Mzee Kawawa afariki dunia!

It pains alot!!!!!!!!!!


 
dah, leo nahisi nitakwenda home kwa MIGUU ili niweze kuona 2010, maana madreva wa daladala hawakawii kutuingiza mitaroni.
R.I.P kawawa
 
Rest In Peace Mzee Rashid Mfaume Kawawa.Utakumbukwa daima...
 


duuuuuh! imetulia hiii
 
MUNGU ailaze roho ya marehemu Kawawa mahali pema peponi AMEN
 

Ni huzuni na masikitiko makubwa kwa Watanzania sote. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amim\na.
 
Tulikupenda sana lakini Mwenyezi Mungu ameamua kukupenda zaidi! Raha ya milele ikuangazie ewe Simba wa Vita. Wanamsimbazi tunakukumbuka kwamba ulikuwa ni mwenzetu wa UKWELI.....
 
Alikokwenda Kawawa ndiko sote tunakoelekea kwa zamu. Mungu atufungue akili za mioyo yetu tutambue hilo na kijiweka sawa tayari kwa safari ya mwisho isiyo na mawaa. Ameacha kumbukumbu nyingi zinazostahili kukumbukwa. Sisi tulimpenda sana, lakini Mungu alimpenda zaidi. Jina la Bwana libarikiwe, Amen.

Leka
 
Wana BOIZIA (Tabora School) tumepoteza mpiganaji Mzee wetu,Simba wa vita Mzee Rashid Mfaume Kawawa! Mzee Kawawa utaishi milele kwenye mioyo yetu japo umepumzika kimwili kwa sasa.Wana BOIZIA wenzangu mtakumbuka kuwa Mzee wetu Rashid Kawawa na Wenzake ndio waasisi wa ORCHARD enzi zile za Warsal na Berlin na hata tulipokuwa pale camp tulinong'onezwa kuwa Hayati Bibi yetu Sophia Kawawa walikutana kule.

Huyu alikuwa JABARI hata Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kukiri katika Kitabu chake cha UONGOZI NA HATIMA YA NCHI YETU kuwa watu kama kina Kawawa HUZALIWA kwa nadra sana!

Poleni Watanzania wenzangu!! Poleni sana wana BOIZIA popote mlipo duniani !!!!
 
Ni huzuni na masikitiko makubwa kwa Watanzania sote. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amim\na.

RIP Simba wa yuda, uwasalimie ..Sokoine, Nyerere, Kreluu uwaambie mwenzao Kingunge siku hizi ni bilionea wa kutupwa na ameasi ukomunisti pia ukatuombee wadanganyika wote tubadilike akili zetu na zifanane na watu wa kikwelikweli, na ukawaombee mafisadi safari yao wafike haraka segerea, Mungu akulaze mahali pema peponi...Amina
 
........................Nani kauona mwaka, kamaliza mwaka...... NI MAJALIWA YAKE MUNGU KUUONA MWAKA (Quoted from DDC Mlimani Park Song)!
 
TBC Wanarun program zake za zamani, hivi sasa anahojiwa na David Wakati. Natumaini pia tutapata fursa ya kuiona tena ile filamu ya 'Fimbo ya Mnyonge'. Mimi niliiona mwaka 79 pale Viwanja vya Tangamano, mjini Tanga wakati huo wakiita Sinema za Dezo.

Sasa Kawawa anaeleza Alipoingia Tanu, 1956, mwaka mmoja baada ya David Wakati kuajiriwa TBC ile ya Mkoloni.

RIP SIMBA WA VITA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…