Paka akiwa mnene ni paka wa kizungu,paka akikondeana ni paka wa kiswahili,
Kuku anayewekwa mahali safi,analindwa,ni kuku wa kizungu ila wale wanaorandaranda wa kienyeji
Mtu akiwa anajali muda msafi ,ana. pesa -yule jamaa mzungu sana hana longolongo kabisa hanaga uswahili kabisa
Lakini mtu muongo,hajali muda ni mswahili-ah yule jamaa mswahili sana maneno mengi,tapeli nk
Mbwa akiwa na mkia mnene,manyoya ni mbwa wa kizungu ila vimbau mbau,wabaya wa kiswahili
Kwenye mabishano au mtu akisifiwa utasikia mimi sini mzungu ,mie siyo mswahili(tapeli tapeli,muongo muongo,hajali muda) kama wewe