Mzumbe University hamjielewi, badilikeni

Mzumbe University hamjielewi, badilikeni

mchapafito

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2013
Posts
607
Reaction score
302
Habari za asubuhi GT wa JF.

Kuna suala kuhusu hiki chuo mimi kama mzazi ninayesomesha kijana wangu pale MU nashindwa kuelewa...nina kijana wangu amemaliza mwaka wa kwanza wiki iliyopita....kituko kinakuja eti likizo wiki 1

i.e siku saba anaingia mwaka wa pili jumatatu ya wiki hii na inatakiwa afanye process zote za registration na ikumbukwe zote hizi zina involve money...sasa nashindwa kuelewa kama mzazi iweje nilipe ada pamoja na gharama zingine pasi kujua matoleo ya kijana angu.....Je chuo hakioni kama hakitutendei haki sisi kama wazazi....

Siombei hili but what if kuna mwanafunzi akadisco nao ndo washasema alipe ada tayari for 2nd year....je itarudishwa???...najua wadau wa elimu mpo humu na MU officials huwa mnapita huku.....tafadhali liangalieni hilo suala katika jicho la tatu
 
Tulia mzazi kwani Mzumbe ni chuo makini sana Tanzania, wewe fanya process zote then kila jambo litaenda vizuri na kama mwanao alikuwa anacheza kombelela chuo basi ajiandae kwa vilio pia.
 
Wee mzazi pia nawe hujielewi...mbona livyopumzika karibia miezi 3 haujaja humu kusema kapumzika sana!!! Lipa ada uangalie mambo mengine kama kacheza utarudishiwa fedha yako na hata ukimuuliza mwanao anajua kama kafeli au kapasua hapo alipo...
 
Vijana Shardcole na Maukiddo mbona hamjajibu swali langu....Je ni utaratibu wa wapi interval ya mwaka wa kwanza na wa pili iwe siku saba ?
 
Tulia mzazi kwani Mzumbe ni chuo makini sana Tanzania, wewe fanya process zote then kila jambo litaenda vizuri na kama mwanao alikuwa anacheza kombelela chuo basi ajiandae kwa vilio pia.
no thank you,

mimi nilikuja majuzi tu nikiwa nimemsindikiza mdogo wangu kufanya registration, kila kitu hovyo, very disorganized.

ukifika unakutana na ASK ME wawili. nikawataka wanielekeze utaratibu mzima.

wao wakanielekeza swala la kuweka mabegi tu, maelezo mengine sikupata nikaona tangazo kubwa linamaelezo kwa first year, basi nikasoma hayo na kujua sasa tayari, tukaingia holini na kupanga mstari.

tulipofika meza ya registration na nyaraka kupitiwa tukaambiwa tulipie hela ya TCU tukalipa,

tuliporudi ndani tukiwa tumelipa kwa huyo mhudumu akatuambia yeye hahusiki kwa registration yetu, akatuelekeza kwingine kabisa.

sasa nikawa najiuliza, INA MAANA HAO ASK ME KAZI YAO NI IPI? AMA HAWAJIELEWI? AMA WAMEWEKWA WATU WASIOFAA?

maana niliwataka wanielekeze utaratibu mzima. kama walijua registration zimegawanyika hivi ama vile wangenielekeza.

nikaona isiwe shida.

nikaenda huko.

tukapokelewa.

nikaulizwa kwa nini mmechelewa maana ilikuwa jioni.

nikamwambia tulikuwa kwenye hall kubwa ila tukaambiwa mpaka tulipe ada ya TCU.

yule mhudumu akashangaa, akauliza "ni nani huyo anayewaambia mlipe hela ya TCU?,

watu wengine wanafanya mambo hata hayapo hivyo"

hapa nikaanza kujiuliza tena ,ni nani ansema ukweli kati ya huyu ama yule aliyenitaka nikalipe? jibu sina ila lazima mmoja hayuko sahihi. nikagundua kuna dosari nyingine hapa.


palepale nikauliza kitu kwa mhudumu mwingine akanielekeza niende sehemu fulani. nilipofika huko hola,

nikarudi ndio nikapewa maelekezo sahihi.

yaani ni tabu tupu mpaka nilikasirika kweli.

kila kitu kilionekana hakiko kwenye utaratibu na mpangilio unaofaa.
 
