Mzumbe yasafisha PhD feki; Kamala na Nchimbi wajifua upya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzumbe yasafisha PhD feki; Kamala na Nchimbi wajifua upya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu66, Nov 14, 2009.

 1. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MAWAZIRI wawili wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, miongoni mwa sita waliotajwa kujipa wasifu wa elimu wasiyokuwa nayo, wameanza kutekeleza mkakati wa kujisafisha.

  Tayari imethibitika kuwa Diodorus Kamala, waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki na Emmanuel Nchimbi, ambaye ni naibu waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa (JKT), hivi sasa wanasomea shahada ya uzamivu ya falsafa (Ph.D) katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.

  Kamala na Nchimbi ambao walikuwa wakiitwa na kujitaja kwa kiambishi cha Dk., walisajiliwa na chuo hicho mwaka jana. Kamala ni mbunge wa jimbo la Nkenge, mkoani Kagera kupitia CCM. Kabla ya kuwa waziri alikuwa mkufunzi chuoni hapo.

  Nchimbi ni mbunge wa Songea Mjini, mkoani Ruvuma. Wote wawili wanafanya mafunzo yao chini ya wakufunzi watatu tofauti.

  Wakati Kamala anasimamiwa na Profesa Joseph Kuzilwa, Nchimbi anasimamiwa na Dk.

  Benedict Lukanima aliyemaliza shahada yake ya juu nchini Uingereza mwaka huu.

  Dk. Lukanima anasaidiana na Dk. Matiku ?€œkumfua?€? Nchimbi. Mafunzo hayo yanafanywa kwa mtindo wa utafiti, MwanaHALISI imegundua.

  ?€œKama waliogopa au walizembea kusoma na kuamua kujipa sifa ambazo hawana, unadhani hivi sasa watasoma kweli??€? ameuliza mwanafuzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ambaye aliomba kutotajwa jina.

  Nchimbi alipoulizwa na MwanaHALISI kwa nini ameamua kusoma shahada hiyo ya juu wakati yeye tayari anatajwa na kujiita mwenye shahada ya uzamivu (Dk), alikataa katakata kuzungumzia suala hilo.

  ?€œMimi siwezi kuzungumza na wewe, mwambie bosi wako?€?(Kubenea, Saed) anipigie simu na kuniuliza,?€? alisema Nchimbi.

  Alisema, ?€œSizungumzi na kila mtu. Nazungumza na marafiki zangu, hapo kwenu rafiki yangu ni Kubenea?€?,?€? alisema na kukata simu.

  Chuo Kikuu cha Mzumbe kimekwenda mbali zaidi katika kuwashughulikia wenye vyeti vyenye utata kwa kuwakana na kuwavua wasifu wa elimu waliothibitika kutokua nao.

  Wakufunzi 12 wamevuliwa wasifu wa shahada ya uzamivu katika fani mbalimbali.

  Pamoja na Kamala aliyekuwa mkufunzi kwenye chuo hicho kabla hajawa waziri, kitabu cha maelezo ya chuo kikuu hicho, ?€œProspectus?€? cha mwaka 2007/2008, kinaonyesha kuwa walikuwa na shahada za uzamivu lakini katika vitabu cha mwaka 2008/2009 inaonyeshwa kuwa wamevuliwa.

  Awali Kamala alitambuliwa na chuo hicho kuwa ana shahada ya uzamivu kutoka chuo kikuu huria cha Commonwealth. Hivi sasa ameishia kuwa na shahada mbili na kurejea kwenye uanafunzi.

  Haijafahamika serikali inaweza kuchukua hatua gani kuhusu taarifa zao za muda mrefu kuwa wana shahada za uzamivu; bali wachunguzi wa mambo wanasema, katika mazingira ya kisiasa, mawaziri hao wamekumbwa na kashfa inayoweza kuwapokonya nafasi zao.

  ?€œItategemea Rais Kikwete analionaje hilo; lakini anastahili kulichukuliwa kwa uzito unaosta
  hili kwani linaathiri hadhi yake na ya serikali yake.

