Mzee Musobi Mageni hatunaye tena

Mzee Musobi Mageni hatunaye tena

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2010
Posts
8,397
Reaction score
7,979
Muasisi wa Siasa za mageuzi na mmoja wa waanzilishi wa chama cha CUF mzee Musobi Mageni amefariki dunia jana saa mbili usiku nyumbani kwake Ngudu, Kwimba. Mzee alikuwa anasumbuliwa na magonjwa ya uzeeni ya presha na kisukari.

RIP Musobi Mageni, kujitoa kwenu muhanga kudai vyama vingi ndio matunda ya demokrasia iliyopa sasa ambapo bado miaka mitatu tu CCM ing'oke.
 
Tutakukumbuka kwa mema yote, taifa lilikuhitaji lakini mungu amekupenda zaidi, RIP Musobi Mageni na pole sana Mageni Msobi.
 
juzi juzi wakati mgogoro na maalim seif na mpiganaji Hamad Rashid ulipokuwa umeshika kasi tulimuona maalim seif akisafiri toka unguja mpaka mwanza kwenda kuomba msaada kwa mzee huyu,inaonesha alikua ni mtu muhimu ndani ya cuf licha ya kwamba tumekua tukiaminishwa kwamba cuf ni chama cha wapemba na waislam!

RIP MUASISI WA MAGEUZI NCHINI
 
Kazi ya mungu haina makosa poleni sana wafiwa.
 
R.I.P Mzee Musobi Mageni pole sana rafiki yangu msobi wa Chang'ombe Bora.
 
R. I. P Mzee! Matunda ya kazi yako tutayafaidi sisi na wajukuu wako!
Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu, apumzike kwa amani. Aamen!
 
Pumzika kwa amani mzee Musobi Mageni, kazi ya Mungu haina makosa.
 
Muasisi wa Siasa za mageuzi na mmoja wa waanzilishi wa chama cha CUF mzee Musobi Mageni amefariki dunia jana saa mbili usiku nyumbani kwake Ngudu, Kwimba. Mzee alikuwa anasumbuliwa na magonjwa ya uzeeni ya presha na kisukari.

RIP Musobi Mageni, kujitoa kwenu muhanga kudai vyama vingi ndio matunda ya demokrasia iliyopa sasa ambapo bado miaka mitatu tu CCM ing'oke.

RIP Mzee Musobi...unaiacha Tanzania wakati inanuka kisisasa. Peleka salamu kwa mwalimu na mwambie kwamba hatuna hata miaka mitano kwa taifa alilolipigania kugeuka taifa la mauaji ya kisiasa.
 
R.i.p mzee musobi mageni mungu akulaze mahala pema peponi amin umefanya makubwa
 
RIP Mzee Mageni.
Hivi huyu mzee si ndiye baba yake na Mh. Leticia Nyerere (Viti Maalum Chadema)? Kama nimekosea, nisamehewe. Nauliza tu maana Mh. Leticia pia anazaliwa Kwimba na surname yake niliwahi kusikia ni Mageni?!
 
Poleni watanzania wenzangu kwa msiba huu,BWANA ALITOA NAYE AMETWAA!
"Ulikuwa taa tuliyojivunia sana".Pole pia sweetlady
 
Back
Top Bottom