Mzee Pinda, Mh. Zitto na Ridhiwan Kikwete

wote hawa ni mamilionea tena kuna ujanja wanatumia ,ambapo kwenye mali zao wana-sajili kwa majina ya ndugu zao na pesa wanatunza katika account za wafanyabiashara wakubwa nchini, ila ipo siku yote yatajulikana .

Millionea ni wengi tu Tanzania, watu wengi mishahara yao inawaruhusu, labda useme mabilionea
 
Hapa jf tuna tatizo la watu waitwao "hate preachers", watu hawa wana chuki na yoyote bila sababu yoyote!, hivi vijisababu vya kutafuta mali zao ni scapegoat ya kujaribu ku justify chuki zao!.

Kwa watu wanaowachukia, hawana jema lolote, kwao kila jambo ni baya tuu!.

Mtu kakueleza aliletewa Hammer , Vogue na Vx katumia akauza, sasa what is a big deal!.

Mtu anakiambia gari yake na kishamba chake bado huamini, unalazimisha lazima kaficha utajiri!.

Please stop this hate!. Acheni chuki, ikizidi sana inageuka ugonjwa unaotokana na "deep rooted neurosis"!.

Pasco.

Pepo wa kijicho, wivu na chuki ameiwavaa watanzania.
 
QUOTE=Tyad of fake Politcs;4575173]Wadau mtoa mada,amejenga hoja naomba tumjibu kwa hoja........................hapo katkat kuna kiin macho na kgugumiz cha mali..tuwe wa kweli..viongoz uwa hawako tayar kutaja mali zao,ni kama ambavyo ww mdau uwez kututajia mshahara wako wa kweli.

ZZK,RJK,MPP Waje na htaarfa za ukweli hapa[/QUOTE]

Sijaona hoja ya mtoa mada zaidi ya majungu na wivu wa kike,hivi hzo hammer mnaona gari ghali sana ?mimi nafanya kazi simple sana hapa ughaibuni mwaka 2010 nilinunua hammer H3 kwa kiasi cha 35,000 Dirham kama Ths 14m na laki 7 za bongo,model 2000 kwa hyo swala la kumiliki hammer sioni kama ndio mtu kawa tajiri,mto uzi kama wewe sio mnafiki toa ushahidi ambao unapingana na Mh zitto ili tujue kweli wewe sio mnafiki,vinginevyo wewe ni mtu mwenye wivu,wabongo kwa wivu wa kike tuko fiti,

s
 
Wewe hapa unalenga kumchafua zitto, kwa taarifa yako hata uvue nguo, Zitto ni Rais 2015 hata kama sio CDM, itakuwa hata ugombea binafsi. nyie endeleeni kuimba kikasuku tu.
Ninadhani careboy una mapenzi na Uraisi wa Zitto, Jambo ambalo siyo baya kwa vile kila mtu huwa ana objectives zake katika maisha, lakini sidhani kama wewe unafaa kuwa mtafsiri wa objective za Zitto Zuebri Kabwe.Hata hivyo wa kusema nani awe Rais si ni waTZ ama umeona utusemee? Great thinkers huwa hawaleti upuuzi kwenye hoja muhimu, changia objectively hata kama mapenzi yako ni Zito kuwa Rais 2015. Mimi sioni kama kura yako ndani ya chama ama nje ya chama itakufikisha kwenye hiyo objective yako. Jambo la msingi ni kwamba mwandishi ameona kuna angalizo ambalo wewe ni juu yako kuliondoa hilo angalizo kwa hoja za ushahidi kwamba hilo sio angalizo la kweli ama ni kweli. Kwangu mimi na nadhani kwa yeyote mwenye kuelewa mambo, Yote mawili kweli ama si kweli halizuii Zitto kugombea na hata kuwa Rais kwa kuwa ni haki yake kikatiba kama ulivyo na haki wewe kuwa rais bdalla ya kuset objective kwa niaba ya mtu mwingine, siyo lazima uwe mapiga debe wa Zitto. Mara nyingi zitto amesikika akiwalaumu sana watu wanaopenda kuwa wasemaji wake kwa vile yeye Zitto anao uwezo wa kujieleza kama alivyojieleza alipoulizwa masawali hayo kuhusu mali zake, ameweza kujibu vizuri ingawa hayakumridhisha mwandishi. Ushauri wangu:Wewe tunza kura yako mpaka Zitto atakapo tangaza kwamba yeye ni mgombea Urais halafu umpe na ikibidi chukua na mkeo na watoto wako tayari atapata kura tatu labda na ya kwangu zitakuwa nne. lakini kwa sasa bado ni mapema mnno Mr. Careboy.
 
Hawa wengine hawanihusu sana lakini kuhusu zitto, ni aibu kubwa kwa 'the great thinker' kumiliki V8, Freelander, Hammer nk alafu ukailaza kwenye nyumba ya kupanga au shamba la urith la bibi!!! Hii itakuwa ni uongo na uenda muda ukatueleza ukweli juu ya haya.
Hii inaanza kunipa wasiwasi maana huyu bwana nilimuamini na kumhusudu sana katika nyanja ya 'ukombozi'

Ebwana ata mimi nimejiuliza same question? ukiangalia hapo chini nimekupa kitufe cha "like"
 
Hii thread ingekuwa na maana iwapo mwandishi angekuja na vidhibiti vya utajiri wa anaowatuhumu. Jinsi alivyoandika inaonekana anaendeshwa zaidi na hisia. Tukiamua kila mtu kuandika hisia zake hapa JF nadhani mtandao utajaa within one hour...
 