  Hao tumewasikia; je, wamo wangapi wa aina hiyo,?€? ameeleza Profesa Mshiriki kutoka chuo kikuu cha Mzumbe.

  Katika mkakati wa kutambua na kuchukua hatua zinazostahili, Chuo Kikuu cha Mzumbe kimeonyesha kutotambua shahada za uzamivu za baadhi ya wakufunzi.

  Miongoni mwao ni Profesa Moses Warioba ambaye alitambuliwa kuwa na shahada ya uzamivu ya utawala, sasa ?€œshahada?€? yake hiyo haitambuliwi, imeeleza prostectus ya chuo.

  Christopher Sotta, alitajwa kuwa ni Dk. mwenye shahada ya uzamivu ya utawala lakini sasa imekanwa.

  Dk. Raphael Habi alitambuliwa kuwa na shahada ya uzamivu ya uongozi tofauti na sasa ambapo hatambuliwi hivyo na chuo hicho.

  Awali Arstarch Kiwango alitambulishwa kuwa na shahada ya uzamivu ya uchumi. Sifa hiyo sasa imeondolewa. Naye Dk. Colman Riwa, aliyekuwa anajitambulisha kuwa na shahada ya uzamivu ya utawala, amenyang?€™anywa hadhi hiyo.

  Mwaka 2007/2008, chuo hicho kilimtaja Leonard Shio kuwa ni Profesa mwenye shahada ya uzamivu ya utawala. Siku hizi hatambuliwi hivyo.

  Wengine waliotajwa na chuo hicho kuwa wana shahada za uzamivu bila kutaja vyuo walikozipata ni pamoja na Mujwahuzi Njunwa. Shahada yake ya uzamivu ilielezwa kupatikana nchini Marekani. Kwa sasa ?€œimefutika.

  Prosper Ngowi alitajwa kuwa na shahada ya uzamivu ya Uchumi na Biashara; sasa haitambuliki; wakati Benard Nsana aliyetambulishwa na chuo kuwa ana shahada ya uzamivu, sasa hatambuliwi kuwa nayo.

  Gabriel Elisante alikuwa anatajwa kuwa na shahada ya uzamivu ya masoko (Marketing) kutoka nchini Finland; sasa hatambuliwi hivyo.

  Naye Didas Mrina alinadiwa na kujinadi kuwa ana shahada ya uzamivu ya biashara kutoka nchini Marekani, lakini sasa hanadiki hivyo tena.

  Swali kubwa ambalo wengi wanajiuliza ni kwa nini imechukua muda mrefu kugundua hivyo. Aidha, ni kwa nini walimu wanapoomba kazi, hawaelezi vyema vyuo walikosomea na lini ili utawala uweze kufuatilia mkondo wa elimu yao.

  ?€œMwanaharakati?€? Kainerugaba Msemakweli, amekuwa akitoa hadharani orodha ya majina ya watu, wakiwemo mawaziri, ambao anadai hawana digrii wanazodai kuwanazo.
  Msemakweli anadai amepata taarifa hizo kwa njia ya utafiti na kwa msaada wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU).


  Chanzo:
  Mwanahalisi
   
 2. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Still Phd ya Mzumbe ni feki!Kwa nini Kamala na Nchimbi wasifanye UDSM?
  Muda gani wanasoma wkati ni wabunge?
  Huyo lecture wa Mzumbe atapewa pesa za ufisadi
   
 3. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Basi kuanzia sasa wasiitwa mdkt.ni aibu mtu kama nchimbi eti dk? mara kumi kamala ana uwezo kishule sio kilaza nchimbi -darasani ni hamna kitu kabisa.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Nov 15, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mzumbe is not accredited university
  angalieni TUC website!

  Habari ndiyo hiyo!
   
 5. R

  Raia Member

  #5
  Nov 15, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh, hii hatari kuna jina hapo nimeliona la Elisante Gabriel nami nilikuwa nafahamu anatambulika kama DR. Kwa mwendo huu hakuna tunachoweza kujivunia kwani hata wale tunaoona ni role model wetu baadhi yao elimu zao ni za mashaka. Tuwe wakweli katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.
   
 6. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Yoyo na masanilo mko wapi? mnatukashifu sisi watu wa madrasa kumbwe nyinyi mnakomba ma Phd feki.kashfa nzito
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mushobozi, Nungwi mko wapiiii?.........nawapongeza wanataaluma wa Mzumbe kwa hatua waliyochukua.......
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Elisante alianzia Madrasa kabla ya kuslimu na kuwa mkristu! hahahahaha kanda2 mchokozi ww!
   
 9. A

  Aviseniamarina New Member

  #9
  Nov 17, 2009
  Joined: Dec 8, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aibu, Mzumbe bado wa full registration bado hawajakuwa accredited for this long, vyuo vilivyo kuja nyuma Kama Hubert Kairuki are already accredited but MU not!!. Degree nyingi ni za ch.u.p.i na feki tupu, naamini hata hao walionyang'anywa PhD bila shaka hata Masters hawana kama itafuatiliwa itagundulika tu.
   
 10. M

  Middle JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2009
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  UFEKI UMEANZA pale wakati wanatoa Degree,siamini mtu kama Riwa au Mrina walikuwa Madk jamani.
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwani UDSM ndo nini?
   
 12. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hii ni aibu kwa Taifa watawala pamoja na TCU. Hili jambo linaonekana kuwa la kawaida katika jamii yetu ya kitanzania. Watu 12 ni wengi sana, nilitegemea TCU iitishe mafaili na vyeti vya waadhiri Tanzania nzima kuhakiki degree zao hili kuondoa aibu hii.

  Lakini wakati wa sakata la Msemakweli ilionekana hata CEO wa TCU alionekana kutolipa uzito kabisa na kukwepa maswali ya waandishi kuwa yeye hajamtuma Msemakweli afanye uchunguzi.

  Hii ni sawa sawa na kupeleka mhalifu polisi halafu polisi wakakukimbia.
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ilishathibika kuwa walikuwa na degree feki . Je hili sio kosa kisheria? Mbona hazichukuliwi hatua na mamlaka zinazohusika?
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  TUC yenyewe nayo ni feki na haiko accredited
   
 15. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  A public official, better yet an elected one, apparently said that.

  Sijui atakapoenda kuomba kura nako atazungumza na rafiki zake tu?
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  Nimeona wana jengo jipa karibu na rose garde nikadhani ndo watakuwa na meno kabisa ya kufutilia mbali huu ujinga!
   
 17. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Nimejaribu kufungua website ye CTU hapa naona, hii ni dakika ya kumi sasa bado inafunguka!
   
 18. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mtu mwenye akili sawa hawezi kufoji PhD, sioni kama hata hawa walioenda kusoma kama wanaelewa kwa nini wanahitaji hiyo PhD.
   
 19. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Naomba msaada jamani, inakuwaje vyuo vingine hata majina hatuvijui viko accredited wakati Mzumbe chuo kikubwa tena cha serikali bado kiko kwenye level ya Full Registration? Je uzembe wa viongozi wa chuo au ni kitu gani? Haingii akilini eti Chuo kinaitwa Stefani Moshi Memorial University kiko Moshi kiwe accredited, halafu Mzumbe bado.

  Kuna chuo kilikuwa sekondari ya Mazengo zamani pale Dodoma, sasa hivi kinaitwa St. John's University nacho kiko accredited tayari. Mzumbe vipi? Ni tatizo la Mzumbe au TCU?

  http://www.tcu.or.tz/universities.html
   
 20. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Wanahitaji PhD ili majina yao yatanguliwe na title ya Dr. Kwa kuwa wao sio wanamuziki au wasanii maarufu, ni vigumu kuipata hiyo title. Hawana tofauti na wanamuziki kina Dr. Remmy Ongalla, Prof. Jay, Ispector Haroun, Luteni Kamala, Sir Nature na wengine waonaofanana na hao!
   
Loading...