Mzee Kikwete, leo ndiyo leo; msituangushe

Mzee Kikwete, leo ndiyo leo; msituangushe

Huo ni mfano wa outsiders ndani ya CCM usiyekuwa ya sasa.

Tunahitaji mabadiliko kamili.

Wote hao wanaweza kuwa bora kuliko:

1. Majaliwa
2. Ndugai
3. Simbachawene
4. Chenge
5. Mwigulu
6. Kabudi
7. Nk.nk

Na wa namna hiyo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Hapa sijaona mtu mwenye akil wote wazee wa mihemko t
 
Kikwette alianzisha mwenyewe suala la katiba mpya.

Katiba mpya ni msingi.

Magufuli alikataa pamoja na yote aliyovuna yanajulikana. Acha tujaribu nyani wapya kwenye pori jipya.

Ya Mussa hutokea.

Tusifunge milango kabisa.
Kwanini unafananisha JK na JPM kwenye katiba?, Kwanini JK hakuzalisha katiba?
 
Sasa zile kelele ambazo ulikuwa unampigia. Marehemu kuhusu barakoa na lock down mpigie na huyu.
Alafu tuone atawasikilizaa
Nilitabiri lockdown. Kwani kuna ubaya gani kutabiri lockdown?

Lockdown unajua maana yake lakini jombi? Usije kuwa unadhani ni dubwana fulani eeh?

Kwenye kupambana na Corona zipo njia mbili hizi zinazopendekezwa:

1. Mabarakoa
2. Social distancing

Hapo ukichanganya na kunawa nawa maji tiririka hata bila AstraZeneca unaweza kudunda kwa muda.

Lockdown ni total social distancing yaani 100% social distancing. Yaani kiwango cha mwisho cha social distancing.

Kumwelesha mburula haijawahi kuwa rahisi lakini.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
sasa zile kelele ambazo ulikuwa unampigia. Marehemu kuhusu barakoa na lock down mpigie na huyu.
Alafu tuone atawasikilizaa
Marehemu hakuwa na kosa moja tuu bali mengi, kuteka watu, kuua watu, kubambikia kesi watu, kupora mali na hela za watu, udini, ukabila, ukanda na chuki.
 
Mh. Rais mstaafu Jakaya Kikwette tunayo matumaini makubwa kwenu kuwa ule muda ambao taifa hili limeusubiri mno hatimaye umewadia.

Ni wazi kuwa kila mtu katika nchi hii angalipendelea tuishi sote kwa usawa na haki. Utashi wa viongozi wa juu katika kufanikisha hayo ni jambo la muhimu sana.

Kufanya maamuzi magumu yatakayorejesha imani ya wananchi kwa nchi yao itakuwa jambo la msingi mno kwa sasa labda kuliko jambo lolote lile.

Pana watu wakiwamo watia nia wengi waliojaribu kuutaka urais na kura kuwa hazikutosha hali nafasi ni moja wakiwamo akina:

1. Asha Rose Migiro
2. Mzee Mwandosya
3. Bernard Membe
4. Mizengo Pinda
5. Frederick Sumaye
6. Edward Lowassa
7. Abdulhaman Kinana
8. Philip Mangula
9. Anna Mghwira
10. Dkt. Slaa
11. Dkt. Nchimbi
12. Nk nk

Watu ambao hawakuwamo ndani ya establishment ya sasa au wale waliokuwa na maoni tofauti kuhusiana na establishment ya sasa kwa hakika wangetufaa sana.

JK tupeni raha kwa kuandaa mustakabala mwema utakaotuletea mwanzo mpya.
Hatuhitaji mtu yoyote kwenye orodha hoyo. Tunachohitaji ni mtu kutoka wsyeule wa Magufuli. Makamu wa Rais atoke kwenye baraza la mawaziri wa JPM. Binafsi naona Kabudi atafaa nafssi hiyo.
 
Upuuzi ni tusi.

Hoja zajibiwa kwa hoja. Ilipokuwa lazima Nyerere aliingia ulingoni.

Go JK go. Tupo wengi tu, tulio nawe.

Chatto Inc. ni wa kuogopa kuliko ukoma!

