Mzee Pinda, Mh. Zitto na Ridhiwan Kikwete

Kama wao walikuwa wanapiga Blabla jitofautishe kwa kuweka Plate namba za gari wanzomiliki,Block / plot namba ya majumba wanayomiliki sio kurudia nyimbo za Kikasuku, mnaogopa nini kiweka ushahidi wa vitu hivyo! Nyie kipindi kile mnatumika kama wawezeshaji wa Mtandao si mlimzushia sana Mzee Sumaye eti anamiliki Trillion 10.

kwani hizo ndio hati za umiliki?hata hati za umiliki zenyewe si uthibitisho.Uthibitisho ni pale wanapodhulumiwa na wahindi ,waarabu na wengine wanaoshikilia kwa majina yao.Wengi tuu wamelizwa baada ya kutoka katik channel.

Wengi wamelizwa na hawa jamaa haswa katika biashara za nje, at a time panakuwa na hela nyingi nje zaidi ya ndani ndipo wanahama nchi.Mbaya huwa hawana pa kudai zaidi ya vitisho vya nyuma ya mlango.
 
Masuala ya kusema fulani ni Rais mwaka 2015 ni uendawazimu unaoweza kuzungumzwa na wendawazimu pekee. Umeingia kwenye akili na utashi wa watanzania wakakuambia Zitto ndiye Rais 2015? Acha uzumbukuku jibu hoja iliyoko mbele yetu kwa hoja na si utumbo kama huo. Zitto huyo unayemsema anafaa kuwa Rais, kwa maneno yake anasema alinunua gari la kifahari aina ya Hummer kisha akauza eti kwa kushindwa gharama zake! Ina maana alikurupuka kulinunua kabla hajafanya analysis ili kujua kama ana uwezo wa kulimudu au la? Kama anashindwa jambo dogo kama hilo la kutumia umakini na akili ya kawaida tu, leo unamuota eti ndiye Rais 2015 si ataitumbukiza nchi kwenye tope kutokana na kukurupuka? Iliwahi kudaiwa na gazeti moja kwamba anamwasiliano ya karibu sana na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa. Je, ni kwa ajli ya urafiki wa kawaida au kufanya ukachero ndani ya CDM kwa maslahi ya CCM na Serikali yake? Tuache ushabiki. Hata kama magari hayo ya kifahari kayauza lakini si alikuwa nayo na aliyanunua kwa bei mbaya? Hapo hoja ya kwamba ana utajiri mkubwa kiasi cha kununua magari ya kifahari kama hummer na mengine inakufa eti kwa sababu kayauza? Mbona hakusema chanzo cha pesa alichotumia kununulia Hummer, V8 na Range badala yake amesema chanzo cha pesa alichotumia kununua gari analodai kutumia kwa sasa? Huo si ubabaishaji katika kujibu hoja?
 
Great minds discuss ideas; average minds discuss events; small minds discuss people
 
nilishawa kuonyeshwa lile jengo la ghorofa moja la kibiashara pale pale kisasa Dodoma,nikauliza la nani ? nikaambiwa la bwana zitto..>>kama kweli Hongera bwana Zitto ..ile hela ilowekwa pale si mchezo,
 
Acha uzembe wewe, nania kakuambia, mtu anayomba ajira hawi discussed na mwajiri wake?

Kujadiliwa unapoomba ajira na kuwa discussed ni idea hiyo, usiwe punguani.

Sasa kwenye hii mada ni nani anaeomba ajira?
 
Kujadiliwa unapoomba ajira na kuwa discussed ni idea hiyo, usiwe punguani.

Sasa kwenye hii mada ni nani anaeomba ajira?

Anayetaka Urais ndiye anomba ajira.Au ata-volunteer.?...kama kuomba ajira ni idea inayohitaji kuwa discussed,na urais ni Ajira .Then upunguani wangu upo wapi hata kwa viwango vyako.Iam discusiing ideas...fool.Zitto ndie apaswaye kujua ajira anayoomba requirements zake zinahitaji personal life iwe discussed.Kama hayupo comfortable kwa hilo ni bora aache na si ku redefine job descriptions.Akajiajiri mwenyewe basi.Au kwa vile anaona ni public properties basi anadhani wengine hawana haki ya kuuliza?
 
eti anaendesha toyota camri :biggrin1: you guys have made my day
Kuna jamaa kaniambia huyu dogo alipokuja New York karibuni alikodisha private jet kumpeleka Washington D,C kwa washkaji wake wakati kuna shuttle za every hour kati ya NY na DC. Halafu eti alimwachia tip ya dola elfu moja mama mmoja aliyekuwa anamhudumia. I do not know how true this is, but it is out there.
 
wakati fulani mbowe alishutumiwa kuwa hakuorodhesha mali zake kwenye kamati ya maadili ya viongozi wa umma.Nakumbuka alijibu kuwa hawezi kukurupuka kuorodhesha mali zake kwa haraka kwani ana mali nyingi na ziko sehemu mbalimbali. Alitaka kupewa muda zaidi ili kuweka taarifa zake sahihi. nilimpenda sana kwa uwazi wake aliouonyesha wa kukiri hadharani kuwa na mali,tena nyingi!
 
