Mzee Pinda, Mh. Zitto na Ridhiwan Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Pinda, Mh. Zitto na Ridhiwan Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Omutwale, Sep 6, 2012.

 1. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nazidi kupata hisia kuwa huu uzio uliopo kati ya Walalahoi na Walalahai sio tu unajenga mahusiano ya kinyonyaji bali pia unapumbaza akili za Walalahai na kudhani Walalahoi wana akili za mahayawani au maiti kabisa. Jana Gazeti la Fahari lilianguka mikononi mwangu. Katika kupitia kurasa, nikakutana na habari ya juu ya Intelijensia ya CDM kuchunguza utajiri wa Zitto. Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni mfanano uliomo katika majibu ya Zitto, Mizengo Pinda na Ridhiwan Kikwete pale wanapochokonolewa kuzungumzia mali zao kwa umma.

  Kipindi Fulani kulitokea uvumi kuwa Mtoto wa Mkulima amewekeza kwenye Sekta ya Usafiri kupitia Kampuni ya SUMMRY EXPRESS. Baada ya uvumi huu kushika kasi sana, Mtoto wa Mkulima akajitokeza na ngonjela kuwa mali alizonazo ni pamoja na pesa shilingi milioni 25 kwenye akaunti yake, nyumba tatu za kawaida moja ikiwa jijini Dar es Salaam, Mpanda na Dodoma na gari moja alilolinunua kwa mkopo.

  kwa maneno yake anasema "Hizo ndizo mali zangu nilizo nazo ndugu.
  Nina nyumba Dodoma kutokana na utaratibu wa mikopo ya nyumba za serikali; nina nyumba Mpanda ambayo imepatikana kwa mpango wa kawaida tu, imetokana na visenti kidogo nikanunua pale ambapo bahati nzuri gharama za ujenzi hazikuwa kubwa sana, nikakikarabati kipo pale kipo Makanyagio pale."

  "Haya! Ukitoka pale unataka niseme nini tena. Dar es Salaam sina nyumba ya kusema ya maana sana ukienda shambani Pugu kule kipo kinyumba kidogo hivyo inahitajika kazi ya ziada kuweza kufanya paonekane pa maana.

  "Kijijini kwa baba yangu pale Kibaoni sina nyumba; pale mlipoona nimekaa na bibi tunapiga porojo, kile kijumba mimi na wadogo zangu tulimsaidia babu kwa ajili ya kumjengea babu yetu na pale ndipo nilipokuwa nafikia siku zote wakati wa likizo."
  [​IMG]Chanzo: Pinda atangaza mali zake

  Baada CD ya Mtoto wa Mkulima kumalizika dukani, ukaletwa mzigo wa "The Dollar Prince" Ridhwan wa Kikwete. Kijana kwa kushindwa kufanyia kazi ushauri aliopewa, wa kukaa kimya, akaja front na kukutana na Waandishi wa Habari ili kukanusha utajiri wa ghafla alionao na pia kutangaza kusudio la kuwashtaki Dr. Slaa na Mch. Mtikila jambo ambalo hadi kesho halitofanyika! Tujikumbushe utetezi wa Ridhwan:

  "Katika yote waliyosema sina hata kimoja, sina kampuni za ujenzi, malori wala maghorofa. Hizi ni tuhuma za juu juu tu maana kama wangekuwa wakweli wangesema hayo maghorofa yako wapi. Nina akaunti CRDB, NBC na STANBIC na anayetaka kujua nina kiasi gani aende kule, lakini mimi sijui ziko shilingi ngapi," alisema na kusababisha kicheko. Alipoulizwa kuhusu kumiliki gari la kifahari aina ya Hummer, Ridhiwan alisema licha ya kwamba, hajawahi kumiliki gari hilo, hajawahi hata kupewa lifti ndani ya gari la aina hiyo. Alisema anamiliki gari moja aina ya CAMRI na shamba la ekari moja na nusu Bagamoyo mkoani Pwani" "Maisha ya mjini hapa si mnayajua wenzangu, si kila unachomwona nacho mtu udhani anakilimiki"
  [​IMG]Chanzo: Home

  Wakati CD ya Ridhwan ikiwa katika studio tofauti tofauti kuongezewa vikolezo na kuendeleza re-mix mpya kwenye album ya utajiri endelevu wa ghafla, soko limeletewa wimbo unaotokana na akapela iliyokuwa imesikika kitambo lakini kwa muda mrefu ilitolewa vipande vipande. Ni santuri ya majibu ya utajiri wa kijana jasiri, mwanasiasa mahiri, mjanja sana na mweledi--Zitto Kabwe. Majibu yake naomba ujisomee mwenyewe kwa kirefu hapo chini:
  "Sijawahi kuwa na nyumba wala kiwanja hapa Dar wala Dodoma isipokuwa nyumbani Kigoma, huko nina nyumba vya vyumba viwili tu ambayo niliijenga wakati wa uchaguzi baada ya wazee kunishauri kuwa siyo vizuri kuendelea kutumia nyumba ya baba yangu.

