Mzungu ni nani?

MIDFIELD

JF-Expert Member
May 27, 2013
1,944
702
Habari za mwisho wa juma wakubwa.

Kuna swali mwenzenu huwa linanisumbua naomba nililete kwenu tusaidiane kupeana majibu. "Hivi kwa kiswahili neno MZUNGU lina maanisha nini. Ni mtu yeyote mweupe, au mtu toka Uingereza, Ujerumani, Ulaya kwa jumla, Mmarekani kaskazini/kusini, mchina, mkorea, mwarabu, mrusi, mwisrael au ni mtu wa namna gani hasa. Hebu naombeni tusaidiane tafadhali
 
Babu zetu,kpnd cha ukoloni,walitumia Neno muzungu kutamka kama lijitu jeupe.Na hawakutamka kwa maana Nzuri,kwa sabb wazungu walikuwa wakiwatesa na kuwanyanyasa Babu zetu(sote twajua.) Basi katika kupeana taarifa Babu zetu walitamka Li-Muzungu limekuja/yamekuja(kwa Ki lugha).Basi wanataarifiana kwa namna hiyo kisha.wanakmbia ama kujifcha.Kama ilivyo kwa kpnd hiki Vijana wakiwa vijiweni(wavuta bangi na Madawa)Mmoja wapo anapowaona Askari Polisi au w/jeshi wao husema ma Mwela hao/huyo au Mjeda/wajeda hao/huyo,wootewanatimua Mbio.
Bas Ndivyo ilivyokuwa kwa babu zetu walitamka Muzungu kisha wanatimua mbio.na hata watoto wadogo walitimua mbio,kwa maana hawajwahi kumwona Mtu mwny ngoz nyeup.
Ama kama Mtemi katembelewa wananchi wanajificha kwanza Taarfa watazipata kwa Chief/Mtemi wao.Mara baada ya Mzungu kuondoka.
 
Sina hakika sana ila kuna mahali nilisoma wanasema hata neno : mungu, limetokana na mulungu, aka mzungu. Sa sijui ndugu yangu
 
Mzungu = European

Kama hiyo ndio maana je watu wafuatao ni wazungu?

Danny Welbeck (mchezaji wa Arsenal mwenye uraia na utaifa wa Uingereza na Uingereza ni sehemu ya Ulaya)...

Zinedine Zidane (mchezaji wa zamani wa Real madrid mwenye uraia na utaifa wa Ufaransa na Ufaransa ni sehemu ya Ulaya)...

na wengineo wafananao na hao
 
Babu zetu,kpnd cha ukoloni,walitumia Neno muzungu kutamka kama lijitu jeupe.Na hawakutamka kwa maana Nzuri,kwa sabb wazungu walikuwa wakiwatesa na kuwanyanyasa Babu zetu(sote twajua.) Basi katika kupeana taarifa Babu zetu walitamka Li-Muzungu limekuja/yamekuja(kwa Ki lugha).Basi wanataarifiana kwa namna hiyo kisha.wanakmbia ama kujifcha.Kama ilivyo kwa kpnd hiki Vijana wakiwa vijiweni(wavuta bangi na Madawa)Mmoja wapo anapowaona Askari Polisi au w/jeshi wao husema ma Mwela hao/huyo au Mjeda/wajeda hao/huyo,wootewanatimua Mbio.
Bas Ndivyo ilivyokuwa kwa babu zetu walitamka Muzungu kisha wanatimua mbio.na hata watoto wadogo walitimua mbio,kwa maana hawajwahi kumwona Mtu mwny ngoz nyeup.
Ama kama Mtemi katembelewa wananchi wanajificha kwanza Taarfa watazipata kwa Chief/Mtemi wao.Mara baada ya Mzungu kuondoka.

Aisee, kwa hiyo kwa ufupi walimaanisha ni mtu mweupe toka nje ya afrika bila kujali katoka bara/nchi gani. good
 
Habari za mwisho wa juma wakubwa.

Kuna swali mwenzenu huwa linanisumbua naomba nililete kwenu tusaidiane kupeana majibu. "Hivi kwa kiswahili neno MZUNGU lina maanisha nini. Ni mtu yeyote mweupe, au mtu toka Uingereza, Ujerumani, Ulaya kwa jumla, Mmarekani kaskazini/kusini, mchina, mkorea, mwarabu, mrusi, mwisrael au ni mtu wa namna gani hasa. Hebu naombeni tusaidiane tafadhali
Asili ya neno haijulikani kikamilifu.
Inaonekana kuna uhusiano na neno mzungu / mizungu lisilo kawaida tena katika Kiswahili cha kisasa lakini limetunzwa katika kamusi za Kiswahili zilizokusanya maneno yao mnamo mwaka 1900. Lilimaanisha mambo mbalimbali kama vile 1) kitu cha ajabu au cha kushangaza, 2) mbinu wa kujiondoa katika tatizo, 3) aina ya muhogo, 4) silika au akili ya wanyama.[SUP][2][/SUP] Waswahili waliwahi kutumia neno "mzungu" kwa "akili" na pia kwa mafundisho ya "unyago" yaliyoitwa "kufundishwa mizungu".[SUP][3][/SUP]. Kama asili ya "Wazungu" iko hapa iliweza kumaanisha "watu wa ajabu, wasio kawaida, wenye mbinu nyingi" au "wageni walio tofauti sana".
Wengine wamehisi kwa utani ya kwamba kuna uhusiano na kitenzi "kuzunguka" na "mzungu" ilitaka kutaja tabia ya wapelelezi, wamisionari na wafanyabiashara wa kwanza kutoka Ulaya ambao hawakukaa mahali pamoja bali kuzungukazunguka kote Afrika.
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
All the credits to Wikipedia...

