenye kasumba nilizoainisha hapo juu wana uwezekano mkubwa sana kwamba wanajua HIV/AIDS haina tiba ilihali tiba ipo lakini hawajui kwa sababu ya kung'ang'ania ushabiki wa kijinga kwa marekani.
HIV/ AIDS ina tiba? Iko wapi hiyo tiba yake? Nani anayo? Na wewe umejuaje kuwa ipo? Ulipata AIDS ukaitafuta na kuitumia halafu ukapona?
Najua kuna watu wataniona mm kichaa,
Teh teh teh....walau umejistukia mapema. Maana kwa huu utumbo ulioutapika hapa sidhani kama ungekuwa na akili timamu ungefanya hivyo.
fuatilia haya kwanza ndipo utagundua kwamba hao wamarekani mnaowashabikia wamefanya blunder ya karne kwenye hili la HIV/AIDS.
Blunder gani hiyo ya karne ambayo Wamarekani wameifanya?
Watu wanaoshabikia marekani inabidi wafahamu kwamba hao tunaowasifia ndio wanasababisha leo hii waafrika na maeneo mengine wanakufa kama kuku kwa magonjwa yanayotibika(kansa/saratani,kisukari,AIDS nk) na vita vya wenyewe kwa wenyewe.Amkeni,we real need to RE-LEARN.
Wewe hebu wahi ukamwone daktari wa magonjwa ya akili kabla hujajidhuru au kudhuru wengine!!
ni mmoja wa watu ambao watakuwa wamenielewa vizuri maana anaonekana anajua vizuri siasa za marekani.
Pwa! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Inawezekana hujajiita hilo jina lako [Deception] kwa bahati mbaya.
GO USA :usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2: GO!