Mada ililenga kumjadili Zitto hao wengine wamechomekewa tu.Hongera kwa kuwaza na kufikiria Mali za watu wakati shughuli zako zinakushinda
 
zitto aliwahi kusema humu kuwa hajawahi kumiliki vogue...mkuu umesahau na HAMMER(nasikia alipewa na rostam)
 
Zitto nilikuwa nimemwamini sana ila kwa kweli nimeanza kutokuwa na imani nae kwani hizi safari zake na magamba zimeanza kunitia wasiwasi kwani hata siku moja chui na paka huwezi kusema ni walewale au umweke chui kwenye kundi la mbuzi useme wote ni wanyama hivyo ipo siku ukweli utajidhiirisha.
 
Hii thread ingekuwa na maana iwapo mwandishi angekuja na vidhibiti vya utajiri wa anaowatuhumu. Jinsi alivyoandika inaonekana anaendeshwa zaidi na hisia. Tukiamua kila mtu kuandika hisia zake hapa JF nadhani mtandao utajaa within one hour...

Ni kweli kuthibitisha jambo kunahitaji vidhibiti. Ndo maana hata DHAHABU, TANZANITE, TWIGA na vingine navyo lazima vikathibitishwe maabara za nje ya nchi, tuletewe makalatasi ya report ndo tujue ukweli! Na hata mtu akiuawa mbele ya macho yako kwa risasi bado unahitaji TUME kuchunguza amekufa kweli? amefaje? nini kimemuua? na labda amelala tu ataamka!
 
Hapa jf tuna tatizo la watu waitwao "hate preachers", watu hawa wana chuki na yoyote bila sababu yoyote!, hivi vijisababu vya kutafuta mali zao ni scapegoat ya kujaribu ku justify chuki zao!.

Kwa watu wanaowachukia, hawana jema lolote, kwao kila jambo ni baya tuu!.

Mtu kakueleza aliletewa Hammer , Vogue na Vx katumia akauza, sasa what is a big deal!.

Mtu anakiambia gari yake na kishamba chake bado huamini, unalazimisha lazima kaficha utajiri!.

Please stop this hate!. Acheni chuki, ikizidi sana inageuka ugonjwa unaotokana na "deep rooted neurosis"!.

Pasco.
Hapa ndugu yangu Pasco hakuna cha hate syndrome tunatafuta viongozi waadilifu wa kuongoza TZ yetu tuipendayo wasio mafisadi, mtu kabla ya kuwa hata waziri anaanza na umiliki wa Rover Vogue v8, Hummer, mra hoo Toyata Land CRUISER V8 bila aibu ananunua na kuuza bado tuu wewe unamwamini awe kiongozi bora???? Kwanza source ya mapato ya kununua hizo mali, je akipata mwanya unategemea nini, CDM anzeni kujichunguza wwenyewe mapema isiwe mnapiga kelele kwa nje kumbe ndani kumeoza!!!!!

Wewe hapa unalenga kumchafua zitto, kwa taarifa yako hata uvue nguo, Zitto ni Rais 2015 hata kama sio CDM, itakuwa hata ugombea binafsi. nyie endeleeni kuimba kikasuku tu.

Mkuu, anayemchafua ni mleta mada au ni hivyo vyanzo vya taarifa ambavyo amevinukuu? Na hilo la kuvua nguo tena limeingiaje hapo mkuu? Jaribu tu kuchangia kwa kutuelimisha ili tujue lengo la mleta mada ni kumchafua ZZK kuliko hivyo ulivyofanya. Ni maoni yangu tu lakini.
 
Kuwa kiongozi haimanishi uwe maskini,kupata kwa mtu ni kujituma na majaaliwa ya mwenyezi mungu.We kama huna ongeza juhudi usiwe na viwu mwishowe utakuwa mchawi.
 
Kuwa kiongozi haimanishi uwe maskini

Umenena vema Mkuu.
Ni haki ya kila mtoka jasho kufaidi matunda ya kazi yake na kuyaonea ufahari. Tatizo ni kwa nini wanaukataa Utajiri na wengine waliowahi kujigamba kwa vinywa au kuandika mali zao, kwa nini sasa wanazikana mali zao?
 
Wewe hapa unalenga kumchafua zitto, kwa taarifa yako hata uvue nguo, Zitto ni Rais 2015 hata kama sio CDM, itakuwa hata ugombea binafsi. nyie endeleeni kuimba kikasuku tu.

Zitto siyo mungu hata asiwe na mapungufu. Kuna kila sababu ya kumchunguza mtu kabla ya kumpa ridhaa kubwa na yenye heshima kama URAIS wanchi.
 
Back
Top Bottom