Mzee Mwanakijiji, Tafadhali...

Mzee Mwanakijiji, Tafadhali...

Great day Comrades,

Leo nimedhani kuwa wakati muafaka kuandika kuhusu hili. imenichukuwa muda kwakweli, kukusanya ujasiri wakuandika haya hasa kwa heshima ya mtu ambaye nina panga kum address, na influence ninayoiona anayo kwa watu katika mitandao hii.. kum address hasa katika namna ya kujaribu kuubadili au kuukosoa mtazamo wake au kubadili approach yake kwa mambo, inahitaji confindence in ones own believe, and in the ability of the one you are addressing to sieve through your argument and pick out the insights put forward at the end of the day rather than pick up a fight.

Nimesoma posts zako nyingi, nyingi nikikubaliana na mtazamo wako kuhusu mambo husika lakini kadhaa nikitofautiana nawe kidhana (ideally or in concept), na wakati mwingine nikitafautiana nawe katika approach tu hakika.

Wakati wa rumors za usaliti wa ZZK, na kesi yake dhidi ya chama na hatimaye kufukuzwa uwanachama. wakati wa mtikisiko juu ya kesi ya kubambikwa ya kamanda Lwakatare na wengine hadi ushindi wetu kama chama katika hilo, na sasa wakati huu wa ujuio wa lowasa chadema, zote nyakati ngumu kwa movement hii, lakini kwote umetoa mawazo yako na hakika umekua mchango mzuri katika kutoa leadership kwa watu wetu... again, whether always right or sometimes wrong si swala sana, kimsingi you have always offered leadership, leadership ambayo watu wakiikosa hutoa hisia zao vinginevyo (na hatari ya husambaratika hua more real)

Nyakati zote za changamoto katika movement yetu ya mabadiliko kwa taifa letu watu wamekuwa wakitafuta uongozi kutoka kwa watu mbali mbali, wakati mwingine Uongozi rasmi wa chama kwamaana ya wenyeviti na makatibu and the like kimkakati na kisiasa wanakua si watu sahihi kutoa mawazo yao kuhusu maswala flani, umefanya vyema mara zote kuwa mstari wa mbele kutoa mawazo yako na mtazamo katika hali hizo ngumu na kwakufanya hivyo kuwapa watu the leadership they needed. Narudia whether leadership towards the positive or leadership towards the negative sihoja sana.

lakini Ilikufupisha bandiko hili, ninaomba kuzungumzia suala hili tulilonalo sasa. Baada ya kumpokea waziri mkuu wa zamani ndugu Edward Lowasa kukaribishwa UKAWA na kupokelewa na Chadema kama mwanachama na huenda kama mgombea uraisi kwa chama chetu yapo mengi yanayo zungumzwa.

kilichonifanya kukosa uvumilivu na kunibidi kutafuta ujasiri waku kuandikia waraka huu "wawazi" ni mtazamo uliyo uweka wazi ukiuita "Msimamo" wakutokukubaliana na move ya lowasa kuja ukawa/chadema na kugombea uraisi, ukizungumzia swala hili kama kuwatupa makamanda wako wa vita wa zamani kwasababu ya makamanda wa adui uliowateka.

while agreeing with this stand in principle, am afraid i differ with you in value. nina jua wewe umeelewa, ila wengi hawajaelewa, nitaelezea;

Wewe ni mtu mwenye influence kwenye jamii ya mitandao hii, maranyingi mtazamo wako una infulence mitazamo ya wengine wengi. in other words you are a leader!.. na nivizuri ulifahamu hili., i dont know you in person, hivyo sijui wewe ni nani hasa, na kama unacheo chauongozi au lah,(possibly adding my confidence:redface🙂 lakini hiyo haijalishi. Just by virtue of having the influence that you have on the public you are a leader! and you should know that!

Now there is a difference between a leader and a manger., and i know you know this. as a leader you are visionary, you look at the bigger picture, you influence and inspire unity towards the main target, yours are the policy issues, the corporate level affairs, you work to remind the people of the greater picture, the greater good. when people are overwhelmed by the emotions (positive or negative) energies that arise from events of the daily affairs of the corporate life, you remind them of what actually we are fighting against, who really is the enemy, leaders bring people together! leaders do not work to divide! leaders maintain the focus of the people! kiongozi na uvumilivu nivitu ambavyo huwezi kuvitenganisha, wakati mwingine kiongozi atayaona mambo yakifanyika tofauti na vile ambavyo anafikiri kuwa sawa, lakini kiongozi atatafuta kuangalia nini anataka watuwake wajifunze kutokana na yanayo tokea.. a leader is not a superintendent wakati mwingine you give room for error because you know that people learn from errors, and there is always a good side in every situation because you can learn. Mara nyingi nimekua nikipenda katika kuzungumzia kwangu tabia za viongozi kutumia kamsemo haka kwamba "wakati mwingine inambidi kiongozi kutafuna pilipili huku akitabasamu"

Kwahakika, inawezekana kabisa kukawa na kiongozi wa cheo (a leader by position) katika institution au jamii flani, lakini wakikaa mathalan kwenye kikao actually asiwe kiongozi pale, anaweza kuwa ndiye mwenye cheo pale, lakini si aliye kiongozi pale, kwanini??? kwasababu huenda yupo mulendani ambaye hana cheo lakini kwa influence aliyo nayo kwa wajumbe wenzake.. yeye ndiye hasaa kiongozi mule ndani.. ana influence mawazo ya wajumbe wenzake.. na wote wanamsikiliza., wanamuamini., wewe nikiongozi kwa influence uliyo nayo.

now because you are a leader! kwanza litambue hilo.

Pili, Sikatai mtazamo wako kuhusu kuto kukubaliana na kuja kwa lowasa na kupewa kugombea uraisi. sikatai wewe kuwa na msimamo wako., lakini ninadhani kwakua unaifahamu nafasi yako, nivyema ukakumbuka lengo kuu, ukakumbuka the real enemy ni nani., ukakumbuka what the vision has always been., ukajiuliza has it been to put someone in power?? or to keep the chadema idea only to the chosen ones and branding some of those that were not with us just not fit to take part in this movement for change??? or has it been kupambana na CCM na kuing'oa madarakani?

Which of the two is the bigger picture?? ukipata majibu ya hayo nimuhimu sana!! sana!! kuhakikisha kwa nafasi yako unainfluence kundi la wale wanao kusikiliza towards oneness, towards the purpose., muhimu kujiuliza je comment yangu kwakua nina influence inawapeleka wapi watu unao waongoza?

Hatakama msimamo wako ulikua wa dhati kabisa, kwamaana yakuwa ndivyo unavyo amini kabisa ndani ya moyo wako, kwamba tunakosea sana kuchukua kamanda wa maadui tuliye mteka na kumpa nafasi kuongoza hukutuki mrelief kamanda wetu wenyewe tuliye kuwa naye wakati wote wa mapambano. kwamba hii sio sawa katika mazingira yoyote!

Well, that may be what you really feel, and its not my intention to talk you out of that belief, lakini.. hapa ndipo unapotakiwa kuhakikisha the leadership that you give to the people that you have influence over is not just ANY KIND of leadership but the right leadership. A positive leadership!!! leadership towards achievement of the greater goal.,!!! making sure you influence them to see the bigger picture!! keeping the team together!

kiongozi hasemi tu hisia zake iliwatu wasikie anavyojisikia kuhusu jambo flani, no! unasema kwa lengo!

Mawazo yako yanayoweza kuvunja umoja wa jeshi lako hatakama ni mawazo ya dhati kabisa na mawazo sahihi kwa mtazamo wako ila hayawezi kutoa a positve leadership to the poeple in approaching towards the greater goal, hayafai kusema!!

ndiyo maana watu flani husema "If you think what you you have to say is not anything positive,keep it to yourself"

Muhimu sana kuzingatia hili kama kiongozi, its not about hisia zako binafsi really. na hii imfikie na Zitto Zuberi Kabwe!! maswala ya kuja na misimamo na conditions za azimio la tabora ilikujiondoa kwenye umoja halafu tunadai eti tunataka ukombozi wa dhati wa Nchi hii kutoka mikononi mwa CCM nadhani ni kuwa very self destructive!!! muhimu sana wote tukazungumza lugha moja! tukapigana vita moja!!

Mimi nadhani wakati kama huu ni wakati ambao movement yetu iko at the vulnerable stage, tumekaribia sana kufikia lengo letu kuu,.- kung'oa CCM. lakini style ambayo nguvu hii ya kumpiga adui imepatikana huenda ikashababisha maumivu kwa wenzetu wachache! na niseme tu itawaumiza tu wale ambao watashindwa kutazama the bigger picture!!

Nina mpongeza sana Mr. Freeman, anafanya kazi nzuri, uwezo wake wakuwaongoza watu towards whta the next right move is hauna mashaka.

ninawaomba sote!, akiwemo ndugu yetu daktari (wa filosofia) W. P Slaa ambaye juzi tu niliandika uzi mwingine niki acknoledge uwezo wake mkubwa na kumuomba asikubali kupandikiziwa hisia negative za retaliation na kuzira na nini ambazo zinapandwa na hao hao wasio itakia mema movement hii (ambao ni CCM hao hao)

Naniwaomba sote ambao tuna influence kwanamna flani hatakama ni kwa mtu mmoja tu mwingine, let us influence them positively!!!

lengo kuu hapa ni kuing'oa CCM.!!!! Mzee Mwanakijiji baada ya yote tuliyo yapitia katika mapambano haya! napenda kuamini hatutakuwa tena sababu ya kutukwaza kufikia lengo letu kuu- kuing'oa CCM!!

ikumbukwe; Siasa niupepo! watu tunaowapa matumaini kila mwaka wa uchaguzi kuwa ushindi unawezekana CCM inang'ooka!! halafu uchguzi unafanyika tunashindwa uchaguzi tena na CCM, si wote wana mioyo mikuu na uelwa wa vita hii na wanaweza kupambana hata kama ingechukua miongo kadhaa au hata maisha yao yote katika mapambano kabla ndoto yetu haija timia, wengine wata kata tamaa., watakapo ona havitimii, kazi yetu itazidi kuwa ngumu!

Mitaani huku tunawasikia wananchi wakisema "CCM isipo ondoka mwaka huu haitakaa iondoke"

Nimeupenda msemo wa bwana mmoja niliuona humu ndani akisema "Chadema Tuna Gawana Majukumu Hatugawani Vyeo" muhimu sana kukumbuka hii.

This time we have a chance!! a real chance!! and am sayi we have a chnace NOT beacause lowasa kahamia upinzani, lakini kwasababu CCM inajibomoa yenyewe!!! nimesema let us propagate that!! wacha wapasuane kabisa!!!! tunapokwenda kwenye uchaguzi tuwamalize kabisa!!

let us not waste our energy in self destructive efforts!! adui yetu tunamjua!! lets not let them survive this last blow!

Mzee Mwanakijiji, Comrade,

Ninakushukuru Sana.

Japo unao uwezo wa kujenga hoja vizuri. Lakini, kitu kinacho niudhi ni jinsi unavyokiharibu kiswahili kwa kuchanganya na lugha nyingine! Si kila msomaji anaelewa lugha ya kiingereza. Jaribu kutumia lugha moja tu katika maandishi. Kama ni kiingereza,basi iwe hivyo mwanzo hadi mwisho na kwa upande wa kiswahili vile vile.. Ukurasa au Uwanja huu wa majadiliano unalenga hadhira ya watanzania, na natambua wote wanaelewa lugha ya kiswahili vema. Ombi langu kwako, wasiliana kwa lugha yao ya kiswahili!
 
Tafakari kwanza what is behind Lowassa kuingia Chadema ndo uje kumshauri Mzee Mwanakijiji.

Sasa ndo naelewa kwa nini wanasema half knowledge is dangerous than total ignorance? Yani kama hii ndo thinking yenu sishangai wale walioaminishwa Gaddafi ndo mbaya na atoke na leo wanashangaa Gaddafi katoka ila yaliyowakuta ni zaidi ya hata yale waliyokuwa wanayawaza.

I feel sorry for you.

Lord Denning, kimsingi nashangazwa na hii hoja ya kuig'oa CCM kama jambo muhimu sana katika uhai wa taifa hili bila ya kuwa na uhakika wa hali itakuwaje baada ya kutangaziwa ushindi? How can the oppressors lead the way of the oppressed. Nadhani hapa kunatatizo la msingi sana, naanza kuyaona yaliyotokea Libya na sasa hakuna wa kulinusuru taifa lile. Kwa nini sifa ya ukombozi apewe adui? Nani hakushuhudia unyonyaji unaoongozwa na Lowasa na watu wake( Chenge, Karamagi, Rostam ) kwa kutaja mifano michache? Nina ukakika uwezekano wa kupoteza pambano hili ni mkubwa kwa kuongozwa na Lowasa kuliko kama asingekuwepo.

UKAWA walikuwa bora na salama zaidi bila Lowasa kuliko baada ya kuwa naye. UKAWA imeisambaratisha CCM, sasa inaishangaza kutanguliza mateka/majeruhi wa kivita kukuonyesheni maficho ya jamaa zake akiwa na zana bora kabisa za maangamizi. Sijawahi kumuona kamanda mpumbavu kama ninaowaona UKAWA kwa sasa. Historia itatuhukumu wote. Mbinu inayotumiwa, haijawahi kufanikisha vita yeyote ya aina hii, Libya wameshindwa, Southern Sudan wameshindwa, Somalia wameshindwa kabisa, Afganistan wameshindwa. Mzee Mwanakijiji nionyeshe ni wapi waliotumia mbinu hii dhaifu wakashinda? Ujasiri unaletwa na nini katiaka vita hii?
Lowasa hawezi kuwa na wafuasi kuzidi CCM kwa ujumla wake, yeye amemega kipande japo ni kikubwa kwa mtu mmoja. CCM inadai kuwa na wanachama millioni 6. Lowasa alipata wadhamini 800,000 tu, hata tukimpa washabiki na wapenzi wake mara mbili zaidi ya waliomdhamini atakuwa na wafuasi wasiozidi 2,400,000 tu. Kiasi hiki kwa ukubwa kinapunguza wafuasi wa CCM sio UKAWA!!. Lakini bado kama Lowasa angekuwa anapambana na CCM bado angeshindwa kwa kura zisizopungua laki mbili!! UKWA ilikuwa na kazi moja tu, kushawishi wapiga kura million 15,000,000. UKAWA ingeshinda bila Lowasa.

Na hii ndio itakuwa sababu ya kushindwa kwetu; sasa kampeni zitaanza kuhitaji fedha kwa sababu Lowasa amezoea kugawa fedha. UKAWA/ upinzani tumekuwa tukishinda bila fedha, watu wanashinda njaa kulinda kura. Nionyeshe jasiri wa kushinda njaa sasa, nionyeshe mtu wa kuvumilia rungu la polisi katika mazingira haya. Nani awetayari kupambana na polisi kupinga mwizi wa kura. UKAWA mmevuja moyo wa ujasiri, wapiganaji wamelowa, wanabaridi. Na nyinyi mmekuwa kama Kikwete, akijua alichokifanya hakifai katika mchakato wa kumpata mgombea wao, anahitimisha kwa kusema, kura za maoni zimekwisha na mgombea wa CCM amepatikana, sasa ni wakati wa kuvija makudi yetu na kubaki na kundi la CCM tu. Msisahau na Lowasa alikuwemo katika mkutano huo. Hebu sasa niambie ni kweli makundi yalivujika? Achani kujidanganya.
 
Shetani ana tabia moja. Huwa ni muongo muongo. Yaani CCM wanahaha nini? Mbona ccm imetulia kabisa? Mi ni moja ya watu ninaokataa ujinga wa kuuza demokrasia kwa bil 10 leo wewe unatete. Mshenziii wewe na ujingaa wako. Unajua kabisa Lowassaa ni mwizi hata CCM alikataliwa tena mapema leo hii kwenu siyo mwizi. Tena mbowe kuna siku alihimiza Lowassa achomwe moto leo hii unatetea? We taahiraa. Ujua kuwa mi ni mpenda mageuzi sipendi kuona upinzani unakufa! Mbowe kaingia kingi ya marando na apson bila kujua. Time will tell wewe subiri na ujinga wako,

mwizi kwa mujibu wa sheria anafanywa nini? au hujui na hilo pia. Kaeni vizuri dawa iingie hahahaha
 
Nimejifunza kuna watu wana busara sana japo wavurugaji pia wamo humu. binafsi mfumo wa ccm siupend ila approach ya kuuondoa ndo naona nayo ina tatzo kama wengi humu pia walivyochangia. wengi wanachangia kua lengo kuu ni kuiondoa ccm halafu iweje? ni hatari sana kuanza safari ambayo hujui unapokwenda. muhimu sana kabla hujaianza lazim ujue unakwenda wapi(underline principles) tunaweza fananisha na misingi y kufuat katika kufanya jambo ambayo cdm ilikua nayo toka inaanzishwa.inatia shaka kuona misingi inabadiliswha je kuna uhakika gani kwamba baada ya ushindi misingi ya awali itarejelewa? ndio tunatak mabadiliko lakini ni lazima tujue ni mabadiliko yepi tunayoyaendea(clear objectives) ili kuweza kuthibiti hali na kuyatathnini baada ya muda fulani.kama mabadiliko tunayoyahitaji hatuwezi kuyapma baada ya muda fulani ni bora yasiwepo sababu tutafika mahali kazi itaharibika kabisa. na hapa ndipo naona hojaya MM sababu anahis ile misingi ya awali imeachwa sasa lengo limekua ni kuiondoa tu ccm. pia nafkiri amehisi hakukua na marithiano ya kutosha(japo inakanushwa lkn hali inajionesha) ndio maana akasema unamuweka askari wako pembeni. ningewaheshimu cdm sana km wasingempokea lowasa kabisa hata wangeeleza kila mtu angewaelew kutokana na misingi yao toka awali na wangeisumbua ccm sana. askai wengine cdm kinachowasuta ni intellectulism yao sio kwamba hawaamini kwamba lowasa huenda si fisadi ila mazingira walojiwekea na tamaduni zao zinawafanya washindwe kufanya kaz n lowasa. kwa hyo ni muhmu sana kuangalia japo mfano wa libya hatutafika ila wasiwasi ni kipimo ch akili maraisi wa nchi zetu hizi wana nguvu sana. na histori inaonesha kwamba wapigania uhuru wote hawakufanya kazi pamoja baada ya uhuru kupatkana mfano kenyata vs onginga oginga( na hapa nkipo kaburi la pan africanism lilipochimbwa)
 
Kuiondoa CCM madarakani ni sehemu ya safari, na sio safari yote. Lengo letu sisi lilikuwa ni kuleta utawala wa kisheria na kutokomeza ufisadi. Ukiitoa CCM lakini ukaendelea na watu wale wale utafika?

Kama walivyoelezea wengine, ujio wa Lowasa hauji na Lowasa peke yake. Unakuja na watu wengi sana, wakiwemo na waliopanga maovu dhidi ya CDM na Watanzania huko nyuma. Unakuja na watu ambao sio CDM, na hawatakaa wawe CDM kwa moyo wao.

Lowasa ameungana na CDM lakini hakujiunga CDM. Lowasa hana wala hawezi kuwa na mtazamo wa CDM, wala hatakaa awe mwana CDM kimoyoni. Amepata tu nafasi ya kutumia CDM. Na akishafikia lengo lake hatakuwa na nafasi ya kujihusisha sana na CDM.

Oh God, how come that something that was going so well could take such a bad turn? How is it that just when we thought we had reached the top we find that we have in fact hit bottom?

I declare again
that I have not lost trust with Dr Slaa. How could I do that when I have trusted him for so many years? I await his guidance on this. Kuna wakati niliandika kwenye hii forum (2009?)kumwomba Dr akubali kugombea Urais. alijibu kwenye hii hii forum, na majibu yake yalitia moyo. Namwomba tena atupe mwongozo sasa, kwani wengi wetu tunajisikia vibaya.

Why support/be a follower of Dr. Slaa while he has neither complained nor dissociated from the new corrupt leadership?

I believe that he does not want to dismantle everything. There is too much at stake. I don't want him to give room to CCM to win. He must be considering the lesser of the two evils. Would it be better to have Lowasa rule through CDM or to have Magufuli rule us through CCM? Let us give him time to come out and speak to us, his loyal supporters.
 
Mwalimu Augustino, na wengine; niwahakikishie kuwa sauti za wapenda mabadiliko ya kweli zinasikika kwa ukubwa wake wote (loud and clear). Ni matumaini yangu kabla ya siku chache zijazo maamuzi sahihi na ya lazima yatachukuliwa yote yakilenga siyo kuing'oa CCM madarakani tu kama baadhi ya watu wanataka bali kuleta uongozi na utawala bora kuliko ambao umetolewa na CCM au unaopendekezwa na CCM katika uchaguzi huu. Nawaomba tuwe na subira kidogo; yote hayajapotea bado.

MMM
 
Its not over until is over, this drama is continuing to unfold.

Bado sijapata jibu kwa nini Mbowe amemkumbatia EL? Yanayotokea hivi sasa CHADEMA yanatia mashaka sana ..... ...... unakumbuka wakati watu walisema kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga na ni chama cha kikabila ambacho maamuzi yake yanaongozwa na ukoo wa Mbowe et al? Pengine sasa hayo yana ukweli maana siku zote ukweli hushamiri. Je, unakumbuka nguvu kubwa ilivyotumika kuifikisha CHADEMA hapa ilipo? They might have forgotten but voters will never.

Kama EL atapewa tiketi ya kuomba urais kupitia CHADEMA basi huo ndio mwisho wa CHADEMA. Mark my words, EL will never be a president of this country never.
 
Kuiondoa CCM madarakani ni sehemu ya safari, na sio safari yote. Lengo letu sisi lilikuwa ni kuleta utawala wa kisheria na kutokomeza ufisadi. Ukiitoa CCM lakini ukaendelea na watu wale wale utafika?

Kama walivyoelezea wengine, ujio wa Lowasa hauji na Lowasa peke yake. Unakuja na watu wengi sana, wakiwemo na waliopanga maovu dhidi ya CDM na Watanzania huko nyuma. Unakuja na watu ambao sio CDM, na hawatakaa wawe CDM kwa moyo wao.

Lowasa ameungana na CDM lakini hakujiunga CDM. Lowasa hana wala hawezi kuwa na mtazamo wa CDM, wala hatakaa awe mwana CDM kimoyoni. Amepata tu nafasi ya kutumia CDM. Na akishafikia lengo lake hatakuwa na nafasi ya kujihusisha sana na CDM.

Augustine umenena! Hiyo ya safari na lengo ndo muhimu kwani wengi wetu independents tuliompigia kura Dr Slaa 2010 tumeshtuka kugundua kuwa muda wote akilini mwao walitaka kutwaa madaraka "kwa gharama na njia yoyote ile". Na kumbe walitumia tu hoja ya kupinga ufisadi kufikia lengo lao hii ili kutudanganya. Na sasa wameona hoja ya anti-ufisadi hauwafikishi so "if you can't beat them, join them"
Kiukweli Lowassa hahitaji kuvaa uCDM kwa sababu kumbe kiuhalisia uCDM ni kutwaa tu madaraka. Hata mashabiki na viongozi wanasema kuwa wanataka kuing'oa CCM tu ambayo ni tafsida ya kusema tunataka kuingia Ikulu kwa gharama yoyote. Hivi kwa mantiki hii Lowassa fits in perfectly na CDM na Ukawa. Wale ambao waliamini kweli ktk utawala wa sheria, utawala bora, haki, wameambiwa wasipopenda waondoke. Na ndiyo maana Dr Slaa kajiondokea. Wasiyo na haya kama Tundu Lissu wamebaki.
Hivi kweli wanaweza kusimama jukwaani na kusema kuwa waliamini ktk rasimu ya Warioba na Katiba ya Wananchi? Au kwamba waliposimama juzi kuhusu Tegeta Escrow walichukizwa na ufisadi huo?
Wametufedhehesha sana!
 
Attachments

  • 1438397129510.jpg
    1438397129510.jpg
    58.2 KB · Views: 145
Wewe Mwanakijiji na mfuasi wa Membe aka joka. Na umekula hela za mmarehemu GGhadafi, lakini pia uko umekaa nyuma ya computer yako huko Houston, Texas halafu unatumia remote control kujaribu kutuchagulia kiongozi wakati matatizo tunayoyapata toka kwa hawa viongozi tulionao sasa ni makubwa mno. Hapa ninapoandika mgao wa umeme kwa sasa ni masaa 12 kwa siku na raisi wa nchi hajawahi hata kuongelea yuko safarini halafu wewe uje na Membe wako. Hatukubali, walichofanya Chadema ni kuwarushia nyani nyie wanafiki, utajua mwenyewe kama umdake au umkwepe

Mwalimu Augustino, na wengine; niwahakikishie kuwa sauti za wapenda mabadiliko ya kweli zinasikika kwa ukubwa wake wote (loud and clear). Ni matumaini yangu kabla ya siku chache zijazo maamuzi sahihi na ya lazima yatachukuliwa yote yakilenga siyo kuing'oa CCM madarakani tu kama baadhi ya watu wanataka bali kuleta uongozi na utawala bora kuliko ambao umetolewa na CCM au unaopendekezwa na CCM katika uchaguzi huu. Nawaomba tuwe na subira kidogo; yote hayajapotea bado.

MMM
 
Miaka kadhaa iliyopita, niliwahi kuhoji wazi kuwa Siasa zetu zina mirengo gani au itikadi gani? Nakumbuka Mkandara alinijibu kuwa Tanzania hakuna itikadi au mirengo.

Tunachokiona ni mufilisi wa Kisiasa. Chama kukosa Itikadi inayoeleweka na kushabihiana na wananchi.

Leo hii, chama kinavutaka kati ya Neo Ultra Conservatives, Centrists na Liberals lakini hawana itikadi hata kidogo ya kusema Chadema ni chama cha siasa za namna gani.

Ukweli ni kuwa Chadema hakikuwa na hoja yeyote ile kujiuza zaidi ya Ufisadi.

Najiuliza kaam leo kwa mazingaombwe CCM wamediriki kumng'oa kwa makusudi kabisa hata kukiukwa demokrasia mtu ambaye angekuwa kibwagizo cha Chadema kwenye uchaguzi kutokana na hisia na taswira ya Ufisadi, leo hii Chadema wanakwenda Uchaguzi mkuu na agenda gani? Je ni agenda ya kiuchumi, kisiasa, kijamii au kimaadili?

Nzkumbuka nilipoandika Chadema must Reform, na matusi ya kuitwa msaliti kisa nilihoji People's Power!

Sasa Chadema wameamua kumfuata Malcolm X "by any means necessary" kama jinsi Kikwete siku ya Mkutano Mkuu aliposema Magufuli atawapeleka CCM Ikulu, Chadema imewekeza macho yote Ikulu!

Si Siri Lowassa anakuja na wasifu mkubwa sana wa kimfumo, kiuongozi na influence. Lakini, je Manifesto ya Lowassa alipotangaza nia akiwa CCM inaendana na Ilani ya Chadema au hata ya Ukawa?

Je katika ushirika huu wa Ukawa, leo hii Chadema wakiamua kunyoa badala ya kusuka na kufarakana kutokana na hamu na tamaa ya kwenda Ikulu iliyowafanya kuingia mkataba na wengine je haitaipa CCM ushindi mkubwa na hivyo kuua kabisa upinzani ukizingatia tayari CCM ina kundi la vijana walio tayari kuwa viongozi wa chama na Serikali 2020 na hata 2025?

Nitasema hivi kuhusu ninavyompima Lowassa pamoja na kuandika mengi kuhusu yeye miaka kadhaa na mpaka kukajengeka dhana kuwa mimi ni mfuasi wa Lowassa.

Lowassa ni Gladiator, anaingia ulingoni akijua ama atatoka hai au atatoka maiti na he has nothing to loose. Lowassa anatafuta uwanja wa kwenda kupigana hata kama itakuwa ndio mapigano yake ya mwisho. He has nothing to loose anymore.

Hivyo, ni lazima Chadema watafakari watakachokifanya na mapokeo hasi ikiwa watawageuka Ukawa na hata credibility yao kushuka zaidi.

Kitendo cha wao kuwa mstari wa mbele kumpokea Lowassa kimewaweka katika predicament mbaya, credibility imeshaingia maoda na walakini kwa kuwa miaka yote 10 iliyopita, walikuwa na hoja moja tuu kama kipaumbele cha kujinadi kwa Taifa na kilianzia MwembeYanga na orodha ya Mafisadi na hadithi za mafisadi.

Lakini hoja yao imejikita zaidi katika watu, mtu mmoja moja na si mfumo mzima ulioleta na kulelea ufisadi.

Ukiondoa fukuto la Zitto akiwa PAC kucharurana na mashirika na hata kuhakiki Serikali, sijaisikia Chadema ikileta hoja au muswaada bungeni wa kurudisha maadili au kuhakikisha matumizi mabaya ya fedha za Serikali kama ripoti ya CAG inavyosema miaka nenda rudi.

Hata kama kura za Chadema zingekuwa ni 10 tuu, na CCM wakipiga kura ya wingi ya hapana, lakini at least ingeonekana wazi kuwa suala la vita vya ufisadi si mikutano ya kutaja majina na tuhuma bali ni kuwepo na msukumo wa kujenga mfumo fanisi wa kisheria ndani ya Serikali hata kumpa DPP na AG uwezo wa kuwa huru kupeleka mafaili Ikulu kupata kibali cha kufungua mashitaka!

Option walionayo sasa Chadema na ni likely inabidi waimeze at this last minute ni ama kumtema Lowassa na kukiri kwa Watanzania kuwa alibugi stepu au kumkubali Lowassa na kuungana naye "kuiangusha" CCM si Ikulu pekee bali hata Bungeni (kumbuka chama chenye viti vingi inatoa Spika na Waziri Mkuu).

Hili liwe fundisho la mwisho kwa vyama vinavyojiendea tuu bila kuwa na itikadi inayoeleweka.

Leo Ilani ya Ukawa ni kubwa kuliko ya Chadema kutokana na makubaliano ya Ukawa. Je Chadema na hasa lile kundi la Neo/Ultra Conservative wa Chadema (rafiki na kaka yangu Mwanakijiji akiwa kundi hili) liko tayari kuheshimu uamuzi wa umoja wa Ukawa?

Chadema haina uwezo kuiangusha CCM pekee yake bila kuungana na wenziwe. Kitendo cha kufarakana na Zitto na hata kutoa mwanya kwa Zitto kuanzisha chama na kukinadi kwa itikadi kwanza, kinaashiria mpasuko wa kifikra ndani ya Chadema kutokana na kukosa Itikadi na Sera inayoeleweka na kuaminika.

Nasikitika kuwa inabidi niungane na Mwalimu Augustine na Susuziri kusema jitihada zote za kujenga Chadema kifikra na kiitikadi zimeishia hapa.

Sasa ni lazima wasuke twende kilioni, waungane na Lowassa kama wamoja, wameze nyembe na ego binafsi na kufanya kazi pamoja kuwadhihirishia Watanzani akuwa lengo la kuing'oa CCM ni la dhati na ikiwa watashinda uchaguzi (Ukawa), lazima watuonyeshe kuwa wao si sawa na CCM kwa vitendo na si hotuba za majukwaani.

Ni aibu kubwa sana kusikia tetesi kuwa kuna mfarakano na kukosekana kwa msemaji mkuu kujibu hoja au kutoa ufafanuzi wa kinachojiri.

Lowassa anarudisha fomu wikiendi hii. Je wale conservatives wakisusa, wakazira na kujitoa, atakayeumia ni nani?

Uchaguzi huu ulikuwa na slogan mbili: Its economy stupid and we want Change and not more of Same... lakini uhalisia Chadema na Ukawa wamebidi kumchukua Lowassa na hivyo wanagota kati ya Change na More of the Same... CCM wanaponea hasira za mkizi na hata yale maswali magumu kwao kuhusu uchumi wa Taifa yatasahaulika kutokana na Chadema kukwama mchangani kutokana na tofauti hizi za kimtazamo na itikadi isiyokuwepo.

Ni wazo la Mchungaji jioni hii!
 
Katika sakata hili la Lowassa kuhamia Chadema kuna vitu vya kuzingatia;

1. Mpaka sasa hakuna yeyote anayejadili sera ya kilimo, elimu , afya , miundombinu, uwekezaji , mambo ya nje, ulizi na usalama, michezo na utamaduni, hali ya hewa, nishati na madini, muungano na mambo mengine muhimu kwa taifa.
Hili ni kosa, lakini si kubwa sana kwa vile ilani za uchaguzi hazijaanza kutangazwa.
Hata hivyo, hapa tunajifunza kuwa ratiba ya kuchagua mgombea kabla ya kuwa na ilani sio sahihi. Inafanya mijadala ijikite kwenye personalities rather than real issues.

