Mzumbe Secondary Alumni

Mzumbe Secondary Alumni

Joined
May 14, 2015
Posts
22
Reaction score
5
Mzumbe Secondary Alumni ni umoja unaowaunganisha watu wote waliosoma shule ya secondari Mzumbe tangu ilipoanzishwa.

Lengo la thread hii ni kupost matukio mbalimbali yanayohusu shughuli za alumni hii.

Kuchangia shughuli za alumni tumia akaunti hii,
Account name: MZUMBE SECONDARY SCHOOL ALUMNI
Account number: 10100705678
BANK: Akiba Commercial Bank
SWIFT Code: AKCOTZTZ

NOTE: You can also transfer money to the bank account using MPESA/Tigo Pesa/Airtel Money.

Karibuni tuonyeshe uzalendo kwa vitendo...
 
Ee bwana elezea kwa ukubwa zaidi lengo la michango hiyo na wewe ni nani na vipi tutakuamini. waliosoma Mzumbe wengi ni watu werevu na wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kutenda na wapo kwenye nafasi kubwa kubwa. kwa hali hii sio rahisi kuchangia hata wenye nia kama mimi kwani hakuna security yoyote. tafadhali tatua maswala haya kwanza kabla ya kuendelea
 
Ee bwana elezea kwa ukubwa zaidi lengo la michango hiyo na wewe ni nani na vipi tutakuamini. waliosoma Mzumbe wengi ni watu werevu na wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kutenda na wapo kwenye nafasi kubwa kubwa. kwa hali hii sio rahisi kuchangia hata wenye nia kama mimi kwani hakuna security yoyote. tafadhali tatua maswala haya kwanza kabla ya kuendelea

Fazili,
Asante kwa interest yako ya kutaka kujua zaidi juu ya hii alumni.
Kwenye thread hii utajua mengi kwa vile ni thread endelevu.
Hivi sasa napata shida jinsi ya kuupload picha kwenye ukurasa hii. Bado sijajua tatizo ni nini.
Unaweza kupata taarifa kuhusu alumni hii kupitia facebook kwenye group inayoitwa Mzumbe High School au WAZUMBE.

Mwenyekiti wa Alumni ni ndugu Eddy Talawa. Huyu ni mtu anaheshimika katika jamii. Katika graduation iliyopota ya form six, yeye ndio alikuwa mgeni rasmi.

Kwa hiyo hii sio organisation ya ujanjaujanja. Iko kihalisia na inalenga kugive back to the comunity.

Once again, asante kwa kuuliza...
 
Ukarabati Mzumbe.jpg
Vyoo vya wanafunzi Mzumbe Sekondari. Vyoo hivi vimekarabatiwa kwa michango ya wanachama wa Mzumbe sec. alumni.
vilikabidhiwa rasmi kwa wizara ya elimu kwenye mahafali ya kidato cha sita yaliyofanyika April 25 2015.
 
Kabla ya ukarabati.jpg
Hali ya vyoo vya shule ni mbaya. Ukarabati unaendelea kuhakikisha Mzumbe sekondari inaondokana na hali hiyo ili huweka mazingira mazuri kwa masomo.

Picha hii inaonyesha hali ya choo kabla ya ukarabati.
 
ujenzi unaendelea.jpg
Ukarabati unaendelea.
Kazi hizi za ukarabati zinafadhiliwa kwa michango ya waliosoma Mzumbe sekondari.
 
ukarabati ndani.jpg
Ukarabati wa majengo ya choo unafanyika ndani na nje.
Kuta ziwekewa tiles ili kuwakinga wanafunzi na ugonjwa wa ZONGWE ambao uliathiri wanafunzi wengi wa shule hiyo.
Ugonjwa huu huathiri kende na kuzichuna. Kuepuka ugonjwa huu ni sehemu ya kuboresha MAZINGIRA ya kuwapatia wanafunzi elimu bora.
 
tayari bado.jpg
Pichani jengo la choo linalokarabatiwa na jengo ambalo litakarabatiwa baada ya hili kukamilika.
Kazi hii ya iukarabati ni endelevu. Imeanza na vyoo, itaendelea pia kwenye miundombinu mingine ya shule ya Mzumbe.
 
Mhagama.jpg
Mwanachama wa alumni, Emmanuel Mhagama, akitathmini jengo ambalo litaanza kukarabatiwa hivi karibuni.
Pamoja na kuchanga pesa, wanachama pia wanajitolea kusimamia kazi za ujenzi.
Jumuiya ya wazumbe inatambua hali hiyo kama Mzumbe spirit...
 
graduation.jpg

Wanachama wa Mzumbe sec. alumni walipohudhuria mahafali ya kidato cha sita tarehe 25.04.2015. Katika mahafali hayo, alumni ilitoa zawadi kwa wanafunzi wote waliofanya vizuri kwenye nyanja mbalimbali pamoja na kukabidhi majengo yaliyokarabatiwa.
Mwenyekiti wa alumni nd. Eddy Talawa alikuwa mgeni rasmi.
 
Msuka.jpg
Mkuu wa shule mstaafu mwalimu Msuka akiwa na wanachama wa alumni kwenye mahafali ya kidato cha sita.
Mwalimu Msuka ndiye aliyekuwa mkuu wa shule wa kwanza baada ya shule ya sekondari Mzumbe kupewa hadhi ya shule ya watoto wenye vipaji maalum...
 
Hongereni sana, huu ni mfano wa kuigwa.

Kutoka kuwa walalamikaji na kuwa waleta masuluhisho ya matatizo yaliyopo, hii ndio njia ya kwenda.

Nimehamasika, nami nitacopy na kupaste hiki mlichofanya kwenye shule ya kijijini kwangu bila kuwa na nia ya kupata kitu in return kama wanafiki wengi wanaofanya haya kwa show tu za kutafutia ubunge au udiwani.

Hongereni sana
 
Back
Top Bottom