Hiyo ndiyo habari yenyewe.
Ila kama zama ya JK itatawala tena basi chawa na kunguni watatawala
 
Marehemu hakuwa na kosa moja tuu bali mengi,kuteka watu, kuua watu, kubambikia kesi watu, kupora mali na hela za watu, udini, ukabila, ukanda na chuki.
🤓🤓🤓🤓🤓

Hivi babu seya yuko wapi⁉️, RIP AMATUS LIUMBA maana aliweza kumpigia simu JK Huku akitumikia kifungo cha magumashi
 
sasa zile kelele ambazo ulikuwa unampigia. Marehemu kuhusu barakoa na lock down mpigie na huyu.
Alafu tuone atawasikilizaa

Hadi pale Corona itakapotokomezwa au pale tutakapo kuwa nasi tumekuwa wahanga wa ugonjwa huu, ikiwa hatua zinazochukuliwa haziridhishi, tunapinga kelele.

Kwamba nyungu, maombi au ushirikina gani, hiyo mkawaambie ndege.

Uzi huu ulimhusu sana mpendwa wetu huyu ambaye kwa ujinga wako unadhani tulimchukia:


Tatizo ni kuwa wengi wanakuja kutambua uliwahusu wakati ni too late.
 
Basi ngoja tusubiri.
Tangazo la serikali la barakoa za lazma
Hadi pale Corona itakapotokomezwa au pale tutakapo kuwa nasi tumekuwa wahanga wa ugonjwa huu, ikiwa hatua zinazochukuliwa haziridhishi, tunapinga kelele.

Kwamba nyungu, maombi au ushirikina gani, hiyo mkawaambie ndege.

Uzi huu ulimhusu sana mpendwa wetu huyu ambaye kwa ujinga wako unadhani tulimchukia:


Tatizo ni kuwa wengi wanakuja kutambua uliwahusu wakati ni too late.
 
Hatuhitaji mtu yoyote kwenye orodha hoyo. Tunachohitaji ni mtu kutoka wsyeule wa magufuli. Makamu wa rais atoke kwenye baraza la mawaziri wa jpm. Binafsi naona kabudi atafaa nafssi hiyo.

Hiiiiii bagosha!
 
Tunataka atakae shikilia pale alipoishia magufuri, tulisha zoea kuchapa kazi tulisha zoea kulipa kodi, teyar tunajua sisi ni matajiri na vijana wamejityuni kukaa na kuchapa kazi hivyo hatutaki kurudi nyuma tunahitaji atakae tupeleka mbele zaidi na Sio kurudi nyuma
Hatutaki wauaji pia.
Watekaji,madikteta n.k.
 
Sijajua kwanini watu wana matumaini na wanapigia chapuo watu wao wakati nafasi ya makamu wa Rais haina influence kivile kwa mujibu wa katiba yetu. Au watu wanaitaka kimkakati zaidi baada ya mama ?
Usiidharau hiyo nafasi, ni kubwa kuliko unavyofikiri ndio imemtoa mama leo amekuwa Rais
 
Tunataka mwanzo mpya. Utakaotambua nchi ni yetu sote. Utakaotambua tuna janga la Corona. Utakaotambua katiba mpya ni agenda yetu muhimu.

Mwanzo utakaotambua maendeleo ya watu nayo ni muhimu tena zaidi ya maendeleo ya vitu.
Hoja mfu hizo kwa sababu Serikali muda wote, kupitia Wizara ya Afya, imekuwa ikitoa tahadhari kuhusu kinga ya magonjwa mbalimbali, ukiwemo COVID-19.

Katiba mpya siyo jawabu la mimi na wewe kutimiza wajibu wetu. Majirani zetu zetu walibadilisha Katiba, upinzani Tz wakawa wanaisifia sana. Sasa hivi wako kwenye mchakato wa Katiba mpya tena.

Uzalendo ndio msingi wa kuheshimu na kutimiza tunayokubaliana
 
Basi ngoja tusubiri.
Tangazo la serikali la barakoa za lazma

Niilazimishe serikali wewe uvae barakoa? Mbona unachachawa jombi?

Sitaki kulazimishwa kutumia nyungu au maombi eti ndizo tiba iliyopo. Sitaki kushurutishwa kubeza na hivyo kutotumia chanjo iliyothibitishwa na WHO.

Hapo ndiyo kwenye mzizi wa fitina.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom