Mzee Mkapa (RIP) aliomba Tume Huru anazawadiwa Kiwanja cha Mpira

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,996
13,978
Nimefuatilia leo kwenye sherehe za kumuaga Rais Mtaafu BW Mkapa. Kilichotokea ni kuwa Rais ameamua kuwa Uwanja wa Mpira Uitwe Uwanja wa Mkapa kama watu wengi walivyopendekeza.

Pia, alisema kuwa Mzee Mkapa hakupenda jina lake liwe kwenye kumbukumbu kama hizo lakini kwa vile hayupo basi ameamua kufanya hivyo.

Wazo langu ni kuwa Mzee Mkapa alitamani Tanzania iwe na tume huru ya Uchaguzi. Na hili ameliongelea hadharani. Sasa kwa nini anaenziwa kwa kupewa vitu ambavyo hakuvitamani wala kuvitaka badala yake kupewa vitu alivyotamani Tanzania tuwe navyo.

Nafikiri Mzee Mkapa angefurahi huko aliko kama angesikia kuwa tunaunda tume huru ya Uchaguzi ya B.W Mkapa (Independent Electoral Commission of B.W Mkapa).
 
Jambo kubwa lamsingi kwa Taifa Imara na Tulivu ni Tume Huru ya uchaguzi

Mkapa aliomba kwa utashi wake yeye mwenyewe Tume Huru ya Uchaguzi

Cha ajabu badala ya kutekelezewa ombi lake, wametekeleza maombi yao binafsi.

Mungu nimwema na Hadhihakiwi...... time will tell.
 
ni jukumu LA mashabiki kubadili slogan ya kushangilia

iwe "tume huru* hasa yanga anaposhinda,

na kila goli mashabiki wanahanikiza kwa shangwe kama zote " tume huruuuu'
 
Kwani aliomba uwanja?
.
IMG_20200725_062956.jpg
 
ni jukumu LA mashabiki kubadili slogan ya kushangilia

iwe "tume huru* hasa yanga anaposhinda,

na kila goli mashabiki wanahanikiza kwa shangwe kama zote " tume huruuuu'

Kabisa, hili nililipendekeza lianze toka mwezi March, nikashauri kuwa kila kiongozi wa upinzani akipata jukwaa lolote la kuongea, lazima aongelee tume huru ya uchaguzi mpaka iwe kero. Napendekeza wakati wa kampeni hizi, kuwe na mabango yasemayo " tunashiriki uchaguzi, lakini hatuna imani na tume ya uchaguzi" Hii itasaidia hata matokeo yatakayotoka yasiaminiwe, na hiyo itapelekea kupata tume huru ya uchaguzi.
 
Hakumaanisha angemaanisha Wala isingeshindikana.wanasiasa ni wanafiki
 
Tatizo misisiemu inaamini kuwa bila sisiemu haitaenda wakati miaka yote hiyo nchi wameikwamisha.
 
Mnataka tumpoteze na mwingine Tena? Cardiac Arrest so mchezo, mtu mwenyewe ana implants, ataanguka muda wowote mkiendeleza nyimbo zenu za TUME HURU, YA HAKI NA WAZI YA UCHAGUZI
 
japo nilikua mdogo ila nampongeza mkapa kwa kuimarisha kwa kiasi fulani uchumi wa nchi hii
mf.kwenye utawala wake nadhani ndo kipindi ambacho soko la hisa lilikua na uelekeo chanya ila kwenye suala la katiba hapa napingana aye
mbona hakufanya hayo alipokua rais mbona wakati anawaita watu malofa hakuzungumza suala la katiba mpya
 
Amegundua kuwa amefanya kosa. Na mambo ambayo mtu anayasema muda mfupi kabla ya kufa kwake huwa unakuwa ni Wosia.
 
Anajua alichofanyiwa Mrema kwenye urais na ubunge wa Temeke, urais tulipiga kura kwa awamu wiki nzima, ubunge kigugumizi siku mbili, akatangazwa usiku wa manane! Mwisho wa siku Temeke tukasingiziwa kunavurugu madukani yamechomwa moto, alipobanwa akasema hatukumuelewa!
 
Ila Kipindi kile Mwinyi ndiye alikuwa Rais ......... Akafuta uchaguzi wote Dar ....... Maana Dar youte ilikuwa imekwenda Upinzani na Mrema.

Inawezekana kabisa alikuwa amechoshwa na wizi wa kura wa CCM na serikali yake ndiyo maana akaja na hii hoja ya Tume Huru kabla ya kifo chake.
 
Hakuna Lolote huyu BM alikwenda ZNZ kuamrishwa atangazwe DK badala ya Maalim,ilhali Maalim alishinda na DK alishakubali matokeo kiungwana kabisa kwa hofu ya Mungu.
Kama hakupata nafasi ya kutubu kazi anayo.
 
Hiyo tume huru kwanini Mkapa hakuileta yeye mwenyewe ndani ya miaka yote10? Shetani akizeeka sana hutamani awe Malaika...
 
Back
Top Bottom