Mzee Mwanakijiji, Tafadhali...


Whether EL is a thief or not we need to see CCM out first.other issues shall be dealt with later.naomba tuvumiliane hivyo.miaka yake ya utawala mbovu yatosha.CCM haina hati miliki ya siasa na madaraka Tanzania.let them go.Tanzanians unite you have nothing to lose except your chains-poverty,ignorance and the like.
 
Lord denning you have nailed it! Ni ujinga eti adui yetu ni CCM! Yaani kuna watu wajinga. Badala ya kuelezea sera wangelea chama!

Ujinga au werevu ni mtazamo tu...

Lakini Kumdhania mwenzako kuwa mjinga, eti kwakuwa anamtazamo tofauti naule ulionao wewe nadhani ndiyo "Ujinga" wenyewe hasa.

nikiwa na maana ya "ignorance". Wala sio kusudi langu kukukosea heshima. Tafadhali


Nasema ignorance, Kwa sababu mtu mwerevu au mwenye elimu kidogo atakuwa amegundua tayari (angalau kwa elimu yake na "exposure") kuwa dunia ni kubwa kwakweli, na katika historia yake, maendeleo hasaa huzaliwa na kushamiri panapo mawazo tofauti. .

Niombe tena, na tena kwakusihi sana. Tuelekeze nguvu katika kuwaweka watu wetu pamoja, tulivuke hili.. Ushindi ni halisi zaidi tunapo nia mamoja. Haitusaiidii kupigana wenyewe kwawenyewe eti juu ya nani anaruhusiwa kutuunga mkono na nani haruhusiwi kutuunga mkono!

Halafu tunasahau yote juu ya kwanini tuliungana mikono in the first place.. Tusahau nini kilituleta pamoja, tuko kufanya nini?

Comrade Vita ni Vita na mapambano ni lazima yaendelee.. Tukisamama kuzodoana , Adui yetu anayachochea haya zaidi..

Ninafahamu pia kwamba wengi wanajifanya kuchukua Mrengo kama huo wa mawazo, kuonekana kana kwamba wanaipenda sana chadema nakujitokeza kutetea maslahi ya wana chadema lakini actually ni makada wa CCM wenye nia ya kulipa audience jambo hili kwania ile ile ovu yakufifisha nguvu ya upinzani wa kweli katika nchi yetu . .

So unfortunately, wengi wachanga wanaangukia katika mtego wao. Lakini most unfortunately hata wale waerevu na wenye uwezo mkubwa wakufikiri na kuongoza pia wanajikwaa hapa.

Ndugu zangu Mwanakijiji na wengine, Let us not wash our dirty linen in a foreign land.. Ni aibu kwetu sote wala sio sifa kayeyote kua eti atasifiwa "anajua kujenga hojaaa" au eti "flani alishasemagaaa" No Never..

Sifa hizo ni nishani ya usaliti wa harakati yetu wenyewe.. Itegemee tu kutoka kwa maadui wetu kwa kazi nzuri tunayo ifanya kwaniaba yao(kuivuruga chadema).. Kwakujua ama pasinakufahamu..

Sifa Za Kijinga!

Mungu atusaidie.,

Comrades,
 
Last edited by a moderator:

Raisi (EL) atafanya nini pakiwa na idadi kubwa ya wabunge wa UKAWA?
Assumptions ni kitu kibaya sana. Msi-assume kwamba UKAWA hawajayafikiri haya mnayowatahadharisha nayo.
 
Hivi msimamo wa Lowasa kuhusu katiba mpya ukoje?
Manake kwangu issues anazosimamia mgombea ndio zinaweza kunishawishi kumkubali au kumkataa.
Usafi ni kigezo ila kwa kuwa kwa sasa hatuna msafi then naweka pembeni
Kwangu katiba mpya ni muhimu sana na natamani mazuri yote yabaki na mabaya yatolewe kabla haijapitishwa.
 

Zaidi ya Zitto, sidhani kama kina Mbowe na Dr. Slaa walikuwa na nia ya kupigania waTanzania hohehahe. Mbowe na Slaa lao kubwa ni madaraka na hawajali watakavyoyapata. Kumfukuza Zitto ilikuwa ni kwa sababu ya tofauti hiyo ambapo Zitto alitaka kuongoza chama ili kiwe na msingi ya kupigania waTZ na sio kwa lengo tu la kuingia ikulu. Kwa CHADEMA kumkumbatia Lowassa, yule yule wa 'List of Shame', ni kuthibitisha tu zile tofauti zao na Zitto.
 


Raisi (EL) atafanya nini pakiwa na idadi kubwa ya wabunge wa UKAWA?
Assumptions ni kitu kibaya sana. Msi-assume kwamba UKAWA hawajayafikiri haya mnayowatahadharisha nayo.

Ndoto za mwendawazimu??
 

