Dr. Slaa, Watanzania tumechoka kuongopewa, leta ushahidi wa haya madai yako

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
Ni vizuri Watanzania tukakumbuka historia ya tuhuma lukuki zilizowahi kutolewana Katibu Mkuu huyu wa Chadema toka aanze siasa na ambazo zote zilikuja thibitika kuwa ni za uongo.

Tarehe 08/03/2015, Dr. Wilbroad Slaa Katibu Mkuu wa Chadema kupitia kwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Ndugu Mabere Marando alitoa tuhuma kwa Serikali na kuwahusisha baadhi ya viongozi wa juu wa CCM kuwa wanapanga njama za kumdhuru Katibu Mkuu huyo wa Chadema.

Kimsingi tuhuma hizi ni za kipuuzi, lakini uongo huu usipojibiwa unaweza kugeuzwa kuwa ajenda na Chama hiki cha Chadema kwa kukosa ajenda zingine za maana. Hakuna asiyejua kuwa Chadema kwa sasa kinapumulia mashine, hivyo maneno na matendo yao kwa sasa lazima yalenge kujaribu kujinasua na balaa la kufa kwa chama chao.

Akiwa Singida katika kampeni za Urais za mwaka 2010,Dk. Slaa aliwatangazia wananchi mkutanoni kwamba kulikuwa kumekamatwa lori kubwa la mizigo (semi-trela) lililojazwa karatasi za kura za Urais zilizokuwa tayari amepigiwa kabisa mgombea Urais wa CCM, Dk.Jakaya Kikwete.


Katika kuonyesha kwamba alikuwa na uhakika wajambo hilo, alisoma hadi namba za lori hilo na tela lake kutoka kwenye karatasi aliyokuwa ameshika mkononi, kisha akasema kuwa lori hilo lilikamatwa katika mji mdogo wa Tunduma, mkoa wa Mbeya wakati likiingia nchini kutoka Lusaka, Zambia.

Lakini baada ya polisi kuchukua hatua za haraka wakitumia namba za lori na tela lake alizokuwa amezisoma na kulikamata, kisha wakalipekua hadharani huku wananchi wakishuhudia palepale Tunduma, kilichokutwa ndani ya lori ilikuwa shehena ya vipodozi vya kina mama na sabuni za manukato.

Baada ya siku chache huku akiwa amesahau yote, Dk.Slaa akatangaza tena kuwa mgombea Urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alikesha katika hoteli ya Lakairo, Mwanza akiweka mikakati ya kuiba kura siku ya uchaguzi huo wa mwaka 2010 ili ashinde. Siku chache alisema kura zimeingizwa na zimeshapigwa, hapa alisahau anadai ndio kwanza mpango unapangwa.

Aliwataja watu wengine aliodai walikuwa pamoja na Rais Kikwete kuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Igunga,Rostam Aziz na Mkurugenzi wa Hoteli hiyo iliyopo katika jiji la Mwanza, Lameck Airo. Lakini wakati Dk. Slaa akisema uongo huo,Rais Kikwete siku nzima na usiku wake wote alikuwa Mtwara akiendelea na kampeni zake za Urais.

Hata Rostam Aziz naye kwa siku hiyo pamoja na usiku wake wote alikuwa Igunga akiendelea na kampeni zake za Ubunge, na pia hata Airo naye siku nzima na usiku wote huo alikuwa jimboni kwake Rorya akifanya kampeni zake za kugombea Ubunge. Baada ya kushindwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk. Slaa aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na ushahidi wa matokeo ya Urais ya kituo kwa kituo ya nchi nzima yakionyesha kuwa alishinda.

Akasema, chama chake kingeyasoma hadharani na kuwakabidhi waandishi wa habari ili wananchi waujue ukweli kuwa alidhulumiwa ushindi wake, kazi iliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na haki yake akapewa aliyekuwa mgombea Urais wa CCM, Jakaya Kikwete.

Lakini kwa vile alikuwa akiwatangazia uongo wananchi, Dk. Slaa hadi leo hajawahi kuyasoma matokeo hayo ya kughushi, badala yake alipowaita tena waandishi wa habari akatangaza kuwa Tanzania isingetawalika mpaka arudishiwe haki yake.



Januari, 2011 aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na mkanda unaothibitisha kuwa mauaji ya Januari 5, mwaka huo yaliyofanyika katika jiji la Arusha kutokana na maandamano ya vurugu ya wafuasi wa Chadema yalifanywa kwa makusudi na polisi, na kwamba wafuasi wake hawakufanya fujo wala vurugu zozote.
Alisema mkanda huo angeuonyesha mbele ya waandishi wa habari ndani ya siku tatu au mbili baada ya Polisi Makao Makuu,kuonyesha unaothibitisha kwamba wafuasi wa Chadema walifanya vurugu ikiwemo kutaka kuvamia Jengo la Makao Makuu ya Polisi la Mkoa na kupora silaha zilizokuwa humo,


wawafungulie wahalifu waliokuwa ndani na kulichoma moto jengo lenyewe.

Lakini tokea kipindi hicho hadi sasa ikiwa tayari imeshapita miaka minne, Dk. Slaa siyo tu ameshindwa kuuonyesha mkanda huo "ndani ya siku tatu ama mbili" alizokuwa ameahidi, bali amethibitisha kwamba alichosema kwa Watanzania ulikuwa ni uongo na uzushi. Mwaka 2011, Dr. Slaa alikwenda mbali kwa kuzusha kwenye mkutano wa hadhara kuwa aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati huu Brig. Gen. mstaafu Yohana Balele amefariki dunia.

Akajaribu kuwaaminisha wananchi pale kuwa ni kweli, baadae ikagundulika kuwa Mkuu huyo wa Mkoa ni mzima na wala haumwi. Haikujulikana mara moja sababu za Dr. Slaa kumzushia kifo Mkuu huyo wa Mkoa.


Julai 2012, Dr. Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika walizusha kwamba wanafuatiliwa na baadhi ya Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ili wauawe, lakini walipotakiwa kupeleka ushahidi wao katika vyombo vya dola ili kusudi watuhumiwa wachunguzwe na hatimaye wakamatwe na kuruhusu Sheria ichukue mkondo wake, wote waligoma na kudai hawapo tayari kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Waliendelea na msimamo huo hata pale Dk. Slaa alipolazimishwa kwenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kuhojiwa, lakini akashindwa kutoa uthibitisho wake mwenyewe wala wa Mnyika kwa sababu walidai suala hilo limezungumzwa katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema.


Mwaka 2012, Dr. Slaa akiwa ziarani Ifakara wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro, alidai kuwa CCM imeingiza silaha kutoka nje ya nchi kontena zima, ili zitumike kuwadhuru viongozi wa Chadema, jambo ambalo hata hivyo hadi leo ameshindwa kulitolea uthibitisho wala kielelezo chochote.

Wanaomfahamu vizuri endapo ingekuwa kweli angeita waandishi wa habari, akatoa ushahidi wake na kuwakabidhi ili wautumie kuandika madai hayo, lakini kwa sababu ulikuwa ni uongo ndiyo maana hakutoa karatasi yoyote hadi leo.
=============================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA CCM


Tarehe 08/03/2015, Dr. Wilbroad Slaa Katibu Mkuu wa Chadema kupitia kwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Ndugu Mabere Marando alitoa tuhuma kwa Serikali na kuwahusisha baadhi ya viongozi wa juu wa CCM kuwa wanapanga njama za kumdhuru Katibu Mkuu huyo wa Chadema.

Kimsingi tuhuma hizi ni za kipuuzi, lakini uongo huu usipojibiwa unaweza kugeuzwa kuwa ajenda na Chama hiki cha Chadema kwa kukosa ajenda zingine za maana. Hakuna asiyejua kuwa Chadema kwa sasa kinapumulia mashine, hivyo maneno na matendo yao kwa sasa lazima yalenge kujaribu kujinasua na balaa la kufa kwa chama chao.

Ni vizuri Watanzania wakakumbuka historia ya tuhuma lukuki zilizowahi kutolewa na Katibu Mkuu huyu wa Chadema toka aanze siasa na ambazo zote zilikuja thibitika kuwa ni za uongo. Hapa nitawakumbusha baadhi.

Akiwa Singida katika kampeni za Urais za mwaka 2010, Dk. Slaa aliwatangazia wananchi mkutanoni kwamba kulikuwa kumekamatwa lori kubwa la mizigo (semi-trela) lililojazwa karatasi za kura za Urais zilizokuwa tayari amepigiwa kabisa mgombea Urais wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete.

Katika kuonyesha kwamba alikuwa na uhakika wa jambo hilo, alisoma hadi namba za lori hilo na tela lake kutoka kwenye karatasi aliyokuwa ameshika mkononi, kisha akasema kuwa lori hilo lilikamatwa katika mji mdogo wa Tunduma, mkoa wa Mbeya wakati likiingia nchini kutoka Lusaka, Zambia.

Lakini baada ya polisi kuchukua hatua za haraka wakitumia namba za lori na tela lake alizokuwa amezisoma na kulikamata, kisha wakalipekua hadharani huku wananchi wakishuhudia palepale Tunduma, kilichokutwa ndani ya lori ilikuwa shehena ya vipodozi vya kina mama na sabuni za manukato.

Baada ya siku chache huku akiwa amesahau yote, Dk. Slaa akatangaza tena kuwa mgombea Urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alikesha katika hoteli ya Lakairo, Mwanza akiweka mikakati ya kuiba kura siku ya uchaguzi huo wa mwaka 2010 ili ashinde. Siku chache alisema kura zimeingizwa na zimeshapigwa, hapa amesahau anadai ndio kwanza mpango unapangwa.

Aliwataja watu wengine aliodai walikuwa pamoja na Rais Kikwete kuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Mkurugenzi wa Hoteli hiyo iliyopo katika jiji la Mwanza, Lameck Airo.

Lakini wakati Dk. Slaa akisema uongo huo, Rais Kikwete siku nzima na usiku wake wote alikuwa Mtwara akiendelea na kampeni zake za Urais.

Hata Rostam Aziz naye kwa siku hiyo pamoja na usiku wake wote alikuwa Igunga akiendelea na kampeni zake za Ubunge, na pia hata Airo naye siku nzima na usiku wote huo alikuwa jimboni kwake Rorya akifanya kampeni zake za kugombea Ubunge.

Baada ya kushindwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk. Slaa aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na ushahidi wa matokeo ya Urais ya kituo kwa kituo ya nchi nzima yakionyesha kuwa alishinda.

Akasema, chama chake kingeyasoma hadharani na kuwakabidhi waandishi wa habari ili wananchi waujue ukweli kuwa alidhulumiwa ushindi wake, kazi iliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na haki yake akapewa aliyekuwa mgombea Urais wa CCM, Jakaya Kikwete.

Lakini kwa vile alikuwa akiwatangazia uongo wananchi, Dk. Slaa hadi leo hajawahi kuyasoma matokeo hayo ya kughushi, badala yake alipowaita tena waandishi wa habari akatangaza kuwa Tanzania isingetawalika mpaka arudishiwe haki yake. Hapo ndipo ghasia zikiwemo za mauaji za Chadema zilipoanza hadi leo.

Januari, 2011 aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na mkanda unaothibitisha kuwa mauaji ya Januari 5, mwaka huo yaliyofanyika katika jiji la Arusha kutokana na maandamano ya vurugu ya wafuasi wa Chadema yalifanywa kwa makusudi na polisi, na kwamba wafuasi wake hawakufanya fujo wala vurugu zo zote.

Alisema mkanda huo angeuonyesha mbele ya waandishi wa habari ndani ya siku tatu au mbili baada ya Polisi Makao Makuu, kuonyesha unaothibitisha kwamba wafuasi wa Chadema walifanya vurugu ikiwemo kutaka kuvamia Jengo la Makao Makuu ya Polisi la Mkoa na kupora silaha zilizokuwa humo, wawafungulie wahalifu waliokuwa ndani na kulichoma moto jengo lenyewe.

Lakini tokea kipindi hicho hadi sasa ikiwa tayari imeshapita miaka minne, Dk. Slaa siyo tu ameshindwa kuuonyesha mkanda huo "ndani ya siku tatu ama mbili" alizokuwa ameahidi, bali amethibitisha kwamba alichosema kwa Watanzania ulikuwa ni uongo na uzushi.

Mwaka 2011, Dr. Slaa alikwenda mbali kwa kuzusha kwenye mkutano wa hadhara kuwa aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati huu Brig. Gen. mstaafu Yohana Balele amefariki dunia.

Akajaribu kuwaaminisha wananchi pale kuwa ni kweli, baadae ikagundulika kuwa Mkuu huyo wa Mkoa ni mzima na wala haumwi. Haikujulikana mara moja sababu za Dr. Slaa kumzushia kifo Mkuu huyo wa Mkoa.

Julai 2012, Dr. Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika walizusha kwamba wanafuatiliwa na baadhi ya Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ili wauawe, lakini walipotakiwa kupeleka ushahidi wao katika vyombo vya dola ili kusudi watuhumiwa wachunguzwe na hatimaye
wakamatwe na kuruhusu Sheria ichukue mkondo wake, wote waligoma na kudai hawapo tayari kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Waliendelea na msimamo huo hata pale Dk. Slaa alipolazimishwa kwenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kuhojiwa, lakini akashindwa kutoa uthibitisho wake mwenyewe wala wa Mnyika kwa sababu walidai suala hilo limezungumzwa katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema.

Mwaka 2012, Dr. Slaa akiwa ziarani Ifakara wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro, alidai kuwa CCM imeingiza silaha kutoka nje ya nchi kontena zima, ili zitumike kuwadhuru viongozi wa Chadema, jambo ambalo hata hivyo hadi leo ameshindwa kulitolea uthibitisho wala kielelezo chochote.

Wanaomfahamu vizuri endapo ingekuwa kweli angeita waandishi wa habari, akatoa ushahidi wake na kuwakabidhi ili wautumie kuandika madai hayo, lakini kwa sababu ulikuwa ni uongo ndiyo maana hakutoa karatasi yoyote hadi leo.

Juzi bila aibu anaibuka na tuhuma zingine za eti kutaka kuuawa. Kupanga kumdhuru Dr. Slaa, ili CCM ipate nini kwa kudhurika kwake? Kwa umri wake, afya yake na kadhalika, kwa nini CCM ipange kumdhuru mzee huyu? Huu ni mwendelezo wa tabia yake ya kuzusha mambo ya uongo kila anapoona anachuja kisiasa. Ni busara kwa umri wake akatumia muda wake mwingi KUMRUDIA MWENYEZI MUNGU.

Lakini hata mtu aliyetumika kuufikisha uongo huo kwa umma, naye ana historia ya kuzusha mambo na kusema hata asiyoyaamini.

Marando aliwahi kuitisha kikao na waandishi wa habari na kudai Katibu wa Itikadi na Uenezi alifaidika na pesa za EPA, alipobanwa na mteja wake aliyekuwa akimtetea mahakamani kwa kesi hiyo hiyo ya EPA, akaruka yale matamshi yake kwa maandishi na kudai ilikuwa ni shinikizo la Chama chake kusoma yale maneno lakini hata yeye hayaamini.

Lakini ni Marando huyu huyu ambaye akipanda kwenye majukwaa ya siasa anadai swala la EPA ni ufisadi mkubwa sana kwa nchi na akishuka tu jukwaani, anakimbia mahakamani kwenda kuwatetea watuhumiwa hao hao wa EPA aliowaita majukwaani mafisadi wa EPA. Mzee huyu naye ni mnafiki.

Hebu tujiulize, ni lini Mabere Marando aliacha rasmi kazi yake ya awali ya ukachero mpaka aaminike leo kufanya kazi afanyayo? Nani alimtumia kujaribu kusambaratisha chama cha NCCR-Mageuzi miaka ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi nchini? Hivi ni kweli Marando ni wa kuaminiwa leo?

Natoa wito kwa Watanzania bila kuingilia utaratibu wa Sheria na vyombo vya Serikali kufuatilia uongo huu mpya, Watanzania nawaomba wampuuze na kupuuza uongo huu. Usitupotezee muda, tuendelee na mambo ya msingi ya kujenga nchi yetu.

Nimshauri pia babu yangu Dr. Slaa, kwa umri wake, wenzake wakifikisha umri huu wa uzee wanatumia muda wao kumrejea Mwenyezi Mungu badala ya yeye kuendelea kutunga uongo na uzushi kila kukicha. Namwomba mwenyezi Mungu ampe kuiona busara hiyo.

Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
10/03/2015


 
Hutatadanganya wengi,
Wewe kama unataka Dr.Slaa umkamate uongo wake kafungue kesi mahakamani.
Ikumbukwe kuwa hata kifo cha Daud Mwangosi mlisema chadema imeshiriki,Tv zilupoleta video mkanywea
Kule Soweto mlipoambiwe mwende mahakamani mliishiwa nguvu mkanywea,
Ulimboka mliambiwa aitwe aje kutoa ushahidi,mkanywea!
Cha kujiuliza tu ndg kama kweli zinachaji;
1. Wakati unahoji haya,watuhumiwa wa madawa ya kulevya wako wapi?,
2. Wakati unaleta huu -----,tuambie unawajua waliorudisha pesa na kuweka mlangoni wa EPA?
3. Wakati unaleta uzembe huu ukitaka kutuaminisha,uliwahi kuona mtu anasema anataka kuuawa harafu polisi wapuuze hivohivi?
4. Tuambie wale vijana,waliouawa wa wamadini kutika Morigoro ilikuwaje?
5. Unaweza kutuambia aliyemuua Mwangosi na kumtesa Ulimboka hatua zimefika wapi?
 
ushahidi number Mojave JE MAKONGORO MAHANGA ALISHINDA UBUNGE SEGEREA? MASELE ALISHINDA SHINYANGA? kama wanaweza badirisha matokeo kwa kusoma matokeo yasio ya Kweli watashindwaje kuleta hata makontena iahirini ili kuongeza kura? tafakali
 
xenaxena;

Huyo Ulimboka si yupo hadi leo, mwambieni awataje au apeleke kesi mahakamani. Kesi ya Mwangosi ipo mahakamani kama ulikuwa hulijui hilo.
 
Last edited by a moderator:
Huyo Ulimboka si yupo hadi leo, mwambieni awataje au apeleke kesi mahakamani. Kesi ya Mwangosi ipo mahakamani kama ulikuwa hulijui hilo.


Acha uhuni kazi ya polisi ni kuhakikisha usalama wa mali za wananchi na raia wake,Ulimboka kwa kitebdo chake hicho alichofanyiwa alistahili kuhojiwa ili kujua nini kimempata.
Ikikuwa vigumu kwa Ulimboka,imekuwa Rahisi kwa Gwajma kumwita kituo cha polisi kuhojiwa.
Nikwambie tu kuwa Daima "Taabu huja na kuisha,ila ujinga hautakwisha sisi tutasonga mbele chadema,haitatishwa na mbinu za kuanzisha tuhuma,kubambikia kesi,kupiga mabomu,kuanzisha vyama bandia na kuvifadhiri,.
 
Great minds discuss ideas; average minds discuss events; small minds discuss people.
jichagulie hapo wewe unadiscuss nini?
f


....ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki,kwa kuwa mnasafisha kikombe nje, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi,...

Ole wenu waandishi na mafarisayo kwamnachuja mbu na kumeza ngamia..
Mwaonekana ndani wenye haki,baki ndani mmejaa unafiki na maaso!!!"
 
f


....ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki,kwa kuwa mnasafisha kikombe nje, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi,...

Ole wenu waandishi na mafarisayo kwamnachuja mbu na kumeza ngamia..
Mwaonekana ndani wenye haki,baki ndani mmejaa unafiki na maaso!!!"


Kamanda povu la nini tena?
 
Mkuu,

Kama Dr Slaa anaongopa ,kwa nini msimpeleke mahakamani ili alete ushahidi???

Haiwezekani mtu huyu kila Siku ya Mungu analeta ule uliouita uzushi halafu mpaka sasa mnashindwa hata kumpeleka mahakamani.Mnahofia nini?

Ukweli ni kwamba mnajua dhahiri kwamba pale mtakapomfikisha mahakamani basi ukweli utawekwa wazi.

MPELEKENI MAHAKAMANI KAMA MNA JEURI.
 
Na ile video ya Arusha aliosema mbowe anayo imefikia wapi

Video ipo raisi aliambia aunde tume ya majaji na viongozi wa CHADEMA wangepeleka ushahidi huko lakini mpaka leo raisi hajaunda hiyo tume ya majaji sasa unataka hiyo video wamepewe wahusika wenyewe wa mauaji wakati mwingine tumia akili unapoandika habari ambazo hujui.
 
Well, Mikataba ya Kishenzi kwenye Madini, ATC, TRL, TPA, NAFCO, BANKS, VITALU VYA UWINDAJI, LIST OF SHAME, UJANGILI, EPA, ESCROW mlisema amedanganya lakini ilikuja kubainika kuwa ni UKWELI mtupu ... Nani asiejua kuwa CCM inapumulia mashine ndo maana kwa kutumia TISS wameanzisha ACT kwa lengo la kuchakachua kura za UKAWA? ... Watanzania wa leo si wajinga tena! Sheria ya mitandao haitazuia watu kupost matokeo kwenye vituo vya kupigia kura ...
 
xenaxena;

porojo zingine hazina hata maana.Nilitegemea wale wote walioathirika na tuhuma hizo za Dr.Slaa waende mahakamani wakashitaki,badala yake tunaona matamko yasiyo kichwa wala miguu.
 
Last edited by a moderator:
porojo zingine hazina hata maana.Nilitegemea wale wote walioathirika na tuhuma hizo za Dr.Slaa waende mahakamani wakashitaki,badala yake tunaona matamko yasiyo kichwa wala miguu.


Hawatafanya hivyo,shetani hajifitini kaka!
 
slaa ana hasira sana na ccm na serikali mpaka anataman kupasuka. Hapo anasema haya yote ili awavuruge wananchi wamuhurumie. Na uzee wake hatakaa awe rais wa Tanzania huyu babu inaonyesha ni mafia wa chinichini
 
Back
Top Bottom