Akiwa amebakiza masiku machache sana katibu mkuu kiongozi mzee Luhanjo yuko katika heka heka kubwa kuwaweka watu wake katika nafasi ya ukurugezi mkuu wa PSPF na TIC, Mzee Luhanjo pale PSPF anahaha kumuweka bwana Masha na Kule kituo cha uwekezaji TIC anahaha kumuweka bwana Mbilinyi.
mzee Luhanjo anapambana sana kuona haya masiku machache yaliyobaki katika kiti chake anafanikiwa mpango wake huo mbovu. wana JF habari ndio hiyo ya babu yetu mamvi.
Sabato Masalia;
nakusalimu kwa unyenyekevu mkuu kayika jina la JAMIIFORUM.
Pia kwa heshima kuu ya kuhani wake INVISIBLE MAN!
ambapo katika yeye wazo hili la makutano ya vichwa vinavyofanya kazi LILIPANDWA, LIKAMEA, LIKAKUA....
likakua na kushiriki katika UKOMBOZI WA FIKRA ZA WATANZANIA...
na likavifunika viblog vyenye kupoteza muda kuonyesha VISUTI VYA WAKUBWA NA DHIFA ZA IKULU...........
hata likawa kero kwa wakubwa hadi kuwa agenda ZA KAMATI KUU YA CCM!!!
itakuwa hivyo mpaka mwisho!!
na kama ilivyo ada, TUNASEMA HAKI, HATUSINGIZII, HATUFANYI MAJUNGU......
Ewe invisible, uendelee kutuombea, bila kupiga ban za moja kwa moja...
ili UKABILA, UDINI NA NI WAPI UNATOKEA visiendelee kutunyemelea......
hata FAIZAFOXY GENUIS BRAIN, MALARIA SUGU, MKIGOMA NAPE na wenzao waache kufikiria kutumia MASABURI......
na kujirekebisha kadiri wanavyoshauriwa na wenye akili, MITUME WA JF
na KINGWANGALAH aendelee kupata Ujasiri.
naye awashirikishe wenZie katika TUNU NJEMA ZA JAMII FORUMS.....
kwa ajili ya mama yetu TANZANIA TUNAOMBA HAYA!
NA WOTE TUSEME AMEN!!!
KAKA,
kuzingatia tunu hizi tulitegemea ulipoipost hii thread ufafanue:
i. je hawa jama hawastahili hizi post?
ii. je CV zao zinasemaje? hawana credentials? je background yao inasemaje? je ni nani anastahili nafasi hizo kuliko hawa waliotajwa?
nachelea kutamka kuwa kama haya hayapatiwi majibu basi tutakuwa tumepoteza muda kukatiza kwenye hii thread!
naomba kuwakilisha!