Benjamin William Mkapa Rais aliyeamini katika Ujenzi wa mifumo

Benjamin William Mkapa Rais aliyeamini katika Ujenzi wa mifumo

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
16,951
Reaction score
62,837
Ndugu Watanzania wenzangu
Kwa hakika Taifa letu limepoteza kichwa, kichwa makini sana kilichoacha alama katika nyumba hii ya maendeleo tunayoendelea kuijenga.

Rais Benjamin William Mkapa amefanya mambo mazito sana kwa nchi hii. Kwa kweli nchi hii ina afadhali leo hii kwa sababu alikuwepo mtu aitwaye Benjamin William Mkapa aliyejitahidi sana kusimika mifumo, mifumo ambayo leo hii ni mawe makuu katika msingi wa maendeleo ya nchi yetu. Baadhi ya mambo makubwa ambayo rais Mkapa aliifanyia nchi hii ni kama haya yafuatayo.

1. Kuvuta Maji kutoka Ziwa Victoria kuelekea Kahama.

Kila mtu anafahamu kusitasita kulikokuwa kunakwamisha matumizi ya maji ya Ziwa victoria kutokana na mkataba wa Kinyonyaji wa kikoloni unaoipa Misri Share kubwa ya maji hayo. Benjamin Mkapa akiwa rais, alitoa go ahead ujenzi wa mradi wa kuyatumia maji hayo bila kuiogopa Misri. Kwa hakika nafuu iliyotokana na maji hayo ni kubwa sana

2. Kuboresha Jiji la Dar (Tume ya Keenja).

Mkapa alipoingia madarakani, Jiji la Dar lilikuwa na hali mbaya sana, lilikuwa limechakaa, lilikuwa chafu kwelikweli. Rais Mkapa akaunda tume ya Keenja iliyofanya kazi kubwa yenye kukumbukwa, ikasafisha jiji, na kukarabati majengo mbalimbali ya serikali yaliyokuwa katika jiji hilo, Jiji angalau likaanza kuwa na muonekano mpya. Kabla ya hapo ilikuwa ni kawaida kwenda kwenye mitaa ya posta na kukuta vinyesi pembezoni mwa majengo mbalimbali. Tume ya Keenja ilijitahidi kurekebisha hiyo hali

3. Kuzipa hadhi ofisi za serikali.

Wakati Mkapa anaingia madarakani, ofisi za serikali zilikuwa choka mbaya sana, yaani zilikuwa kuwa kama mabanda fulani hivi yaliyochoka, samani zilikuwa zimechoka, zimepauka, samani mbayambaya. Lakini Mkapa alizipa hadhi ofisi za umma na heshima ya utumishi wa umma ikaanza kurejea taratibu. Kabla ya hapo watu kazi kwenye utumishi wa umma ilikuwa ikibezwa haswa na vijana walioonja utamu wa hela baada ya nchi kufungulia soko huria kipindi cha mzee Mwinyi

4. Mzee Mkapa aliweka mipango ya kugusa maisha ya watu.

Aluanzisha Mpango Maalum wa Elimu ya Msingi MMEM, Akaanzisha mipango ya Kurasimisha Biashara uitwao MKURABITA, alianzisha programmes kama vile TASAF, MEMKWA, Mipango hii ilikuwa na mchango mkubwa kwenye kuboresha maisha ya wananchi.
Pia ni kipindi cha Mkapa huduma za Afya ziliboreka sana, kwa hospitali nyingi za wilaya kuanza kuwa na vifaa muhimu kama vile X-Rays, na madawa pia kupatikana.

Pia mzee Mkapa alitumia uwezo wake mkubwa wa kidiplomasia kuiwezesha nchi yetu kufutiwa madeni makubwa sana yaliyokuwa yakituelemea

Lakini pia Rais Mkapa alidhibiti mfumuko wa Bei, Bidhaa zilikuwa zinauzwa kwa bei affordable sana. Mfano mzuri ni nauli ya daladala kipindi cha BWM ilikaa shilingi 150 kwa muda mrefu sana bila kubadirika

5. Mzee Mkapa alikuwa champion wa Mageuzi.

Alianzisha reforms nyingi kama vile namna bora ya kuongeza mapato ya serikali kupitia ukusanyaji wa VAT, Pia alianzisha reforms kwenye mifuko ya pensheni kwa kuanzisha NSSF ambayo baadae ilitoa mchango mkubwa sana kwenye kuchochea maendeleo ya nchi yetu na kuwatumikia vyema wastaafu, Pia aliboresha utendaji kazi wa serikali za Mitaa kwa kuanzisha TAMISEMI

6. Mzee Mkapa alianzisha mifumo mingi ya Kitaasisi tunayonufaika nayo hadi hii leo

Baadhi ya mifano ni vitu kama vile
1. Tume ya vyuo vikuu TCU
2. PSRP
3. Wakala wa Barabara TANROADS, Sote tunajua kazi kubwa ya Ujenzi wa barabara iliyofanywa na TANROADS
4. Uwanja wa mpira wa Taifa
5. Yeye ndiye alianzisha mfumo wa Bima ya Afya NHIF, bima inayonufaisha watu wengi sana
6. Alianzisha Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu LOANSBOARD, kupitia Taasisi hii pamoja na changamoto zake, watu wamekopeshwa mikopo ya elimu ya juu lakini pia wameweza kufatiliwa vizuri walipe deni.
7. Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii tuliweza kuwa na TV ya Taifa
8. Alijenga Daraja la Mkapa, daraja lililosaidia kupunguza adha kubwa sana ya usafiri kwa watu wa mikoa ya kusini.
9. Yeye ndiye aliyeanzisha Tume ya Taifa ya kupambana na UKIMWI ya TACAIDS
10. REPOA

7. Mkapa aliilea sanaa kwa matendo

Ni katika kipindi cha Utawala wake aliwapa uhuru wasanii kufanya sanaa, na ninaweza kusema Golden age ya muziki wa kizazi kipya ilikuwa mwaka 2000 hadi 2005 katika utawala wa BWM. Hiki ndo kipindi Taifa lilishuhudia vipaji vya Bongo flavor. Wakati ule BASATA ilikuwepo lakini haikuwa na Fungiafungia, zimazima mawazo huru ya kisanii, na ndiyo maana vibao vingi classic vya Bongo Flavor vya watu kama Professor J, Sugu, Juma Nature na wengine vilikuwa ni kipindi cha Mkapa kwa sababu alivumilia Mawazo huru katika ubunifu.

8. Kwenye Misiba mikubwa ya Kitaifa aliliongoza Taifa na kuwapa wahanga heshima inayostahiki

Wengi wetu tunakumbuka ajali ya meli ya MV Bukoba, na jinsi Benjamin Mkapa alivyowapa heshima stahiki marehemu, Tunakumbuka Msiba wa ajali ya Treni jinsi Rais alivyoonysha kuguswa kwelikweli na kuwapa heshima ya Kitaifa kwa dhati kabisa. Sote tunakumbuka jinsi alivyohandle msiba mzito sana wa baba yetu wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

9. Mzee Mkapa alikuwa fair, alijaribu kuupiga vita Udini kwa vitendo

Waislamu walivyomlalamikia kuhusu kuwa Nyuma kwenye elimu, kwamba hawajanufaika vya kutosha kwa matunda ya uhuru kwenye elimu, Aliamua kuwapa Majengo ya TANESCO ili wajenge chuo chao kikuu, Lakini pia akayarudishia Makanisa baadhi ya shule zao zilizochukuliwa na Mwalimu Nyerere mfano shule ya Wakatoliki ya Forodhani.

Pia ilipoundwa Bodi ya Parole iliyojaa Wakiristo watupu, Waislamu walivyoonyesha kutofurahishwa na hatua hiyo, aliivunja hiyo bodi na kuunda nyingine yenye uwakilishi mpana wa makundi ya kijamii.

10. Alipunguza umasikini wa wananchi kwa kiwango kikubwa sana.

Wakati rais Mkapa anaingia madarakani, pato la mtanzania mmoja mmoja kwa mwaka (GNI per Capita) ilikuwa ni takriban dola 170, lakini kwa kipindi cha miaka 10 ya uongozi wake alifanikiwa kukikuza mara tatu na kufikia Dola 500 kwa mwaka. Hali hii ilileta unafuu kiasi kikubwa sana sana. Leo hii tunashangilia kuingia katika uchumi wa kati, lakini hutuangalii tumetoka wapi kama nchi, Wahenga walisema, Usione vyaelea viliundwa!

Hitimisho:

Hayo ni baadhi ya mambo makubwa ambayo Mkapa aliifanyia nchi hii, yapo mengi sana lakini hayo ni machache.

Binafsi naweza kusema kuwa, Taifa letu lina bahati sana kuwahi kuongoxwa na mheshimiwa Benjamin William Mkapa.

Rais Mkapa alikuwa ni tough kwa muonekano wa nje lakini alikuwa ni mtu mwema sana

Kiukweli Tutaendelea kumuenzi mwana huyu wa Afrika, aliyeifanyia nchi yetu makubwa kwenye ujenzi wa mifumo

Pumzika kwa Amani mzee wetu Benjamin William Mkapa
 
Sisi waislamu kila tukipita Mkoa wa Morogoro na kuyatizama Majengo ya kilichokua chuo cha Tanensco machozi hayataacha kutoka wala Jina lake halitafutika kwa vizazi na vizazi.

Binafsi Nina vijana watatu wamehitimu katika chuo kile. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.

Aamin
 
Mkapa alikuwa msikivu!

Kwenye suala la kuwapa Waislamu Majengo ili waweke chuo chao kikuu hapo, Umma wa Kiislamu nchini kamwe hautomsahau Benjamin William Mkapa. kwenye hilo alionyesha uongozi kwa vitendo!
 
Asante sana kwa kutujuza.
Ila Pemba hatutamsahau

Alikuwa nje ya nchi, Muulizeni Mzanzibari mwenzenu Dr Omar au waziri mkuu wa wakati huo Sumaye, hao ndo walikuwa nyumbani na ndo walikuwa Incharge

Hata hivyo anawajibika kwa kuwa yeye ndo alikuwa Rais wakati huo
 
1595707296447.png
 
Attachments

  • 1595707259677.png
    1595707259677.png
    15.3 KB · Views: 24
Mkuu Missile, kwa kweli umeweza kuainisha ukweli mwingi juu ya gwiji huyu ambaye ametutoka hv karibuni kwa mapenzi yake Mola. Pengine kwa kyongezea nyama kidogo ktk hoja zako zilizopo mezani, huyu alikuwa ni mwana diplomasia makini ambaye alijari kivitendo masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa pasipo kuterereka.
 
Naam, swadakta kabisa ndugu Mbenge

Alipokuwa waziri wa mambo ya nje mwaka 1978/1979 alifanya kazi nzuri mno ya kidiplomasia ya kuishawishi Dunia na Afrika juu ya misimamo yetu kuhusu vita ile, lakini pia alicordinate vizuri na wizara ya Ulinzi kuipatia nchi yetu mahitaji muhimu ya mapambano.

Ukiachilia mbali hilo, alikuwa ni mwanadiplomasia nguli aliyearticulate vizuri sana huko duniani positions za Tanzania kuhusu harakati za ukombozi wa Afrika.
 
Kuna mtu mifumo anaona inamrudisha nyuma.. anatamani hata afute TRA, police ili mwenyewe afanye kazi hiyo.

[emoji1][emoji1][emoji1][emoji111]
 
Naam, swadakta kabisa ndugu Mbenge

Alipokuwa waziri wa mambo ya nje mwaka 1978/1979 alifanya kazi nzuri mno ya kidiplomasia ya kuishawishi Dunia na Afrika juu ya misimamo yetu kuhusu vita ile, lakini pia alicordinate vizuri na wizara ya Ulinzi kuipatia nchi yetu mahitaji muhimu ya mapambano.

Ukiachilia mbali hilo, alikuwa ni mwanadiplomasia nguli aliyearticulate vizuri sana huko duniani positions za Tanzania kuhusu harakati za ukombozi wa Afrika.
1595708884744.png
 
Alipikwa akapikila na nyerere..

Kizazi cha nyerere ndio kizazi pekee nyenye maadili ya ukweli.
Naam, swadakta kabisa ndugu Mbenge

Alipokuwa waziri wa mambo ya nje mwaka 1978/1979 alifanya kazi nzuri mno ya kidiplomasia ya kuishawishi Dunia na Afrika juu ya misimamo yetu kuhusu vita ile, lakini pia alicordinate vizuri na wizara ya Ulinzi kuipatia nchi yetu mahitaji muhimu ya mapambano.

Ukiachilia mbali hilo, alikuwa ni mwanadiplomasia nguli aliyearticulate vizuri sana huko duniani positions za Tanzania kuhusu harakati za ukombozi wa Afrika.
 
Ujumbe murua wa viongozi wengi waliofanya kazi na hayati Benjamine William Mkapa wamemwelezea kama kiongozi aliyekuwa haingilii mjukumu yao alikuwa anafanya shughuli zake. Je hili sio jiwe gizani!!
 
Mkapa alikuwa na imani na wateule wake; walimuheshimu na hawakuwa wanamuogopa. Aliweza kuwapa confidence iliyoufanya utawala wake ulete maendeleo ya nchi bila wananchi kuteseka.

Mkapa aliweza kuleta uwiano kati ya maendeleo ya watu na vitu!!!
 
Back
Top Bottom