.....wasomi kama nyie tunawaheshimuni kwa kuyafuatilia mambo ya harakati za ukombozi wa pili wa mama tanzania kiusomi..kuna vitu mmesaidia sana katika harakati, na kuna vitu mungeweza pia saidia sana ktk harakati za ukombozi wa pili wa mama tanzania..lkn bahati mbaya, ukweli wa "kikombe kilichoja kimiminika humwaga kimiminika, kikiongezewa kimiminika" umeendelea kujidhihirisha kila kukicha ktk harakati zetu tukufu....leo wengine "mitaani" (sisemi darasani au ofisini, au klabu za kikubwa ambazo unywaji wa "vya thamani" unapewa kipaumbele", nasisitiza, MTAANI..)..ufisadi unaishia kwenye kupora mali ya umma na vitendo vya rushwa tu?...tunatafakari., Majungu, Uzushi,Ghilba, na kila aina ya utapeli ktk HARAKATI ZILIZOTUKUKA haviwezi kuwa ni sehemu ya ufisadi ambao ulitakiwa ndo tuanze nao kwanza ndani yetu wanaharakati wenyewe? nani alipitisha na kututangazia habari ambazo "WAKATI", ( mama wa ukweli) amedhihirisha kuwa zilikuwa ni majungu, ghilba, uzushi, na utapeli ktk siasa?..kwa nini (wasomi wetu ktk harakati ) hamtuelezi kwa hoja zisizopingika, ni kwa uadilifu na uzalendo gani, tuendelee kuwasikiliza viongozi wetu wale wale ambao walileta majungu yaliyotufitinisha na waadilifu, wazalendo, wenzi wetu ktk harakati...tuelezeni ni nini kinaendelea kwa wale wote walio na nyadhifa ktk harakati ambao walipita wakitufitinisha na "mwokozi wetu" ktk safari ya matumaini..Je, si wakati sasa wa viongozi wetu ktk "harakati tukufu" kutuelezea pia ukweli juu ya waliyopita wakisema juu ya kina Hamadi Rasheed, Kitila Mkumbo,Zitto Kabwe na wengine ktk harakati, ambao kama Lowassa, tuliambiwa mengi juu ya namna kuwa nao kulivyokuwa kunasaliti harakati..huitaji kuwa msomi wa kiwango cha "usomi tunachofanyiwa nacho mbwewe na waliojaaliwa kuwa nacho" kufahamu kuwa majungu hayana mpaka..kama tuhuma za ufisadi za mh. Lowassa zilikuwa ni majungu, inayumkinika hata za wengine walioitwa wasaliti na kufukuzwa zikawa ni majungu pia..Lakini, lililo kubwa kabisa ni kutaka (labda?) kutuaminisha kuwa ili harakati zetu zifanikiwe, basi ni muhimu (kama si lazima), kuchanganya uadilifu ktk harakati, pamoja na, majungu, ghilba, uzushi, utapeli, na kuongeza "ufisadi na mafisadi" (kwa maana halisi ya ufisadi) ndani yake...kuna hoja gani iliyotukuka ya kiharakati,kuhangaika kuitoa ccm ambayo tayari ni mchanganyiko huo huo, badala ya kuanza kusafisha "mapandikizi" ya mawakala wa waovu, walio ktk mahaba na umasikini wetu (na kutokusoma kwetu-kama ni kweli)....ANGALIZO..wengi mitaani hatujasoma (labda kama mnavyoonekana kuamini), lakini tulijifunza, tumejifunza, na tunajifunza...kwa kusikiliza, kutazama, (ndio), na kusoma, kisha, (TOFAUTI NA WASOMI WENGI) tunatafakari...! ...Mungu atatujalia, mfumo uliopo wa CCM na WAPINZANI KOKO, tutaung'oa, na juu yake, kwa baraka zake mungu,tutaweka mfumo ambao msingi wake utakuwa ni demokrasia ya kiuadilifu, mfumo ambao "nidham ndio itakuwa kichwa chake"..huku majungu, ghilba, uzushi, utapeli, ufisadi na kila aina ya uovu wa kisiasa utakuwa ndio "jasho, kinyesi, na mkojo" wake...