Asili ya neno haijulikani kikamilifu.
Inaonekana kuna uhusiano na neno mzungu / mizungu lisilo kawaida tena katika Kiswahili cha kisasa lakini limetunzwa katika kamusi za Kiswahili zilizokusanya maneno yao mnamo mwaka 1900. Lilimaanisha mambo mbalimbali kama vile 1) kitu cha ajabu au cha kushangaza, 2) mbinu wa kujiondoa katika tatizo, 3) aina ya muhogo, 4) silika au akili ya wanyama.[SUP][2][/SUP] Waswahili waliwahi kutumia neno "mzungu" kwa "akili" na pia kwa mafundisho ya "unyago" yaliyoitwa "kufundishwa mizungu".[SUP][3][/SUP]. Kama asili ya "Wazungu" iko hapa iliweza kumaanisha "watu wa ajabu, wasio kawaida, wenye mbinu nyingi" au "wageni walio tofauti sana".
Wengine wamehisi kwa utani ya kwamba kuna uhusiano na kitenzi "kuzunguka" na "mzungu" ilitaka kutaja tabia ya wapelelezi, wamisionari na wafanyabiashara wa kwanza kutoka Ulaya ambao hawakukaa mahali pamoja bali kuzungukazunguka kote Afrika.
 
Sina hakika sana ila kuna mahali nilisoma wanasema hata neno : mungu, limetokana na mulungu, aka mzungu. Sa sijui ndugu yangu

Aisee, neno Mulungu nadhani linatumiwa na makabila mbalimbali ya kibantu likimaanisha Mungu
 
Habari za mwisho wa juma wakubwa.

Kuna swali mwenzenu huwa linanisumbua naomba nililete kwenu tusaidiane kupeana majibu. "Hivi kwa kiswahili neno MZUNGU lina maanisha nini. Ni mtu yeyote mweupe, au mtu toka Uingereza, Ujerumani, Ulaya kwa jumla, Mmarekani kaskazini/kusini, mchina, mkorea, mwarabu, mrusi, mwisrael au ni mtu wa namna gani hasa. Hebu naombeni tusaidiane tafadhali

Ninavyoelewa mimi ni kuwa ''mzungu'' kiingereza chake ni Caucasian. Hawa ni wa watu wenye ngozi nyeupe wanaoishi Ulaya na USA. Mfano ni wajerumani, wadachi au waswidi. Lakini watu weusi wanaozaliwa huko bila kuwa na ngozi au nywele za kizungu eg Obama sio wazungu. Kadhalika wachina (na wote wenye sura za kimongolia eg wajapani, wakorea) wahindi, machotara, waamerika kusini kama wabrazil, waajentina na waarabu SIO wazungu. Hivyo basi mzungu ni mtu ambaye yuko kama George Bush au Wayne Rooney. Kama hujaishi Ulaya au USA ni vigumu sana kuona tofauti zao lakini kwa mtu ambaye ameishi sehemu hizo ni rahisi kabisa kutenganisha.
 
Hata wahindi, wachina ni wazungu maana ni weupe na wana nywele ndefu
 
Ninavyoelewa mimi ni kuwa ''mzungu'' kiingereza chake ni Caucasian. Hawa ni wa watu wenye ngozi nyeupe wanaoishi Ulaya na USA. Mfano ni wajerumani, wadachi au waswidi. Lakini watu weusi wanaozaliwa huko bila kuwa na ngozi au nywele za kizungu eg Obama sio wazungu. Kadhalika wachina (na wote wenye sura za kimongolia eg wajapani, wakorea) wahindi, machotara, waamerika kusini kama wabrazil, waajentina na waarabu SIO wazungu. Hivyo basi mzungu ni mtu ambaye yuko kama George Bush au Wayne Rooney. Kama hujaishi Ulaya au USA ni vigumu sana kuona tofauti zao lakini kwa mtu ambaye ameishi sehemu hizo ni rahisi kabisa kutenganisha.

Daaa! e bwana kweli penye wengi pana mengi, mkuu macho_mdiliko nimeipenda sana comment yako, hasa ulivyosema ,..'...wale wote wenye sura za kimongolia km wajapan ....'. Hizi bila shaka ni sura kama za mviringo hivi! hahahaaaaa. Good
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom