Mzimu wa "Bunge Live" wamwandama Nape

Mzimu wa "Bunge Live" wamwandama Nape

Mr Pm ivi karibuni alisema kusitishwa kurushwa kwa matangazo ya bunge live kutafanya wafanyakazi wafanye kazi zaidi...ok may be is good idea lakini nashauri to drive home your point..television zilizopo kwenye maofisi ya serikali ziuzwe ilifedha zitumike kununulia komputa katika shule zetu za kata.

Duuuhh, mbona kazi ipo. Kwenye kujibu Maswali ya wabunge nilimsikia Naibu Waziri Ngonyani na Waziri wa viwanda wakisema, naomba kumnukuu, "naomba kuwaagiza watendaji wote kuwa kuanzisha sasa wachukuwe haya niliyoongea kama maagizo na wakatekeleze".

Sasa wafanyakazi ambao hawatakiwi kuona bunge live wanaendaje kutekeleza maagizo ambayo hawana fursa ya kuyasikia.
 
Mtu anaweza kukuonesha kuwa hakutaka kwa kukutaka uwe mtetezi wa ujinga. Nape kapewa kazi ya kuutetea ujinga wa kutorusha Bunge live. Mwisho wa yote ujinga wote uliomo katika uamuzi huu ataubeba Nape hata kama maamuzi hayakuwa ya kwake pekee yake.
 
MZIMU WA ‘BUNGE LIVE’ WAMWANDAMA NAPE

Mzimu wa kuzuia shughuli za Bunge kuonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni uliopachikwa jina la ‘Bunge Live’, umeendelea kumwandama Waziri wa Habari, Nape Nnauye baada ya juzi kupokewa kwa kelele kiasi cha kushindwa kuhutubia wapenzi wa muziki jijini Mwanza.

Nape alitangaza uamuzi wa kusitisha kurusha moja kwa moja baadhi ya shughuli za Bunge, akisema Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linashindwa kumudu gharama, lakini wabunge, hasa kutoka vyama vya upinzani wamepinga hatua hiyo wakisema inawanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kupata habari kuhusu chombo chao cha kutunga sheria.

Lakini Serikali imeshikilia msimamo wake, ikitoa sababu tofauti na kwenda mbali zaidi kuzuia vituo binafsi vya televisheni kurusha matangazo, huku TBC1 ikirusha kipindi cha maswali na majibu pekee ikielezwa kuwa huo ni uamuzi uliopitishwa katika Bunge la 10.

Leo tarehe 24th May 2016 ZBC iko Live kurusha matangazo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Nimejiuliza ni kwanini lenyewe liwe Live na Bunge la JMT liwe gizani! Tutafakari pamoja. ....au kwa sababu BLW is like a single party parliament!
 
Lumumba wakija hapa hawana hoja nikuanza kutoa lugha chafu tu mkuu
 
Najaribu kuwaza kwanini TBC 1 warushe kipindi cha maswali na majibu LIVE kwa kodi zetu ilhali kuna Television zingine ambazo zingeweza kurusha bunge live kwa gharama zao.

Dhana ya kubana matumizi imekaa kimaigizo zaidi ya uhalisia

This government is not serious at all'

#BringBackBungeLive

kipindi cha maswali na majibu ndio kipindi ambacho serikali haipati kashikashi,inakuwa imejiachia.Ninachojiuliza,muda huo watu wanakuwa hawapo makazini?Waziri mkuu alitoa sababu ya kazi,amewadanganya watanzania ambao wanaujua ukweli
 
CCM na serikali yake Imeishiwa pumzi , muda si mrefu itakata roho
 
Duuuhh, mbona kazi ipo. Kwenye kujibu Maswali ya wabunge nilimsikia Naibu Waziri Ngonyani na Waziri wa viwanda wakisema, naomba kumnukuu, "naomba kuwaagiza watendaji wote kuwa kuanzisha sasa wachukuwe haya niliyoongea kama maagizo na wakatekeleze".

Sasa wafanyakazi ambao hawatakiwi kuona bunge live wanaendaje kutekeleza maagizo ambayo hawana fursa ya kuyasikia.
Si unajua mtu akikaribia kufa anaanza kuongea mambo yasoeleweka. Ndo ilivyo kwa hii serikali
 
Mr Pm ivi karibuni alisema kusitishwa kurushwa kwa matangazo ya bunge live kutafanya wafanyakazi wafanye kazi zaidi...ok may be is good idea lakini nashauri to drive home your point..television zilizopo kwenye maofisi ya serikali ziuzwe ilifedha zitumike kununulia komputa katika shule zetu za kata.
Kama issue ni watu kufanya kazi basi wasirushe live kipindi cha maswali na majibu maana muda huo watu wanakua kazini badala yake waanze kurusha live kuanzia saa kumi jioni watu wanakuwa wameshatoka maofisini
 
Mzimu wa kuzuia shughuli za Bunge kuonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni uliopachikwa jina la ‘Bunge Live’, umeendelea kumwandama Waziri wa Habari, Nape Nnauye baada ya juzi kupokewa kwa kelele kiasi cha kushindwa kuhutubia wapenzi wa muziki jijini Mwanza.

Nape alitangaza uamuzi wa kusitisha kurusha moja kwa moja baadhi ya shughuli za Bunge, akisema Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linashindwa kumudu gharama, lakini wabunge, hasa kutoka vyama vya upinzani wamepinga hatua hiyo wakisema inawanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kupata habari kuhusu chombo chao cha kutunga sheria.

Lakini Serikali imeshikilia msimamo wake, ikitoa sababu tofauti na kwenda mbali zaidi kuzuia vituo binafsi vya televisheni kurusha matangazo, huku TBC1 ikirusha kipindi cha maswali na majibu pekee ikielezwa kuwa huo ni uamuzi uliopitishwa katika Bunge la 10.

Juzi, Nape aliyekuwa mgeni rasmi katika tamasha la Jembeka Festival lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, alipokewa na kelele za maneno “Bunge Live” wakati akikaribishwa kuhutubia mamia ya wapenzi wa burudani waliohudhuria tamasha hilo, ambalo lilijumuisha wasanii nyota kama Shaffer Chimere Smith a.k.a Ne-Yo kutoka Marekani na Diamond Platnum.

Baada ya mkurugenzi wa kampuni ya Jembe ni Jembe, Sebastian Ndege kumkaribisha waziri huyo kuzungumza na wananchi hao, Nape alisimama lakini akapokewa kwa kelele.

“Bunge live, Bunge live, Bunge live,” walipiga kelele mashabiki waliohudhuria tamasha hilo.

Kelele za “Bunge Live” zilisababisha Waziri Nape kushindwa kuhutubia na kulazimika kuketi chini na Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula alisimama kujaribu kuokoa jahazi, lakini naye akakumbana na kimbunga cha sauti za wananchi walioamua kulitaja jina la mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Ezekia Wenje.

“Wenje, Wenje, Wenje,” wananchi hao waliimba kwa sauti wakati Mabula akijaribu kuwatuliza ili Nape ahutubie.

Akizungumzia tukio hilo, Nape alisema wananchi waliompigia kelele za “Bunge Live” walisukumwa na masuala ya kisiasa, ndiyo maana aliepuka kuendelea kuzungumza ili kutochafua hali ya hewa uwanjani.

“Pale uwanjani tulikwenda kwa ajili ya burudani, sasa baada ya kuona wananchi wanaanza kuleta masuala ya kisiasa nikaona ni busara kuacha kuhutubia. kuepusha shari,” alisema Nape.

Pamoja na Nape, tamasha hilo pia lilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Mabula.

Ukiachilia mbali dosari hizo, tamasha hilo lilikonga nyoyo za wapenzi wa sanaa ya muziki waliokesha uwanjani hapo hadi saa 11:00 alfajiri wakiburudishwa na wasanii nguli.

Wasanii wengine waliopata nafasi ya kutumbuiza ni Juma Nature, Ney wa Mitego, Ruby na Fid Q.
 
Nape, ulikwenda Mwanza kwa ajili ya burudani, lakini ulisahau kwamba wananchi hawana amani na mauaji mnayoyafanya kwa kivuli cha bunge na dniyo sababu hamtaki watu waone. Kuna budurani pasipo amani?

Nape, uliacha kuhutubia kwa sababu watu waliingiza siasa, siasa gani tena ya kukusumbua wakati Mwanza CCM mna wafuasi wa kutosha waliowafanya mshinde kwa kishindo? Wametoka wapi tena hao wapinzani hadi kukuzuia usihutubie jamani? Utakuwa umekosea tathmini.

Nape, Unaweza kuteganisha namna gani siasa na maisha ya watu ya kila siku ikiwa katika siasa ndiko mfumo wa maisha yao, kwamba walime nini, waimbe nini wacheze nini, wavae nini, wapite kushoto, wakose sukari, wapate wapi mahitaji, wasome nini, wazike wapi, watibiwe wapi na waishije, ndiko unakosindikwa?

Ulitaka wasahau adha zote kwa sababu ya hotuba yako ambayo sidhani kama ungehutubia usingegusia siasa. Sasa ninashukuru wnanchi wa Mwanza wamekuonyesha kisogo mwonekano wa kisogo chako.

NINAOMBA USIJIFARIJI KWA HLI BALI LICHUKLIE KAMA SOMO KWA NAMNA MNAVYOENDESHA SERIKALI, MATUMIZI YA DOLA NA MAHAKAMA NA UMUHIMU WA KUJALI WATU KATIKA UTAWALA HATA KAMA NI MISUKULE.
 
Ni vema Nape awe anahudhuria mikusanyiko yenye uhakika ya kuwa na makada wengi wa CCM.
 
Back
Top Bottom