Ndo jinsi ilivyo hivyo..............kila anayefikiliwa kufanya vizuri na kupewa nafasi anafanya mambo ya kipuuzi,akipanda jukwaani anajifanya ni kiongozi anayefuata misingi ya mwal.[huyo ni Pinda na Zitto].Ridhiwani yeye yupo nchi ya kifalme anatumia mali ya nchi kama ya baba yake.Wasali sana maana hawajui siku wala saa watanzania watakapobadili mawazo yao.
 
Riz1 ana mali kibao...ananuka ufisadi wa silimia 100. Vipi kuhusu kampuni iitwayo RIJK ZWAAN Q-SEM ya kule Tengeru, Arusha? Narudia kusema ni jirani yangu kule eneo la kisongo nilikojenga na ana viwanja na mashaba kama settler...Vipi pale ktk mashamba ya Burka Estate, waqlala hoi tulikosa hata hizo medium density na yeye akapata low density tisa (zenye uwezo wa kujengwa shule, hospitali na makorokoro mengine kibao............mbona mengi tu tunayajua?

Vipi kuhusu mlolongo wa mahoteli kupitia kampuni ya Hyatt toka uarabuni? Yeye na baba yake Mhe. JK ndio waliochukua hoteli za kempiski (Bilila Kempiski-kule serengeti).......Vipi kuhusu hotel ya Mt Meru Arusha? kupitia mwavuli wa Hyatt hiyo hiyo baada ya kampeni ya muda mrefu ya kumpokonya Mengi Reginald toka mikononi mwa Bill Clinton Foundation na South African Enterprises Development Fund (SAEDEF) ya Mzee Nelson Mandela...Aache ubishi ataumbuka!!

Asome alama za nyakati kwa mtoto wa Omar Bongo na mali zake kule Ufaransa.
 
Hivi kama mtu atanunua majumba ya kifahari leo halafu baadaye akahojiwa juu ya chanzo cha mapesa yaliyotumika kununua majumba hayo, kisha yeye akajibu kwamba; ni kweli majumba hayo alikuwa nayo kisha akaamua kuyauza kwa sababu zozote zile, itaondoa hoja ya msingi? Ndivyo ilivyo kwa Nyepesi. Kakili alikuwa anamiliki Hummer, Range, V8. Yote ya bei mbaya kisha kayauza eti kisa kashindwa kumudu gharama za matumizi yake. Hiyo inaondoa hoja? Nyie mnaosema ndiye Rais 2015, nyie tu ndio mtachagua kwa niaba ya watanzania wote na kumpa huo urais? Kama alinunua magari ya kifahari kwa mapesa mengi bila kujua kama atamudu gharama za matumizi yake huko si kukurupuka? Kama ameshindwa hilo, unampima kwa kigezo gani kiasi cha kusema ndiye rais wako 2015? Hivi mtu anaweza akamiliki magari hayo ilihali hana nyumba ya maana? Hapo si changa la macho? Mbona kataja chanzo cha pesa cha gari analodai kuwa anamiliki kwa sasa na hajataja vyanzo vya fedha vilivyomwezesha kununua Hummer, Range na V8?
 
Nikienda mbali zaidi..nikiangalia msururu wa magari aliyonunua zitto na kuyauza kwa sababu nyepesi kama naona Zitto hafai kwa mambo mengi.Hajui uchumi na hajifunzi.Kama hajui gari ni liability kama litatumika vibaya, ila kuna mengine ni liability zaidi kwa asili yake Zitto hakuona hayo+ La kwanza hakujifunza, la pili hivyo hivyo la tatu + hivyo hivyo.

Pamoja na kwamba Zitto ana matatizo sana ktk "Esteem",anatafuta furaha katika material things baadaye life itakuwa too boring kwake.(Na anaweza kuja kuwa Religious fanatic, akikimbizwa na fikra kuwa anachukiwa), bado Zitto Elimu yake inaanza onekana kuwa haina faida kwa nchi.Ni mmoja wa watu ambao wanfaa CCM kuwa waziri aisyejua sheria kupewa wizara hiyo, na hivyo kufanya mgogoro mkubwa na makatibu wa Wizara.
 
Kuna jamaa kaniambia huyu dogo alipokuja New York karibuni alikodisha private jet kumpeleka Washington D,C kwa washkaji wake wakati kuna shuttle za every hour kati ya NY na DC. Halafu eti alimwachia tip ya dola elfu moja mama mmoja aliyekuwa anamhudumia. I do not know how true this is, but it is out there.
Duh!hii kali mkuu wangu!duuh!hopefully ni majungu tu.
 
Bongo kila mtu ni jambazi asikuambie mtu, hakuna hata mbongo mmoja asiependa pesa hata mimi ni zimind mbaya nikipata upenyo watanikoma
 
Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom