Mzee Mohamed Said na Mapinduzi ya Zanzibar

Jidanganye,palikua na link Kati ya zenji-tabora-kigoma-congo kitambo,pembe za ndovu etc

Mimi nasema; kama kulikuwa na link, zenji---Tabora---Kigoma---Congo kwa ajili ya biashara ya pembe za ndovu, na mimi nakubali hiyo link na ndio link hiyo iliyowatoa Wamanyema kutoka huko Congo au Kigoma kuingia Tabora---Dar---Zenji, sasa naomba link ya Malawi---Zenji.
 
Ina...
Mbona historia ya Zanzibar na muungano imeandikwa na waandishi wengi na bado wapo?
Kitabu kipya ni hicho hapo chini cha Khamis Abdulla Ameir (2022).

Kitabu hiki kina kurasa 500+ na ameyachabua mapinduzi na muungano kwa undani kupita mwandishi yeyote yule.

View attachment 2180958
Kinapatikana wapi hiki kitabu? Bookshop gani?
 
Wewe umechelewa kujua. Karume kazaliw Malawi mkuu

Siwezi kukataa kama nimechelewa lakini pia siwezi kukubali kirahisi bila kupata angalau ushahidi mdogo wa kihistoria kuthibitisha kwamba Karume alitokea Malawi, ilikuaje atoke malawi kuja kuanzisha makao zanzibar??, je alikuja kufanya biashara na biashara gani au kutafuta ajira nk.

Ni historia ndio mfafanuzi wa jambo hilo.
 
Sio kweli, Karume ni jina lenye asili ya Wamanyema, Majina hayo yanapatikana sana Kigoma miongoni mwa Wamanyema, Kigoma ndio lango la wamanyema kuingia Tanganyika kutoka Masharikk ya DRC, kutoka Kigoma wakaingia Tabora hadi Dar na Zanzibar.
Ndiyo kwanza nikusikie wewe kama Karume alikuwa Mmanyema, sisi tumesoma alikuwa Mnyasa na hata watu waliokuwa wanamjua kwao Mwera alipofikia hawajawahi kusema alikuwa Mmanyema. Hata akina Amani Karume walipelekwa kwao Malawi kwa muda fulani na sio Kigoma.

Zanzibar wapo Wamanyema wengi sana wala isingekuwa issue kusema Karume alikuwa ni Mmanyema.
 
Je waweza thibitisha hilo??---- Malawi na Zanzibar enzi hizo kijiografia na kidemografia mbona ilikuwa kinyume sana!!!😱
Umewahi kusikia kwamba Karume aliwahi kupelekwa mahakamani kwa vile yeye kiasilia hakuwa raia wa Zanzibar alikuwa raia wa Malawi? Ukumbuke Malawi, Tanganyika na Zanzibar zote zilikuwa chini ya mtawala mmoja Muingereza.

Karume alishinda kesi ile.
 
Siwezi kukataa kama nimechelewa lakini pia siwezi kukubali kirahisi bila kupata angalau ushahidi mdogo wa kihistoria kuthibitisha kwamba Karume alitokea Malawi, ilikuaje atoke malawi kuja kuanzisha makao zanzibar??, je alikuja kufanya biashara na biashara gani au kutafuta ajira nk.

Ni historia ndio mfafanuzi wa jambo hilo.
Karume alikuja Zanzibar akiwa mgongoni kwa mama yake, yaani bado ni mchanga kabisa. Maisha yake yote ameishi Zanzibar. Hapo zamani mke wake akielezea hiyo hadithi kwenye TVZ.
 
Karume alikuja Zanzibar akiwa mgongoni kwa mama yake, yaani bado ni mchanga kabisa. Maisha yake yote ameishi Zanzibar. Hapo zamani mke wake akielezea hiyo hadithi kwenye TVZ.

Asante kwa historia hiyo.
Kuna mtu mmoja humu kasema karume alilelewa na mmanyema huko Zenji na ndio sababu ya yeye kupata jina hilo, je kuna ukweli hapo??!
 
Mimi nasema; kama kulikuwa na link, zenji---Tabora---Kigoma---Congo kwa ajili ya biashara ya pembe za ndovu, na mimi nakubali hiyo link na ndio link hiyo iliyowatoa Wamanyema kutoka huko Congo au Kigoma kuingia Tabora---Dar---Zenji, sasa naomba link ya Malawi---Zenji.
Kwamba watu hawakuwa wakitembea!!?..na Congo na Malawi ni mbaali saana,wakati Mambo yalipokuwa hayaeleweki zenji,amani karume na mdogo wake walipelekwa nyasa/Malawi..kwa mujibu wa amani mwenyewe,na darasani anasema Kuna mwalimu alikua alimwambia baba yenu atauawa,kwa nini wapelekwe Malawi na si Kenya au bara!?...
 
Wangepelekwa Kenya si nyie mngesema wao ni Wakenya!!!
 
Ndiyo kwanza nikusikie wewe kama Karume alikuwa Mmanyema, sisi tumesoma alikuwa Mnyasa na hata watu waliokuwa wanamjua kwao Mwera alipofikia hawajawahi kusema alikuwa Mmanyema. Hata akina Amani Karume walipelekwa kwao Malawi kwa muda fulani na sio Kigoma.

Zanzibar wapo Wamanyema wengi sana wala isingekuwa issue kusema Karume alikuwa ni Mmanyema.

Mimi sijasema kwamba kwao ni kigoma, ninachosema ni kwamba; jina Karume yanapatikana zaidi miongoni mwa Wamanyema na ndio maana inference yangu ya kwanza ikawa yeye anayo damu ya kimanyema hata kama hakuzaliwa Kigoma pia ikizingatiwa historia ya uwepo wa wamanyema huko Zenji nk.
 
Dah,tnachoshana tu jamaa yangu

Haya hebu niambie jina la Abeid kapewa na nani??, jina Amani ni la nani?? Sasa jina Karume lilipatikanaje??--- hapo inahitajika udadavuzi wa kihistoria.

Asilimia kubwa (karibu 99%) ya Wamanyema wanayo majina ya kiisilamu na ni waisilamu kwa asili.
 
Mohamed Said ni mwanaharakati na mwandishi wa habari. Habari zake nyingi ni wazee waislamu wa kariakoo baada ya Uhuru
hao wazee ndio waliodai Uhuru wa Tanganyika akina Sykes.

Mganda Mkristo John Okello huwezi kukuta ametajwa kwenye waasisi wa mapinduzi.

Mzee Mohamed Said mbona huandiki mambo haya? Kila siku wewe ni Nyerere na wazee wa kariakoo tu?
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Kwamba watu hawakuwa wakitembea!!?..na Congo na Malawi ni mbaali saana,wakati Mambo yalipokuwa hayaeleweki zenji,amani karume na mdogo wake walipelekwa nyasa/Malawi..kwa mujibu wa amani mwenyewe,na darasani anasema Kuna mwalimu alikua alimwambia baba yenu atauawa,kwa nini wapelekwe Malawi na si Kenya au bara!?...
Na prefect aliyekabidhiwa watoto wa Karume shuleni anaitwq Banda. Ni mzee sasa na anaishi Stockholm.
 
Back
Top Bottom