Mzee Mangula kufunga ndoa na mwalimu kesho...

Mzee Mangula kufunga ndoa na mwalimu kesho...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
mangulla.jpg

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Phillip Mangula

Na Shaban Lupimo na Brandy Nelson | Mwananchi | Aprili 5, 2013

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Phillip Mangula anatarajia kufunga ndoa kesho katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini, mjini Njombe.

Mzee Mangula anafunga ndoa na Mkuu wa Sekondari ya Philip Mangula, iliyopo wilayani Wanging'ombe, mkoani Njombe, Yolanda Kaberege.


Hatua hiyo ya Mzee Mangula kuoa inakuja baada ya aliyekuwa mke wake kufariki dunia mwaka 2004, kutokana na ugonjwa wa saratani.

Msemaji wa familia ya Mzee Mangula ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) tawi la Njombe, Dk Lechion Kilimike alilieleza Mwananchi kuwa ndoa hiyo itaongozwa na Askofu Mstaafu wa Kanisa hilo, Solomon Swalo.

Dk Kilimike alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye anatarajia kuwasili kesho mkoani hapa akitokea Mbeya ambako atatua leo saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Songwe.

Waziri Mkuu Pinda anatarajiwa kufuatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali walioalikwa kwenye sherehe hiyo.

Habari zinaeleza kuwa, baada ya kumalizika kwa ndoa hiyo itakayofungwa saa 3:00 asubuhi, Pinda ambaye ndiye kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni, atakwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti linaloanza Aprili 9
 

Wow alikuwa AMECHOKA KIJIJINI viatu vimechoka; PESA ya CCM Imeshamtakatisha na kupata KIPUSA cha KUOA...
Kweli PESA za CCM hazidanganyi... Lakini MONEY is not all the HAPPINESS in the WORLD!!!
 
Mimi naona ni utaratibu wa kawaida kabisa.Hata Mzee Mandela alioa ili apate mtu wa kumsaidia katika shughuli zake.Lakini hii ya kuitana Wachumba na kuishi pamoja bila kuhalalishwa ni dhambi kubwa sana.Tena ukifikiria meno yameisha anza kudondoka kinywani.
 
Wow alikuwa AMECHOKA KIJIJINI viatu vimechoka; PESA ya CCM Imeshamtakatisha na kupata KIPUSA cha KUOA...

Kweli PESA za CCM hazidanganyi... Lakini MONEY is not all the HAPPINESS in the WORLD!!!

Alianza kufanya ngono zembe na mwajiriwa wake, na pengine alipata nafasi hiyo ya ukuu wa shule hiyo kwa rushwa ya ngono, leo wameamua kutakatisha ufuska waliozoea kufanya kwa kufunga ndoa.

Huwezi kuamini mambo haya CCM katika umri kama huo kufunga ndoa leo wakati mtu ni wa kutunzwa na wajukuu. Hakuna kufanya maendeleo ila kuchuma na kuzitumia kwa kwenda mbele kustarehe na wanawake. Hii habari inatufumbua mengi kama ile ya Gazeti la habari leo Jumapili kuipa Habari Kuu ukurasa wa mbele kuhusu Makahaba wa Kinywarwanda kutinga Dodoma kuwafuata Wabunge kuwapa ridhio la ngono.
 
Nakumbuka tungo ya Shaaban Robert kuhusu kizungumkuti chake kuoa baada ya kufiwa na mke katika kitabu cha "Maisha Yangu Na Baada Ya Miaka Hamsini", sura ya 5, "Mke Wa Pili"

Pengo katika maisha yangu ya nyumbani lililotokea kwa mauti lilikuwa kubwa. Nilizungukwa na upweke pande zote nne. Ujane ulinilemea na katika kila pembe nilikuwa kama windo lake.Nilijiandaa kuvumilia bahati yangu mbaya lakini sikuweza.

Ni bahati mbaya kabisa mtu kufiwa na mshirika wake wa maisha. Kila bidii ya kuvumilia ilikuwa bure. Ni vigumu sana mtu kufaulu katika jaribu kama lile. Nilitamani sana tena niwe na kimbilio, msaada na faraja katika maisha yangu yaliyobaki.......

Kwa zaidi soma kitabu cha Shaaban Robert "Miasha Yangu Na Baaada Ya Miaka Hamsini".
 
shemejiiiiiiiiiii!
hongera sana kwa MKUU WA SHULE YA PHILLIP MANGULA!
hiv hii shule ni ya serikali au binafsi?
NAULIZA TU!
 
Wamekutana baada ya kupata Umakamu wa CCM Taifa? Mwalimu mkuu shule ya sekondari Phillip Mangula na mme mtarajiwa Phillip Mangula is it coincidence? Mangula mke wake ni marehemu, je Bi harusi mtarajiwa nae mme wake ni marehemu?
 
Mi nalia na utitiri wa shule za secondary kujaaa majina ya viongozi hata kama hao viongozi hawakufanya lolote lile la maana katika nchi hii!! There should be some exceptional contribution from somebody in order to be honored a name of the school. This is bullshit!!
Kila la kheri mzee Mangula, ila pia punguza fitina kwenye siasa.
 
dah, afadhali pinda kapata pacha wake aisee

maana tukiwaweka pale kati Pinda, Mangula, mgimwa na Wasira lazma mtu ukae

....hahahahaha......halafu na wewe mwenyewe ukijiweka katika kundi....basi inakuwa balaa.....hahahah
 
mwenye historia ya huyo mwanamke, hajawai kuolewa au kuzaa.?
 
Mimi naona ni utaratibu wa kawaida kabisa.Hata Mzee Mandela alioa ili apate mtu wa kumsaidia katika shughuli zake.Lakini hii ya kuitana Wachumba na kuishi pamoja bila kuhalalishwa ni dhambi kubwa sana.Tena ukifikiria meno yameisha anza kudondoka kinywani.
so alikua anazini kwa kipindi chote hicho
 
hawa wazee ni balaaa sna wapenda sana vitoto hata umri umeshawaacha wanaona ndio watafia kwenye mjengo
 
Back
Top Bottom