Vijana Shardcole na Maukiddo mbona hamjajibu swali langu....Je ni utaratibu wa wapi interval ya mwaka wa kwanza na wa pili iwe siku saba??
hii ni aibu, watajibu nini, ukiwa unatetea kitu cha kijinga unahitaji kujivika umwehu na kujitoa fahamu.

huu ni ujinga kweli.

yaani na hicho chuo eti kina viongozi wasomi wanakaa wanapanga ujinga huu na degree zao,masters zao,phd zao na uprofesa wao.

hao wamejitoa fahamu
 
Wee mzazi pia nawe hujielewi...mbona livyopumzika karibia miezi 3 haujaja humu kusema kapumzika sana!!! Lipa ada uangalie mambo mengine kama kacheza utarudishiwa fedha yako na hata ukimuuliza mwanao anajua kama kafeli au kapasua hapo alipo...
inahitaji umwehu kutetea ujinga huu wa mzumbe.

yaani likizo ya kubadili mwaka ni siku saba? matokeo hayajatoka usharudi na kuanza kusoma? this is more than silly.

lazima ujivike umwehu wa kiwango cha hali ya juu kama wewe kuweza kutetea upuuzi huu.
 
Katika hilo nakubaliana na wewe kabisa mkuu 100% mwaka jana nilipokua naenda kumpeleka huyu kijana aliengia 2nd year juzi i faced the same problem yaani poor organizatiom...inakua as if chuo kimekurupushwa kupokea hao wanafunzi kwa maana wanakua hawajajiandaa kabisa....na katika hilo la mapokezi na vijana wa 'ASK ME'

Napenda kuwasifu UDSM wamejitahidi sana katika hilo..kuna mpwa wangu nilimpeleka wiki iliyopita kuanza masomo pale kwa kweli nililidhika na huduma ya pale mlimani...tukirudi katika suala hili la MU sio siri inabidi wajipange upya kwa kweli...

Binafsi kijana angu alipangiwa sehemu ya maradhi NYIRENDA...yaani panatia huruma its like an old deserted haunted house huko ndo wanatuwekea vijana wetu..sijui MU wanawaza nini katika hilo lakini naamini kuna watu makini officials wa MU wanapita humu naomba muondoe hiyo aibu jamani...MU sio chuo cha kufanya hayo kabisa.
 
inahitaji umwehu kutetea ujinga huu wa mzumbe.

yaani likizo ya kubadili mwaka ni siku saba? matokeo hayajatoka usharudi na kuanza kusoma? this is more tha silly.

lazima ujivike umwehu wa kiwango cha hali ya juu kama wewe kuweza kutetea upuuzi huu.

Hilo ndo limeniacha hoi kabisa likanifanya hadi labda ni google vyuo vya wenzetu sehemu mbalimbali duniani wanafanyaje katika suala zima la kuingia academic year nyingine..yaani siku 7 seriously???...na hapo matokeo hata hayajatoka si ajabu hata kuna walimu hawajaanza marking...

Sasa kwa kijana anyeishi MUSOMA kwa mfano.. ndani ya hizo siku saba aende na kurudi kwao plus wazazi watafute ada.... wazazi wanajipangaje katika situation kama hiyo ? ... MU mnajiabisha katika hili suala jaribu kubadilika naongea kama mzazi SIJAPENDEZWA KABISA.
 
Kuna mdogo wangu kachaguliwa certificate hapo, ila kaugua na lushindwa kufika wakati wa registration, natarajia kumleta next week, sijui watasumbua?
 
Vijana Shardcole na Maukiddo mbona hamjajibu swali langu....Je ni utaratibu wa wapi interval ya mwaka wa kwanza na wa pili iwe siku saba??

Mzumbe ina utaratibu wa likizo moja ndefu sana baada ya kumaliza semester ya kwanza kwa sababu wanafunz wengu venue chache.. so chuo hakina uwezo kuwaacomodate wanafunzi wote kwa pamoja so inabid wapisha... sasa kuna semester waita stagard ndo hiyo mwanao kaimaliza baada ya hapo ili kuwahi semester mpya likizo uwa ni wik 2 maxmum... mwanafunzi anarud na kuingia mwaka wa pili ili awahi kalenda, so sio ajabu mzumbe ni chuo makini na weled mkubwa sana tuliobahatika kusoma pale tunajivunia
 
Last edited by a moderator:
Mzumbe ina utaratibu wa likizo moja ndefu sana baada ya kumaliza semester ya kwanza kwa sababu wanafunz wengu venue chache.. so chuo hakina uwezo kuwaacomodate wanafunzi wote kwa pamoja so inabid wapisha... sasa kuna semester waita stagard ndo hiyo mwanao kaimaliza baada ya hapo ili kuwahi semester mpya likizo uwa ni wik 2 maxmum... mwanafunzi anarud na kuingia mwaka wa pili ili awahi kalenda, so sio ajabu mzumbe ni chuo makini na weled mkubwa sana tuliobahatika kusoma pale tunajivunia

Binafsi nimekaa kimya kwa sababu sioni cha kukujibu ingali nliuliza swali...je alivyokaa nyumbani miezi mi3 ulikuja humu kuuliza au unakurupuka tuu kuhoji likizo ya wiki 1...kwa uelewa wangu inaonyesha unampenda sana mwanao ukae nae nyumbani...
 
Katika hilo nakubaliana na wewe kabisa mkuu 100% mwaka jana nilipokua naenda kumpeleka huyu kijana aliengia 2nd year juzi i faced the same problem yaani poor organizatiom...inakua as if chuo kimekurupushwa kupokea hao wanafunzi kwa maana wanakua hawajajiandaa kabisa....na katika hilo la mapokezi na vijana wa 'ASK ME' napenda kuwasifu UDSM wamejitahidi sana katika hilo..kuna mpwa wangu nilimpeleka wiki iliyopita kuanza masomo pale kwa kweli nililidhika na huduma ya pale mlimani...tukirudi katika suala hili la MU sio siri inabidi wajipange upya kwa kweli...binafsi kijana angu alipangiwa sehemu ya maradhi NYIRENDA...yaani panatia huruma its like an old deserted haunted house huko ndo wanatuwekea vijana wetu..sijui MU wanawaza nini katika hilo lakini naamini kuna watu makini officials wa MU wanapita humu naomba muondoe hiyo aibu jamani...MU sio chuo cha kufanya hayo kabisa

ni kweli kabisa, mimi mwenyewe nilipeleka rafiki yangu udsm mwaka jana. kwanza ukifika wale ask me ni wengi karibu kila kona ukihitaji usaidizi unapewa na maelezo wanatoa kwa kina, na wao watakuuliza pia na si kusubiri kila kitu waulizwe maana wanajua nini kinapaswa kufanyika kwa wanafunzi wa aina ipi, na lini na wapi ,mpaka na maelezo ya ziada unapata. lakini pale ni hovyo
 
Huo ndo UJUHA wa MU we ushawahi kuona wapi chuo interval ya mwaka wa kwanza na wa pili iwe wiki moja???

Mwambie aweke wazi hatua zote alizopitia kijana wake tangu aanze first year!

Kuna kipindi baadhi ya kozi wanakuwa nyumbani ambao hawaku join second semester moja kwa moja.

Hawa hurudi baadaye wakati wengine wakiwa likizo ya July-Oct.

Hichi ndicho kipindi ambacho nao husoma. Hivyo hutakiwa kuendelea na second year hapo hapo hivyo hupewa likizo ya wiki 1
 
Huo ndo UJUHA wa MU we ushawahi kuona wapi chuo interval ya mwaka wa kwanza na wa pili iwe wiki moja???
nyie si ndoo mnadanganya wadgo zetu kuwa mzumbe ndo chuo bora ,chuo kama college bwanah
 
Back
Top Bottom