MZEE WA UPAKO AJIKOMBA KWA jk

chidide

Member
Nov 11, 2010
91
9
Naona sasa manabii wa uongo wanaanza kujionyesha. Wewe Luseleko unafikia wapi mpaka umfananishe Nyerere na hawa viongozi wa sasa? Au babu wa loliondo kaanza kukata mirija yako ya kiuchumi ndio unatafuta pa kutokea???


'Mzee wa Upako' ataka Kikwete asisemwe vibaya
Imeandikwa na Shadrack Sagati; Tarehe: 29th March 2011 @ 23:20 Imesomwa na watu: 54; Jumla ya maoni: 0


KIONGOZI wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, amewataka Watanzania waache tabia ya kumlaumu au kumsema vibaya Rais Jakaya Kikwete hadharani kwa kuwa vitendo hivyo vinamvunjia heshima kiongozi mkuu wa nchi.

Mchungaji Lusekeko maarufu kama Mzee wa Upako ameshauri viongozi wa dini na wanasiasa wafuate itifaki ya kuzungumza na rais kama ilivyokuwa zamani ili kudumisha utulivu wa nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Mchungaji Lusekelo alisema, kitendo cha kumlaumu Rais Kikwete hadharani ni kukosa heshima mbele ya kiongozi huyo na akatolea mfano kuwa dini zote zinakataza kumsuta kiongozi wako hadharani.

Alisema, Rais Kikwete amekuwa mtu wa kulaumiwa tu wakati kuna mengi mazuri anayofanya; lakini Watanzania hawayaoni badala yake wanasubiri siku amekufa ndiyo waanze kutoa sifa zake.

"Tuheshimiane tukiwa hai, tusisubiri kutoa sifa akiwa marehemu…hizi ni fikra za kishetani na hazipaswi kunyamaziwa," alisema Mchungaji Lusekelo.

Alitoa mfano kuwa wakati Mwalimu Julius Nyerere akiwa hai hakuwa na sifa zinazotolewa sasa na watu walisema kuwa wamechoka na unyerere. "Lakini leo hii tunamsifu kwa kila nderemo…watu wamebadilika wanasifu viongozi mpaka wanapotoka ndani ya madaraka," alisema Mchungaji Lusekelo.

"Inakuwaje Rais Kikwete tunayemfahamu aliingia madarakani akiitwa masia na chaguo la Mungu, leo hii ni adui wa kwanza…hivi sasa kukitokea tatizo kama kutonyesha mvua, basi lawama atatupiwa Rais Kikwete."

Mchungaji Lusekelo alisema, imejengeka tabia kuwa sasa ukimsema Rais Kikwete ndiyo unaonekana kuwa jasiri na mzalendo, kitendo alichosema ni utamaduni mbaya kwani hiyo inatokana na uungwana na uhuru alioutoa Rais mwenyewe.

"Uhuru usivuke mipaka hadi tunamvunjia heshima rais wetu," alisema Mzee wa Upako ambaye aliwataka Watanzania kumsaidia na kumtia moyo Rais Kikwete ili awatumikie kwa moyo. Alisema iwapo Watanzania watafanya hivyo Mungu ataendeleza nchi hii na itafika mbali.

Alitoa mfano wa mfumuko wa bei kuwa Watanzania wanamwonea Rais Kikwete kwa kumlaumu kuwa ndiye chanzo cha gharama za maisha kupanda kwani kilichosababisha mfumuko huo wa bei ni kupanda kwa mafuta kwenye soko la dunia.

"Hivi huu utamaduni wa kulaumu viongozi wanaotuongoza ambao unazidi kushamiri utaisha lini? Nchi hii ni sawa na gari, Rais Kikwete akiwa ndiye dereva; hivyo kitendo cha kutoa maneno ya kejeli kwake kinaweza kumchanganya na kujikuta akiliingiza gari katika shimo," alisema kiongozi huyo.

Alisema, wengi wanafikiri kuwa ukiwa Rais basi una moyo wa chuma, kumbe naye ni binadamu anahitaji imani ya Watanzania ili kutekeleza majukumu yake vizuri na yeye ajiridhishe katika kufanya maamuzi yake.


Source: Habari leo
 
Mtoa mada kabla hajatoa kilichoelezwa na mchungaji ameanza kuwa bias! Tukuunge mkono ama tuchangie mada?
 
Aah, kumbe ni Lusekelo wa upako? Mimi nilidhani ni rafiki yangu Adam Lusekelo.
 