So now you support the most corrupt leader ever, in Tanzania, E. Lowassa, just because he is with CHADEMA? Who will stop Lowassa from being a corrupt leader if he becomes the prez, i.e. the most powerful Tanzanian? How is Lowassa better than, a so far non corrupt Magufuli?
 
Chadema imefikia lango kuu haina haja ya kubishana atangulie nani. angalieni maadui watawakuta hapo nanyi mtashia hapo. hapo itakuwa kilio na kusga meno. wafuasi wenu mtawaambiaje. Ingieni ndani kwanza na yule alieshafika mbele asivutwe shati! Maana nyuma yake watu wengi wanamhimiza INgiaaa! Ingia! Ingia! umati mkubwa!
 

I hear you Rev.

Twende kazini sasa mavuno ni Mengi. tutashinda, tutarekebisha..

Lakini kwanza tutashinda!!

Comrade,
 

Bwana Character X wewe sikujui ni nani in personal ila labda nikuulize. Unasema adui yetu ni ccm.
1)Naomba utusaidie kueleza ni adui yetu kwa mambo yapi hasa kwa sasa ili iwe rahisi kuyaeleza mambo hayo kwa wananchi.
2) na kama ccm ni adui yetu je sisi tuna matazamio gani kama endapo tutashinda uchaguzi mwaka huu.
3)
 

Bwana Character X wewe sikujui ni nani in personal ila labda nikuulize. Unasema adui yetu ni ccm.
1)Naomba utusaidie kueleza ni adui yetu kwa mambo yapi hasa kwa sasa ili iwe rahisi kuyaeleza mambo hayo kwa wananchi.
2) na kama ccm ni adui yetu je sisi tuna matazamio gani kama endapo tutashinda uchaguzi mwaka huu.
3)je tumejipangaje kuundoa mfumo uliotoka ccm na kuhamia ukawa kwa sasa kwa sababu najua ni limfumo lipana sana na lina mizizi mireeefu sana.
Usituambie tu adui yetu ni ccm basi unaishia hapo. Weka mambo wazi, vinginevyo tutajua sababu hasa ni kutaka tu madaraka na iwe zamu ya kutawala na si vinginevyo.
Unashawishi wananchi wapambane kuitoa ccm ili nasisi tuweze kula keki ya Taifa zamu yetu hahahah! Hizo zitakuwa fikra potovu na mbaya sana tutakuwa tunazipandikiza. Kama hakuna hoja kwa sasa, ili kulinda amani ya nchi yetu ni bora tujitahidi tuongeze wabunge tuu na ccm iendelee kujisafisha na kutawala, fullstop. Hakuna raslimali ya kuanza kugawa eti kwa zamu wakati majority wanahangamia.
Kuna watu wanajifanya eti wazalendo wanataka vitalu vya gesi wapewe wazalendo. Sijawahi kuwaelewa hata kidogo. Yaani badala ya kuipa kampuni ya ummamiliki hiyo apewe mtu binafsi kwa sababu ya uzalendo. Tunakuwa tunanufaisha mtu binafsi au watanzania kwa ujumla.wao? ??
 


Raisi (EL) atafanya nini pakiwa na idadi kubwa ya wabunge wa UKAWA?
Assumptions ni kitu kibaya sana. Msi-assume kwamba UKAWA hawajayafikiri haya mnayowatahadharisha nayo.

How can you say assumptions ni kitu kibaya sana, while you have just made one assumption yourself? Idadi kubwa ya wabunge wa UKAWA, you are assuming that they will be loyal to UKAWA and not the guy who was ceremoniously brought in to help UKAWA!! And i didn't make any assumptions, i made a number of observations and gave my opinion based on those observations.
 

Tutasubiri, katika kusubiri huko ndipo pia tutafahamiana vizuri hulka na tabia.

Na pia tukubaliane kuwa bado tutaelewana ikiwa wewe ulikataa langu nami nikikataa lako na bado safari itaendelea kwa msigano!!!

Uzuri boti usiyokuwemo ikizama utahadithia.
 
Adui wa Tanzania ni CCM kwa attribute ya ufisadi tu. Ufisadi ndo uliotufikisha hapa tulipo kwa mashua ikiwa ni CCM kwa sababu ya ufisadi. Lakini manahodha walioifikisha hapa CCM kwa sababu ya ufisadi wamekitekeleza chombo cha mashua CCM, na kutimukia ktk mashua CHADEMA, ili kuwafikisha CHADEMA walipowaacha CCM. Very interesting.

