Nakumbuka tungo ya Shaaban Robert kuhusu kizungumkuti chake kuoa baada ya kufiwa na mke katika kitabu cha "Maisha Yangu Na Baada Ya Miaka Hamsini", sura ya 5, "Mke Wa Pili"
Pengo katika maisha yangu ya nyumbani lililotokea kwa mauti lilikuwa kubwa. Nilizungukwa na upweke pande zote nne. Ujane ulinilemea na katika kila pembe nilikuwa kama windo lake.Nilijiandaa kuvumilia bahati yangu mbaya lakini sikuweza.
Ni bahati mbaya kabisa mtu kufiwa na mshirika wake wa maisha. Kila bidii ya kuvumilia ilikuwa bure. Ni vigumu sana mtu kufaulu katika jaribu kama lile. Nilitamani sana tena niwe na kimbilio, msaada na faraja katika maisha yangu yaliyobaki.......
Kwa zaidi soma kitabu cha Shaaban Robert "Miasha Yangu Na Baaada Ya Miaka Hamsini".