Lusekelo?? I am sorry to say this but i don't know this guy if he works for God or himself.Miongoni mwa watu wasioheshimu wenzao ni yeye na chuki zake juu ya Kakobe.Iweje yeye ashauri hiki afu atende kinyume chake??
 
mzee wa upako anahitaji upako. namshauri akamuone ndugu yake Ambilikile nafikiri hata tiba anaweza kupata bure maana hawa ni ndugu,wote ni wenyeji wa Mbeya.
 
huu ni muendelezo wa Mafisadi kusafishana tu,wote ndio wale wale,ufisadi unabomoa uchumi unatueleza kisingizio cha kupanda bei ya mafuta duniani,kwani Tanzania pekee ndio inanunua mafuta kwa bei mbaya?Aje na hoja nyingine na sio utetezi huu wa kilozi...
 
amenikumbusha wimbo wa bwana misosi NITOKE VIPI?
ushauri wangu kwake vyovyote anaweza kutoka mradi isiwe uchi.
 
Huyu atakuwa anamtumikia shetani nadhani anhaitaji maombi.ujasiliamali wake kwa njia ya upako wa shetani umefunikwa na babu wa Loliondo
 
yule hata kuongea hajui...na huwa anakurupuka...kazi kujisifia tu
 
amka2.gif

MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi la Ubungo Kibangu (GRC), Antony Lusekelo, amelitaka taifa kuacha kumsema na kumkosoa vibaya hadharani bila staha Rais Jakaya Kikwete kwani kitendo hicho ni kumkosea adabu.
Mchungaji Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’ alisema Rais wa nchi ni mtu mwenye heshima ya hali ya juu, lakini wapo baadhi ya watu wanatoa lawama na shutuma mbalimbali bila kuzingatia utamaduni uliozoeleka.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mchungaji Lusekelo aliwataka watu hao kuacha dharau na badala yake wamheshimu Rais kwa wadhifa alionao.
Mchungaji Lusekelo ambaye alikuwa akizungumzia juu ya afya ya amani, umoja, upendo na utulivu alisema ziko dalili zinazoonyesha kuwa hivi sasa watu wameanza kucheza na afya ya taifa iliyodumu kwa zaidi ya miaka 50.
“Ninachokisema kinatoka ndani ya moyo wangu, sijatumwa na mtu yeyote….bali ni kutaka kuhakikisha nchi yangu inaendelea kudumu katika amani tuliyokuwa nayo siku zote,” alisema.
Alisema afya ya nchi inahitaji matunzo lakini kwa sasa matunzo hayaonekani maana kelele na kulaumiana kumeshika kasi.
Tangu Rais Kikwete aongoze kwa miaka mitano mazuri aliyoyafanya hayasemwi lakini mabaya hata kama yamejificha yanaibuliwa.
Aliwashangaa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimnanga Rais Kikwete hadharani na kusema kuwa hata maandiko matakatifu yanawakataza watu kumnyooshea kidole kiongozi wa nchi.
Lusekelo alisema hivi sasa ukionekana unamsema Rais Kikwete ndiyo jasiri na mzalendo, lakini hawajui hata kumsema Rais kwa mazuri ni uzalendo huku akionekana kurudia maneno ya biblia kuwa katika harakati zao, watashindana lakini hawatashinda. Alisema hamtetei Rais Kikwete na wala hajipendekezi kwake, kwa kuwa nafasi aliyonayo ya uchungaji ni kubwa kuliko ya Rais maana urais unakwisha lakini cheo cha uchungaji hakiishi.


h.sep3.gif
blank.gif
 
Mtoa mada kabla hajatoa kilichoelezwa na mchungaji ameanza kuwa bias! Tukuunge mkono ama tuchangie mada?
Mizizi, nakuunga mkono mkuu. Huyu ndugu ameonesha wazi ushabiki na chuki kwa Rais. Kama unaleta mada acha watu wachangie tu usitake ku influence. Huyuhuyu Lusekelo angeandika neno zuri kuhusu kiongozi wa chama fulani angetukuzwa sana humu. Asingeitwa nabii wa uongo. Ama kweli kupenda kubaya jama.
 
Waumini wengi wamekimbilia Loliondo kwa Babu, hivyo anataka huruma ya Kikwete kwani anajua sadaka sasa zitapungua. Hakuna tena watu wa kuwadanganya na maombezi yake.
 
kuna uwezekano mkubwa ni njaa inamsumbua. Kwanini hasipime yale watu wanayo sema kwanza? huwezi zuia watu kulalamika hata kama ni vitu vidogo, kama matatizo yapo watu wanahaki ya kulalamika, tatizo kubwa Tanzania yetu ina matatizo mengi sana NA makubwa sana lakini serikalini watu wamejisahau, hajui wanalipwa kwa kodi ya watu hao hao wanaowaibia na kuwa nyanyasa kila siku.
 
Mchungaji huyu namheshimu sana lakini nadhani yeye haoni hali halisi jinsi ilivyo mtaani. Amesahau jinsi watu wanavyofanya madudu kupitia cheo cha urais, namkumbusha mzee wa upako kuwa aache kuingia kwenye siasa inaweza kumshusha hadhi haraka sana na si yeye tu bali viongozi wote wa dini.
 
Back
Top Bottom