Na ukiiondoa attribute ya ufisadi ndani ya CCM, hivi adui wa Tanzania anakuwa ni nani? Kwi kwi kwi kwi
 
Nliwah kusema na nitasema tena Mnisamehe tu kama nitawakwaza. DR SLAA SI PRESIDENTIAL MATERIAL. mimi si CCM wala CDM ila napenda niseme kwa uwazi Dr Slaa si Mtu wa kuwa Rais. huyu anafaa kuwa Mbunge. Niliwatajia matatizo kadhaa ya Dr Slaa. Ila niwaambie kama Dr Slaa atajitoa aua mejitoa CDM si kwa sababu eti tatizo ni shutuma za Lowassa. Dr slaa anaamini anaweza kuwa rais wa tanzania. mke wake anaamini anaweza kuwa first lady na hivyo kulipiza kisasi kwa yote aliyotendewa kipindi kile cha kufanyiwa vurugu mpaka ujauzito kuharibika. tukubali tusikubali uzito wa Dr Slaa na ED Lowassa ni tofauti sana. Lowassa ana uzito jaman. hata akisimama yeye mwenyewe peke yake ana uzito ukiacha chama. dr slaa anabebwa na chama pia. hivi unadhani kwa siasa za kawaida J.Mbilinyi sugu angeshinda MBY kama si kubebwa na chama na wananchi kuwa na chuki na CCM? ndiivyo ilivyo kwa dr slaa. sina tatizo naye hata kidogo ila kwa Urais hatoshi. Kama kuna nia dhabiti ya kushinda vita kila silaha hutumika. wazungu wanase,a " ALL IS FAIR IN LOVE AND WAR" watanzania wamechoka na CCM NA DR SLAA hawezi pambana na Magufuli, hawezi pambana na CCM. kuiangusha CCM INABIDI KUIMEGA,KUIPASUA. kwa sasa lowassa ni mtaji mkubwa. huyu atakuja na siri zinazotumika kuiba kura CCM. atakuja na watu weng ambao wamemkubali, huyu anaijua CCM vibaya sana. ni sawa sawa na unapigana vita kuingia Nchi ya adui kumwondoa halafu kamanda wake mmoja akaamua kujiunga nanyi... huyu hudhan kama anapaswa akae mstari wa mbele kuwasaidia kuingia ndani ya nchi husika kwa kuwa anajua kila kona na vichochoro? anafahamu udhaifu wa adui yenu? kama mnataka ushindi vitani mtatumia kla silaha inayopatikana kupigana na adui yenu. hakutakuwa na muda wa kuchagua uhalali wa silaha husika. KAMA LOWASSA ANA UFISADI HIVYO ASINGETHUBUTU KUTOKA CCM maana anajua CCM WATAMWANIKA HADHARANI. FISADI HAWEZI HAMA CCM hata siku moja. KWA FISADI CCM NI BABA NA MAMA YAKE. nani anathubutu kukihama na kukipinga chama kilichomsaidia kufanya ufisadi? nadhan NYERERE ALIPOTISHIA KUHAMA CCM nini kilimpa ujairi huo? coz alijijua alikuwa safi. leo HII MKAPA, MWINYI KIKWETE hata watukanwe na wadhalilishwe vipi hawawezi hama CCM. hawana ujasiri huo kwa kuwa wanajua siku wakihama ni mengi yatafunuliwa kuwafuata nyuma yao. CDM mtumie LOWASSA. DR SLAA aache ubinafsi. aangalie maslahi makubwa ya umma, ya watanzania, by the way kama watanzania wataamua safari hii kumchagua fisadi waachiwe. jiulize wamewaza nini kuamua kumchagua fisadi na kuacha watakatifu wengi waliopo? by the way MAGUFULI SI MSAFI. system ina mbeba tu angalia report za CAG.
 

You Sir, misread me. I do not support Team Lowasa ruling us, not even through the machination of taking over CHADEMA first. Changing from Team Kikwete to Team Lowasa is not a real change. No, Sir, I am for real and substantial change, a change that would usher in the rule of law and zero tolerance for corruption.

I am baffled. What would it benefit CHADEMA to win Lowasa and lose Tanzania?
 

Mwalimu, kuna maswali ambayo ukiyafikiria majibu yake unaogopa kweli kweli. Wengi tunataka mabadiliko na siyo madogo hivyo; tunataka CCM ing'oke kweli kweli. Lakini huku kung'oka ambako tunaahidiwa sasa hivi kunaacha mengi sana ya kutamania. Regime change just for the sake of regime change has proved in a number of countries now to be exercises in futility. Hatutaki kubadilisha uongozi tu ilimradi tuseme tumebadilisha. Wananchi wa Zambia walipomuondoa Kaunda wakiongozwa na Chiluba waliamini kabisa kuwa lengo leo limetimie; wameking'oa chama kilichotawala tangu Uhuru madarakani. Well, boy were they wrong.
 

But CHADEMA seems to have already declared that Lowassa is their prez nominee, why keep on crying over CHADEMA rather than picking a better alternative? What's wrong with ACT-Wazalendo or Magufuli?
 

Kumbe na Zitto naye mlimsingizia tu kama mlivyomsingizia Lowasa. Watu wabaya sana ninyi. Zitto amehama na Lowasa amehama na wote wametuhumiwa na CHADEMA.
Kumbe hata ufisadi mwingine mnaosema kuhusu CCM ni uongo tu. Na System mnayosema ni uzushi tu. Hamna lolote la kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…