Mzimu wa "Bunge Live" wamwandama Nape

Mzimu wa "Bunge Live" wamwandama Nape

Wananchi wa mwanza heshima kwenu mmefanya vizuri tunataka bunge live siyo porojo nyingi. Kama serikali PM inasimamia kwenye haki inaogopa nini bunge kurushwa live?
 
Nimeishi huko,hakuna watu wasioangalia Bunge kama wao.
Sasa watu kupenyeza Siasa za kitoto,wangejua kwamba Tamasha hilo ni muhim kwa Wasanii wa kwao wasingefanya ujuha huo kwa pesa za Pombe.
Biashara imekweisha,wakikuwa wataancha,bado watoto na ushamba ni Janga pia.Maana mhhh nakujua huko
Angekuwa Waziri mwingine angepata shida,lakini Mtoto wa Mjini Nape,ni issue ndogo saana na imepangwa kitotooooo
Decayed mind!!!!
 
MZIMU WA ‘BUNGE LIVE’ WAMWANDAMA NAPE


Mzimu wa kuzuia shughuli za Bunge kuonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni uliopachikwa jina la ‘Bunge Live’, umeendelea kumwandama Waziri wa Habari, Nape Nnauye baada ya juzi kupokewa kwa kelele kiasi cha kushindwa kuhutubia wapenzi wa muziki jijini Mwanza.

Nape alitangaza uamuzi wa kusitisha kurusha moja kwa moja baadhi ya shughuli za Bunge, akisema Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linashindwa kumudu gharama, lakini wabunge, hasa kutoka vyama vya upinzani wamepinga hatua hiyo wakisema inawanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kupata habari kuhusu chombo chao cha kutunga sheria.

Lakini Serikali imeshikilia msimamo wake, ikitoa sababu tofauti na kwenda mbali zaidi kuzuia vituo binafsi vya televisheni kurusha matangazo, huku TBC1 ikirusha kipindi cha maswali na majibu pekee ikielezwa kuwa huo ni uamuzi uliopitishwa katika Bunge la 10.
Wamesalimu amri lile la TBC2 ni live jana nimeona
 
Wema walimshindwa wenye kukifahamu kiswahili kilichonyooka na wanaojua mapenzi iwe yeye.Muache afilisikiepo na kusahau hata kwenda ofisini sijui anamwona Magufuli akiwa amevaa mawani ya mbao?Hamcheleweshi atamtumbua.Mimi katika hili wala sioni pa kumlaumu sana Nape kama yeye.Yeye anatekeleza maagizo anayopewa na viongozi wenye nafasi zao kwenye nec ya chama chao na wabunge wa ccm.Kwani suala hili halikupitishwa bungeni kwa kura nyingi za wabunge wa ccm?Hamkuwaona wabunge wa upinzani wakipinga kwa vifungu lukuki na kwa nguvu zao zote lakini mwisho wake ni nini zaidi ya kura?Hivyo kelele wapigiwe wabunge wa ccm nae Nape akiwemo kwani nae aliunga mkono uamuzi huo kwa kura pia.
hata ukimwona anaonesha ni mvivu wa kufikiri na kuchanganua, hujaji lile lililo mbele yake na kutoa majibu
 
Baada ya Muda kidogo watabaini ushauri huo haukuwa mzuri hata kidogo,tuvute subira kidogo.
 
Ila kati ya vyoote hili la bunge kutooneshwa live wamechemka kupita maelezo...sio kila kitu usifanye kisa eti gharama...ebooo
Gharama gani ni uongo mbona ile miziki ya kunengua viuno inaoneshwa masaa 24 kila siku? uongo mwingine hata mjinga atakushangaaN
Napenda kufahamu CV za viongozi wangu. Mwenye ya huyu ndg naomba anisaidie tafadhali.
nape hana CV
 
Wamesalimu amri lile la TBC2 ni live jana nimeona

5efc2450b633dcb09897d559775762fb.jpg
 
Kumbuka mchezo huu hautaki hasira watanzania wamewashtukia 2020 siyo mbali
Haya matamanio yalimponza fisi mpaka akafika kwenye makazi ya wanadamu na kuuwawa kwa kuzani mkono wa mwanadamu utaanguka kumbe kujitupa kwa mikono kule ndio asili yake.
Toka mwaka 2010 ujinga wenu uliwaaminisha kuwa mtachukuwa nchi. Kilichotokea chadema mmeshindwa hata kufikisha wabunge hamsini wa majimbo kati ya majimbo 264.Pia mlishindwa hata kuwa na mtu anayefaa kuwa mgombea wa urais. Hata mwaka 2020 mtafanya haya haya kwa kuangalia nani mtu maarufu kwa wakati huo, siajabu akawa Kingwendu au Msagasumu kwa umaarufu wa kucheza singeli na mchiriku.
 
Back
Top Bottom