2. Kila upande unaweza kuathirika au kunufaika na maamuzi ya Lowassa kwenda Chadema kama ifuatavyo;
i) CCM
Faida
a) Kupunguza lawama za kuitwa chama cha mafisadi. Chadema wameshaanza kuondoa neno ufisadi na mafisadi kwenye kauli zao. Kauli yao mpya ni kubadili mfumo. Hata hivyo bado Chadema wana kibarua cha kuelezea wataubadili vipi mfumo kwa sababu mfumo sio chama cha siasa.

b) Kutoa fursa kwa wanasiasa wasio waaminifu kwa chama kukikimbia na kuacha wale walio tayari kukipigania chama. Rafiki wa kweli hujulikana kipindi cha changamoto.

c) Kupata fursa ya kuingiza wimbi kubwa la mamluki ndani ya upinzani kwa kisingizio cha kumfuata Lowassa. Hawa watapewa hero's welcome na kuaminiwa kirahisi.

Hasara
a) Siri zake za maandilizi ya uchaguzi zitafahamika kwa upinzani. CCM italazimika kufanya mabadiliko makubwa kwenye mikakati jambo ambalo litakigharimu chama.

b) Kupoteza baadhi ya watu ambao fundamentally wanaamini Lowassa ndio mtu pekee nchini mwenye uwezo na haki wa kuongoza. Ingawa kundi hili ni la watu wasielewa maana ya chama lakini lipo. Hawa wstamfuata Lowassa kokote anakoenda, wanasema "ulipo, tupo". Mrema alikuwa na watu wapatao 200,000 kwenye kundi kama hili. Lowassa anaclaim kuwa anao milioni moja. Hata hivyo inahitajika utafiti zaidi kuthibitisha idadi hii.

i) Chadema
Faida
a) Kupata mgombea tajiri ambaye ni high profile politician.

b) Kupewa siri za CCM.

c) Kupokea wafuasi wa Lowassa.

d) Kuongeza uhalali wake wa kuwa chama kikuu cha upinzani na kuweza kupata nguvu ya kusikilizwa Zanzibar. Lowassa ana wafuasi Zanzibar ambako Chadema hushindwa kuwa hata nafasi ya tatu kwenye uchaguzi.

Hasara
a) Kujenga sura ya kuthamini umaarufu na pesa kuliko misingi ya Chama.

b) Kukiri de facto kuwa hawakuwa na uwezo wa kuishinda CCM. Hapa watahojiwa je mtu mmoja ndio amewaletea uwezo? Je , kama mtu huyo ana nguvu kubwa kuliko Chama, mtamdhibiti vipi akiwageuka huko mbeleni?

c) Kuwakatisha tamaa wanaojitolea kwa ajili ya Chama. Kitendo cha Slaa kukatwa na kutokusikilizwa kitawafanya watu kama kamanda Mawazo wakae chini na kutafakari kazi wanayojitolea inalenga kubadili nini? Wengi wa wanaojitolea kwa nia njema huongozwa na misingi na itikadi ya Chama. Chama kinapotoka nje ya misingi , kinahatarisha kupoteza au kuwavunja nguvu watu hawa.

d) Kupunguza kuaminiwa na wananchi. Sura iliyojengeka ni kuwa Chadema inacheza tu mchezo wa siasa na hailengi hasa kuboresha maisha ya mtanzania. Mtu yeyote anayewapa pesa za uchaguzi watamtukuza ilimradi tu washinde. Kauli hizi za Mbowe hazijapokelewa vizuri na watanzania.

e) Kutumia nguvu kubwa kusambaza ujumbe mpya. Siku zote inafahamika ujumbe wa chadema ni kupinga mafisadi. Sasa kuna mabadiliko, tatizo sio mafisadi ila mfumo. Hii itahitaji resources nyingi kuwaeleza watu mpaka waikubali. Kwahiyo muda wa kuzungumzia masuala mengine ya maisha ya kila siku utakuwa mdogo kuliko wa kufafanua mabadiliko haya ya msimamo. Hii inaatarisha Chadema kuonekana Chama kinachotafuta madaraka bila kuwa na mkakati wa kuongoza nchi na kuboresha maisha.

f) Iwapo Chama hakitashinda uchaguzi kitakosa misingi ya kukiendeleza. Kitabaki kuonekana chama cha wajanjawajanja. Watu wa Lowassa ambao wameahidiwa vyeo serikalini itabidi watake vyeo kwenye Chama. Chama kitachukuliwa na watu wasiokijua wala kukijali kwa dhati.

Pamoja na kwamba watu hudhani siasa ni mchezo, lakini siasa ni taaluma. Katika haya yanayoendelea, mwenye taaluma zaidi ndiye atayejipatia faida zaidi kuliko hasara.

Sisi kama watanzania tunachotakiwa kuomba ni Mungu aendelee kuilinda nchi yetu iwe na amani na umoja kama taifa.
 
Kwa CHADEMA ya sasa kama Slaa anaweza kutosikilizwa basi Mwanakijiji ndo kabisa
so irrelevant.....watu hawamsikilizi Mwanakijiji tena

The Boss

Chadema ni Mbowe na Mbowe ni Chadema.. Hao wengine wapo kujaza nafasi kikatiba lkn hawana say yoyote.
 
Last edited by a moderator:
Miaka kadhaa iliyopita, niliwahi kuhoji wazi kuwa Siasa zetu zina mirengo gani au itikadi gani? Nakumbuka Mkandara alinijibu kuwa Tanzania hakuna itikadi au mirengo.

Tunachokiona ni mufilisi wa Kisiasa. Chama kukosa Itikadi inayoeleweka na kushabihiana na wananchi.

Leo hii, chama kinavutaka kati ya Neo Ultra Conservatives, Centrists na Liberals lakini hawana itikadi hata kidogo ya kusema Chadema ni chama cha siasa za namna gani.

Ukweli ni kuwa Chadema hakikuwa na hoja yeyote ile kujiuza zaidi ya Ufisadi.

Najiuliza kaam leo kwa mazingaombwe CCM wamediriki kumng'oa kwa makusudi kabisa hata kukiukwa demokrasia mtu ambaye angekuwa kibwagizo cha Chadema kwenye uchaguzi kutokana na hisia na taswira ya Ufisadi, leo hii Chadema wanakwenda Uchaguzi mkuu na agenda gani? Je ni agenda ya kiuchumi, kisiasa, kijamii au kimaadili?

Nzkumbuka nilipoandika Chadema must Reform, na matusi ya kuitwa msaliti kisa nilihoji People's Power!

Sasa Chadema wameamua kumfuata Malcolm X "by any means necessary" kama jinsi Kikwete siku ya Mkutano Mkuu aliposema Magufuli atawapeleka CCM Ikulu, Chadema imewekeza macho yote Ikulu!

Si Siri Lowassa anakuja na wasifu mkubwa sana wa kimfumo, kiuongozi na influence. Lakini, je Manifesto ya Lowassa alipotangaza nia akiwa CCM inaendana na Ilani ya Chadema au hata ya Ukawa?

Je katika ushirika huu wa Ukawa, leo hii Chadema wakiamua kunyoa badala ya kusuka na kufarakana kutokana na hamu na tamaa ya kwenda Ikulu iliyowafanya kuingia mkataba na wengine je haitaipa CCM ushindi mkubwa na hivyo kuua kabisa upinzani ukizingatia tayari CCM ina kundi la vijana walio tayari kuwa viongozi wa chama na Serikali 2020 na hata 2025?

Nitasema hivi kuhusu ninavyompima Lowassa pamoja na kuandika mengi kuhusu yeye miaka kadhaa na mpaka kukajengeka dhana kuwa mimi ni mfuasi wa Lowassa.

Lowassa ni Gladiator, anaingia ulingoni akijua ama atatoka hai au atatoka maiti na he has nothing to loose. Lowassa anatafuta uwanja wa kwenda kupigana hata kama itakuwa ndio mapigano yake ya mwisho. He has nothing to loose anymore.

Hivyo, ni lazima Chadema watafakari watakachokifanya na mapokeo hasi ikiwa watawageuka Ukawa na hata credibility yao kushuka zaidi.

Kitendo cha wao kuwa mstari wa mbele kumpokea Lowassa kimewaweka katika predicament mbaya, credibility imeshaingia maoda na walakini kwa kuwa miaka yote 10 iliyopita, walikuwa na hoja moja tuu kama kipaumbele cha kujinadi kwa Taifa na kilianzia MwembeYanga na orodha ya Mafisadi na hadithi za mafisadi.

Lakini hoja yao imejikita zaidi katika watu, mtu mmoja moja na si mfumo mzima ulioleta na kulelea ufisadi.

Ukiondoa fukuto la Zitto akiwa PAC kucharurana na mashirika na hata kuhakiki Serikali, sijaisikia Chadema ikileta hoja au muswaada bungeni wa kurudisha maadili au kuhakikisha matumizi mabaya ya fedha za Serikali kama ripoti ya CAG inavyosema miaka nenda rudi.

Hata kama kura za Chadema zingekuwa ni 10 tuu, na CCM wakipiga kura ya wingi ya hapana, lakini at least ingeonekana wazi kuwa suala la vita vya ufisadi si mikutano ya kutaja majina na tuhuma bali ni kuwepo na msukumo wa kujenga mfumo fanisi wa kisheria ndani ya Serikali hata kumpa DPP na AG uwezo wa kuwa huru kupeleka mafaili Ikulu kupata kibali cha kufungua mashitaka!

Option walionayo sasa Chadema na ni likely inabidi waimeze at this last minute ni ama kumtema Lowassa na kukiri kwa Watanzania kuwa alibugi stepu au kumkubali Lowassa na kuungana naye "kuiangusha" CCM si Ikulu pekee bali hata Bungeni (kumbuka chama chenye viti vingi inatoa Spika na Waziri Mkuu).

Hili liwe fundisho la mwisho kwa vyama vinavyojiendea tuu bila kuwa na itikadi inayoeleweka.

Leo Ilani ya Ukawa ni kubwa kuliko ya Chadema kutokana na makubaliano ya Ukawa. Je Chadema na hasa lile kundi la Neo/Ultra Conservative wa Chadema (rafiki na kaka yangu Mwanakijiji akiwa kundi hili) liko tayari kuheshimu uamuzi wa umoja wa Ukawa?

Chadema haina uwezo kuiangusha CCM pekee yake bila kuungana na wenziwe. Kitendo cha kufarakana na Zitto na hata kutoa mwanya kwa Zitto kuanzisha chama na kukinadi kwa itikadi kwanza, kinaashiria mpasuko wa kifikra ndani ya Chadema kutokana na kukosa Itikadi na Sera inayoeleweka na kuaminika.

Nasikitika kuwa inabidi niungane na Mwalimu Augustine na Susuziri kusema jitihada zote za kujenga Chadema kifikra na kiitikadi zimeishia hapa.

Sasa ni lazima wasuke twende kilioni, waungane na Lowassa kama wamoja, wameze nyembe na ego binafsi na kufanya kazi pamoja kuwadhihirishia Watanzani akuwa lengo la kuing'oa CCM ni la dhati na ikiwa watashinda uchaguzi (Ukawa), lazima watuonyeshe kuwa wao si sawa na CCM kwa vitendo na si hotuba za majukwaani.

Ni aibu kubwa sana kusikia tetesi kuwa kuna mfarakano na kukosekana kwa msemaji mkuu kujibu hoja au kutoa ufafanuzi wa kinachojiri.

Lowassa anarudisha fomu wikiendi hii. Je wale conservatives wakisusa, wakazira na kujitoa, atakayeumia ni nani?

Uchaguzi huu ulikuwa na slogan mbili: Its economy stupid and we want Change and not more of Same... lakini uhalisia Chadema na Ukawa wamebidi kumchukua Lowassa na hivyo wanagota kati ya Change na More of the Same... CCM wanaponea hasira za mkizi na hata yale maswali magumu kwao kuhusu uchumi wa Taifa yatasahaulika kutokana na Chadema kukwama mchangani kutokana na tofauti hizi za kimtazamo na itikadi isiyokuwepo.

Ni wazo la Mchungaji jioni hii!
  • Ndugu zangu, tutambue kuwa itikadi ni zao la kutambua nani ni adui wako na kivipi utapambana naye. Shida ya viongozi wetu wengi wa dunia ya tatu (hususani wa Afrika) hawatambui nini ni adui wa jamii zao katika muktadha wa siasa na maendeleo..! Kwa mtazamo wangu hili linatokana na uvivu (wa kujifunza na kusoma) kwa viongozi waliowengi (ambalo ni tatizo la mfumo pia)....Maskini ya Mungu, hawajui kuwa itikadi ndiyo injini ya taasisi yoyote ile ama iwe katika kupambana/kuboresha mfumo uliopo ili kuleta maendeleo linganifu katika jamii...Hawafahamu kuwa hawatakiwi kupambana na kile kinachodhiri (manifestation kwa mfano: ukosefu wa ajira), bali wanatakiwa kupambana na mfumo (Processes/essence yaani mizizi/sababu zinazopelekea ukosefu wa ajira)... Hili linadhihiri katika Tanzania yetu ya leo, kwa mfano: wakati CCM wakilaumu makada wao wachache hususani mapacha wa3 (Chenge, Rostam na Lowassa) kuwa ndiyo wanaoharibu chama, wapinzani wao wanatuletea orodha "list of shame" zenye kutaja majina ya watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi na ubadhirifu, na jamii ikendelea kuhadaiwa na vyama vya siasa kuwa X, Y, na Z ndiwo mafisadi na kutufanya jamii nzima kusahau kuwa tatizo si watu pekee bali ni mfumo mzima na watu wake..Ki ukweli si kosa lao kwani viongozi wetu ni zao la jamii hii hii yetu inayopuuza maarifa na kubariki mfumo mbaya wa kujifunza (elimu na malezi)...Hivyo basi uwepo wa siasa mufilisi tusishangae huenda sote (jamii na viongozi wetu) tumekariri ile maana finyu (narrow definition) ya chama cha siasa (a political party) waliyotupa waleta demokrasia isemayo "A political party is a group of people with common intersests who aim at ruling/controlling the state" (yaani chama cha siasa ni kikundi cha watu wenye maslahi yanayofanana wenye leongo la kuongoza dora)…Hapana natania tu! Hatujakariri tumefundishwa:smile-big:

  • Hivyo basi siasa yetu mufilisi ni zao la jamii yetu mufilisi; hivyo basi kwakuwa viongozi ni zao la jamii mufilisi basi na wao pia ni mufilisi...
​
Kwa maoni yangu kinachoendelea sasa katika siasa zetu ni mabadiliko yasiyomithirika, na ndiyo njia itakayotupeleka katika siasa za kweli. Tukitumia nadharia kuu mbili za maendeleo, yaani ile ya misigano na misuguano (Conflict perspective) na ile ya mageuzi (evolution perspective) ni dhahiri ya kwamba minyukano inayotokea katika vyama vyetu na ogani za serikali hususani bunge zitaleta athari chanya kwa taasisi husika kwani kuna mambo mawili yaweza tokea ama taasisi hizo zijiboreshe au ziendelee kufanya uozo kulingana na muktadha. Hilo litafuatiwa na maamuzi ya wananchi ambau watakarishishwaa na maboresho ya taasisi hizo na kuyakubali au kuchukizwa na uozo wa taasisi hizo na kuamua kuzibadili, hatimaye kuleta mageuzi....

#MunguIbarikiTanzania

cc: Rev. Kishoka
 
Huyo Mzee Mwana kijiji, tupa kuleeeeeeeeeeee.... lofa tu, hajui siasa, kazi yake chuki binafsi ndio inamuongoza kwa mtu husika,,hasa kwa Lowassa, Mzee Mwanakijiji ana chuki binafsi na Lowassa..

Huyu Mwanakijiji hafai kabisa CDM... yeye
kumpamba tu Dr. Slaa, cjui shemeji yake...?? Very unethical indeed...hana akili kabisa

Tuna safari ndefu sana ikiwa hata huyo lowasa akijua ana mtu kama wewe.

Alichokifanya MM ni mawazo yakevna wazima wastaarabu wayaheshimu hapa cha msingi ni kushindanisha hoja.
 
Nashangaa watu wanasema ati Adui yao ni CCM, what the hell is that? Adui wa Watanzania ni tabia ya viongozi wezi kama EL et al. Adui hawezi kuwa jina, adui ni matendo. EL amepata fedha zake kwa kuiliibia taifa kwa mwendo wa kupokea rushwa na kufilisi mashirika ya umma leo hii kuna wanaodiriki kusema huyu ndiye mwadilifu kwa watanzania. Are you serious?
 
We what CCM out!!! Hayo mengine tutayafanya wenyewe...

Whoever is willing is welcome to join in.. This Change is for all

Comrade
 
Tafakari kwanza what is behind Lowassa kuingia Chadema ndo uje kumshauri Mzee Mwanakijiji.

Sasa ndo naelewa kwa nini wanasema half knowledge is dangerous than total ignorance? Yani kama hii ndo thinking yenu sishangai wale walioaminishwa Gaddafi ndo mbaya na atoke na leo wanashangaa Gaddafi katoka ila yaliyowakuta ni zaidi ya hata yale waliyokuwa wanayawaza.

I feel sorry for you.
Lord denning you have nailed it! Ni ujinga eti adui yetu ni CCM! Yaani kuna watu wajinga. Badala ya kuelezea sera wangelea chama!
 
Last edited by a moderator:
Asante Mzee Mwanakijiji kwa kuanda majibu ya hoja za wadau, labda niseme kabisa kuwa napenda sana CCM itoke madarakani kwa njia yoyote ile,
Mzee Mwanakijiji, katika majibu yako ningependa pia urudi nyuma kidogo na uuangalie huo umoja wa Katiba ya wananchi (Ukawa), nikiwa na maana kuwa CUF kama mshiriki wa Ukawa lakini pia yupo ndani ya Serikali inayopingwa na Ukawa (Serikali ya Umoja wa Kitaifa), sasa Chadema walikubali vipi kuwa pamoja na CUF ambao wako serikalini pamoja na CCM, kwa minajili ya kuwa la CUF ndio la CCM, na la CCM ndio la CUF, SIJAWAHI KUKUSIKIA/KUKUSOMA UKIPINGA MUUNGANO HUO WA CHADEMA NA CUF ndani ya Ukawa,
Nadhani kupinga kwako kwa Lowassa kuja Ukawa/Chadema kungeanzia na kupinga kwa CUF kuwa Ukawa,

pili, ningependa pia ujaribu kuelezea kwa kifupi tu, malengo hasa ya Vyama vya upinzani ni nini kwa hapa Tanzania?, ni kuikaripia na kuikosoa CCM au kuna mkakati wa kuitoa CCM kwenye Madaraka?, na kama malengo hasa ni kuitoa CCM madarakani ni njia gani hasa sahihi ya kufata?,

tatu, unaweza kuziainisha limitations zozote za vyama vya upinzani kuchukua watu kutoka CCM?, kwamba huyu achukuliwe na huyu aachwe?

This Mwanakijiji is useless!
Kwa kuongezea kwenye hoja ya character X hapo juu, a real leader has three grand characters:
1. Power to influence
2. Ability to envision
3. Ability to tap on to insights.
Kama mwanakijiji ni leader basi anakosa sifa namba 2 na 3.
To envision means to see by inner mental/spiritual eyes.
To tap on to insights for a leader means to listen much, read much, learn much etc for wisdom.
It is absolutely dangerous to being void of inner (mental/spiritual) vision.
mental blindness is as bad than physical blindness.
When you lose/lack mental vision you're termed as a fool.
The highest objective ya opposition part yoyote is to grab on to power.
Objective ya timu yoyote uwanjani ni kupachika bao.
How fool am I nimepata nafasi ya kuweka mpira golini nisifanye hivyo?
Only a fool ndo badala ya kufunga ataokoa.
Halafu huwa anajibainisha kama mwanachadema...ni gamba tu huyu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom