Najua ya kwamba ulikuwa ukitupenda sana,japokuwa una mapungufu yako kama Binadamu wote tulivyo lakini ulijitahidi sana kutufanya wenye furaha...
Lakini Dakika za mwisho ukawa si wewe tena tuliyekuwa tunakujua,mwingi wa hekima,mpole,mwenye subira,mnyenyekevu na usiyependa makuu wala kujikweza...
Ni kitu gani tulikukosea hadi ukachukia?
Najua Mzee wangu huwa unapita humu kimya kimya,nami natarajia jibu lako kimya kimya.
NB: Mods Nawaomba muulinde huu Uzi uchangiwe kwa hekima, atakayeleta chuki za kisiasa au matusi na kejeli dhidi ya wengine, apate stahiki yake .