  Ninapaswa kuwa na kwangu. Labda kuna shamba la hekari tatu na nusu nililopewa na bibi yangu liko Kigamboni eneo la Mbutu, sijaendeleza hadi sasa, lipo tu. Lakini pia ieleweke kuwa nina uwezo wa kujenga kama Mbunge, wabunge wenzangu wengi tu wanajenga, mimi ninashindwa kwa sababu ya majukumu yangu ya kifamilia. Nimeshasikia sana watu wanazungumza ninajenga ghorofa kubwa Dodoma na baadhi ya watu wanaiita sehemu hiyo kuwa ni kwa Zitto sina hata kiwanja Dodoma, uzushi mtupu wa maadui zangu kisiasa".

  Akizungumzia Utitiri wa magari ya kifahari anayodaiwa kuwa nayo anasema "Watu wanaishi maisha ya kufikirika sana, hayo magari wanayodai ninayo sina, iko hivi; mimi nina gari moja dogo aina ya Toyota Vista na nina Land Rover, Free Lander ambalo nimelichukua kwa mkopo, bei yake ni Dola 30,000, sijamaliza kulipa. Hayo mengine yanayosemwa ninayo ni ujinga tu wa watu.

  Baada ya kuwa mbunge, nakumbuka April 2007 niliingiza nchini gari aina ya Hammer na nadhani nilikuwa mtu wa pili kuingiza gari hilo hapa nchini. Kaka yangu Salum anayefanya biashara ya magari ndiyo aliyeniletea na hili sikuliendesha zaidi ya wiki mbili, likanishinda. Lilikuwa la kifahari mno, nikamwambia alichukue aliuze na hela yangu anirudishie.
  Nakumbuka nilikwenda nalo Dodoma nikiwa naendesha na nilikwenda na Dk. Slaa na siku moja mwenyekiti wangu Mbowe baada tu ya kuletewa tukiwa Protea Hotel iliyo karibu na Kanisa la mtakatifu Petro, alijaribu kuliendesha akaniambia ni gari zuri sana. Hili nililikataa. Mwaka 2008 nilinunua Toyota Land cruiser V8. Hili nililitumia hadi kwenye kampeni mwaka 2010 na baada ya hapo nililiuza.

  Salum alipoona sina gari kwa sababu nadhani ya kujua mimi ni mbunge akaniletea tena Range Rover Vogue Sport nililitumia kidogo likanishinda kwa sababu ni la kifahari sana, sikuweza kuligharamia. Nina akaunti mbili tu moja benki ya NMB na nyingine benki ya CRDB na zote hazina fedha zaidi ya shs Mil. 15 kila moja."- Zitto Kabwe
  [​IMG]
  Chanzo: HABARI MOTOMOTO: ZITTO KABWE 'AANIKA' UTAJIRI WAKE


  HITIMISHO
  Kila Mtanzania anayo haki ya kumiliki na kutumia rasilimali anazopata kwa jasho lake halali. Na hii inampa pia haki ya kujionea fahari hata kuwa huru kutangaza chochote anachomiliki kihalali. Hizi hadhithi za Shamba la kuridhi toka kwa bibi, magari ya kuazima toka kwa washkaji, au mali ya mikopo toka serikalini hazina mashiko.

  Mathalani, mtu wa sifa za weledi kama Zitto Kabwe kama anaweza kununua magari katika nyakati tofauti bila kuwa amefanya upembuzi yakinifu juu ya gari na Uwezo wake kulimudu katika mahitaji (Fuel, maintenance, repairs, etc) basi hafai na wala hastahili kuongoza au kuwa katika chombo chochote kile kinachofanya kazi ya Mipango na Matumizi. Mtu kama anashindwa kupanga mambo yake mwenyewe kwa kupima mapema urefu wa mfuko wake anawezaje kusimamia Wizara ya Fedha au Kamati zinazohitaji mipango madhubuti ya Kimkakati? Sijawahi kuamini kuwa Zitto anaongoza Taasisi yoyote kwa Trial & Error! Kitu ambacho anataka kuwaaminisha watu pale anajitetea juu ya umiliki wa magari ya kifahari kwa kisingizio cha kushindwa kuyamudu na kuyauza katika nyakati tofauti. Zitto anajisahau kuwa mwaka 2008 alipata kuandika hapa kwa kujitapa kuwa amefanya kazi Friedrich ebert Stiftung Foundation, amefanya Consultancies Wizara ya Fedha na ZNZ na ni MB hivyo asingiweza kushindwa kumiliki hammer kwa hela yake mwaka 2008! Sasa iweje miaka ya hivi karibuni amegeuka kauli yake?


  • Hivi nani asiye na akili ya maiti anaweza kuamini kuwa Ridhwan anatembelea (achilia mbali kumiliki) gari aina ya Toyota CAMRI?

  • Ni nani katika watu wenye macho aliyepata kwenda Msoga, Kiwangwa, Fukayosi, Lusako, Miono, au Lugoba anaweza kuamini Ridhwan kumiliki shamba ekari tu la urithi wa bibi na si maekari ya urithi wa Watazania?
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Yeah_hata mimi siwapendi hawa,...ila siwezi kuwaita mahayawani.
   
 3. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Role model wake ni Zenawi Meles........!
   
 4. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zoezi la kuorodhesha mali unazomiliki kimaandishi kabla ya Utumishi wa umma naona ama limeshindwa kutekelezeka kwa ufanisi au kuna usanii mwingi mnoo!Ndio maana mpaka leo kuna baadhi ya watumishi srikalini mishahara yao na marupurupu yamekuwa siri.Kama tawala za kiafrika zinaficha fedha uswiss au kufungua viitega uchumi nje ya nchi.Utapata wapi ushahidi wa kuwaban?
   
 5. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  Hawa wengine hawanihusu sana lakini kuhusu zitto, ni aibu kubwa kwa 'the great thinker' kumiliki V8, Freelander, Hammer nk alafu ukailaza kwenye nyumba ya kupanga au shamba la urith la bibi!!! Hii itakuwa ni uongo na uenda muda ukatueleza ukweli juu ya haya.
  Hii inaanza kunipa wasiwasi maana huyu bwana nilimuamini na kumhusudu sana katika nyanja ya 'ukombozi'
   
 6. C

  Careboy wamuntere Senior Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe hapa unalenga kumchafua zitto, kwa taarifa yako hata uvue nguo, Zitto ni Rais 2015 hata kama sio CDM, itakuwa hata ugombea binafsi. nyie endeleeni kuimba kikasuku tu.
   
 7. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  hiyo ndiyo tz na kama unabisha ko njiani kwenda mabwepande
   
 8. T

  Tyad of fake Politcs Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau mtoa mada,amejenga hoja naomba tumjibu kwa hoja........................hapo katkat kuna kiin macho na kgugumiz cha mali..tuwe wa kweli..viongoz uwa hawako tayar kutaja mali zao,ni kama ambavyo ww mdau uwez kututajia mshahara wako wa kweli.

  ZZK,RJK,MPP Waje na htaarfa za ukweli hapa
   
 9. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  small minds speaks about people..............
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Labda Rais wa TFF au Miss Tanzania.
   
 11. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  rekebisha 'kangereza' kao hapo then we shall move to issues!
   
 12. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ha ha utajiri kwetu Tanzania zambi. Haitoshi kuwahoji wao tu kuna haja ya kuhoji mali wanazomiliki wake na hawara zao.
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Anza kurekebisha wewe kwanza ili tuendelee na mjadala.
   
 14. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zoezi la kuorodhesha mali unazomiliki kimaandishi kabla ya Utumishi wa umma naona ama limeshindwa kutekelezeka kwa ufanisi au kuna usanii mwingi mnoo!Ndio maana mpaka leo kuna baadhi ya watumishi srikalini mishahara yao na marupurupu yamekuwa siri.Kama tawala za kiafrika zinaficha fedha uswiss au kufungua viitega uchumi nje ya nchi.Utapata wapi ushahidi wa kuwaban?
   
 15. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Haya yote nimeshakuwaga na hofu nayo kitambo sana,ila hakika lenye mwanzo hakika hata mwisho upo!
   
 16. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  wote hawa ni mamilionea tena kuna ujanja wanatumia ,ambapo kwenye mali zao wana-sajili kwa majina ya ndugu zao na pesa wanatunza katika account za wafanyabiashara wakubwa nchini, ila ipo siku yote yatajulikana .
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Hapa jf tuna tatizo la watu waitwao "hate preachers", watu hawa wana chuki na yoyote bila sababu yoyote!, hivi vijisababu vya kutafuta mali zao ni scapegoat ya kujaribu ku justify chuki zao!.

  Kwa watu wanaowachukia, hawana jema lolote, kwao kila jambo ni baya tuu!.

  Mtu kakueleza aliletewa Hammer , Vogue na Vx katumia akauza, sasa what is a big deal!.

  Mtu anakiambia gari yake na kishamba chake bado huamini, unalazimisha lazima kaficha utajiri!.

  Please stop this hate!. Acheni chuki, ikizidi sana inageuka ugonjwa unaotokana na "deep rooted neurosis"!.

  Pasco.
   
 18. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  zitto si yuko humu kwenye jamii forum atupe ukweli kwa haya maana kukanusha hakutoshi aseme ukweli
   
 19. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mkuu mie nadhani hatuwatendei haki viongozi wetu kwa kuwahoji juu ya kiasi cha mali walichonacho kama hatujui kiasi wanachopata (mishahara yao). Tuondoe siri hii katika mishahara ya watumishi wa umma.. iwe wazi ....tuijue.... ili tuiilinganishe na mali wanazomiliki.....
   
 20. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  tatizo Zitto haeleweki, jana alikataa kuwa hajawahi kumiliki Hammer
   
Loading...