Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,237
Kuna mambo yanashangaza sana! Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye alikuwa miongoni mwa wasimamizi wa uchaguzi Mkuu nchini Zambia ameonekana hadharani akiwa na Mahasimu wakuu wa siasa za Zambia baada ya kikao cha upatanishi, Tunamshukuru kwa jambo hilo.
Lakini swali letu linabaki kuwa hili, ikiwa kama ameweza kupatanisha Dikteta uchwara Edgar Lungu na Rais mpya Haikainde Hichilema aliyeteswa miaka yote ya Lungu madarakani, ameshindwaje kupatanisha chama chake cha CCM na wapinzani wanaoteswa kwa kubambikwa kesi za uongo ili kuwakomoa? Au Mzee huyu akili yake inafanya kazi anapokuwa nje ya nchi lakini inaondoka anapofika Tanzania? Kupatanisha wa nje wakati kwako kunateketea amelenga kutafuta umaarufu wa bei rahisi kwa jumuia ya kimataifa ili apate ujiko?
Kama Kikwete anataka upatanishi basi muda wake ni huu, aielekeze CCM kufuta kesi zote za uongo walizofunguliwa wapinzani nchi nzima na ahakikishe KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI vinapatikana nchini Tanzania, vinginevyo asije akathubutu kuja kuomba upatanishi baada ya sisi kuiangusha CCM 2025, hatutakubali na TUTAMTIMUA .
Mungu ibariki Tanzania