Mzee Jaji Warioba ndani ya Dk 45 ITV

Mzee Jaji Warioba ndani ya Dk 45 ITV

Chris Lukosi sina hakika kama unaijua Iringa kabla ya kuwa na Njoluma! Nina wasiwasi mkubwa.
 
Last edited by a moderator:
Go jaji warioba. Nasikitika kwamba kijiti cha kutukanwa na wana ccm kimepokelewa na wenye akili ndogo kutoka kwa rais dhaifu kikwete pale alipowaelekeza wana ccm namna ya kukutukana. Ndo tatizo la akili ndogo kuongoza akili ndogo. Yaani ccm ni bendera fuata upepo hakuna hoja. Nilishangaa mwanamama mmoja bungeni baadaye niliambiwa anatabia ya kujikojolea kitandani usiku eti anamtukana warioba! Hiyo ni laa a mbaya
 
Chris Lukosi sina hakika kama unaijua Iringa kabla ya kuwa na Njoluma! Nina wasiwasi mkubwa.

Bwana Chris Lukosi naichukua hali ya wana Iringa kuanzia Mlandege, Mwangata, Isakalilo, Njia panda ya Ipamba, Kalenga, Mwika (kwao na Costa Magoloso), Mangalali, Nzihi naishia Kidamali. Nije njia ya Mtera nikutajie Nyegere, Makatapola na Radwa. Hivi ni wewe wa Comment hizi bana Chris Lukosi?
 
Last edited by a moderator:
Hana jipya

Jipya lipi unataka ? Hayo mapya si Ndio yameigeuza Zanzibar Kuwa Nchi , hapa kwenye muungano watu wanataka Yale ya Zamani yaani muungano ulee wa Nyerere na karume muungano harisia, kumbuka sasa muungano umechakachuliwa Tanganyika imevaa koti la muungano lenye matobo .
 
Tanganyika ni muhimu Kama Pumzi wasioitaka Tanganyika wanashangaza sana !
 
Mtangazaji: Sina hakika mie nakufahamu kama wewe ni wanachama wa CCM lakini kwa nini wanachama wa wenzako wa ccm wanakushambulia kwa kiasiwakati maoni haya ni ya wananchi?
Warioba:Aaa wanasema ni sera ya chama
Mtangazaji: chama chenu lakini wewe ni wanachama ?
Warioba:Mimi niliwambia wala sikuwambia ccm nilisema na taifa zima.Tulichaguliwa wajumbe 34 tulikuwa kwenye tume,wajumbe 32 kutoka makundi mbalimbali ,katibu na naibu katibu.Kwenye tume kama nilivyosema nilivyokuwa natoa taarifa nilipoteuliwa kuwa mwenyekiti na kuona kundi nilikuwa nalo nikaona hapa siamini kama tutatoka na kundi litakoundanisha watanzania kulikuwemo wawakilshi wa yama vya siasa kwa hivyo tulikaa na kukubaliana huyo ametoka ccm,mwingine chadema,cuf,nssr na mkundi mengine tukibaki na misimamo ya vyama hatutafanya lolote.kwa hiyo sisi kama watanzania tumepewa kazi ya taifa na tutakuwa waaminifu na tutakwenda kuwasikiliza watanzania tupendekeze kama wanavyotaka wanachi na si vinginevyo.
Sasa chama change baada ya kutoka ile na ni kweli wote wananitukana ni kutoka chama change sasa nashangaa kwa sababu wananifahamu kama ni muumimi muundo wa muungano mie ni mmoja wao yaani nimetumia nchi hii kama unajua 1994 nilifika nikakata tama nikasema tujaribu seriakli mbili kuelekea moja.
Mtangazaji:Nani aliwapa hii kazi?
Warioba: Kwanza Nashangaa Yule mama aliyetoa taarifa kamati number moja anasema hatukuwatuma kwenda kufanya hii ,sisi tumefanya kazi kwa mujibu wa sheria na tumefanya kazi kwa kuangalia sheria popote tulikukuwa ilikuwa jambo ambalo la kuzingatia ni uwepo wa muungano na sheria haikusema tuzingatie muundo wa serikali mbili bali uwepo wa muungano na wanachi ndo walizungumzia muundo wa muungano na tukaangalia hoja zilizpo na uhalisia wa utulivu wengi walipendekeza serikali tatu kwa hoja zilizpo na matitizo tukiendela na muundo wa serikali mbili mambo yatakuwa mabaya
Mtangazaji:Wanasema hamkuzingatia hadidu za rejea mkaenda kivenuvenu tu?
Warioba:Katika taarifa tulizotoa kuna vitabu vingi moja ya ile ripoti imeeleza mzhakato wote ,imeeleza historia unajua wakati mwingine wanavyoongea inafikiwa wakati mtu unaoana hawajasoma hizo taarifa
Mtangazaji:Jaji kutoka rohoni mwako unajuta kuwa mwenyekiti katika mchakato huu?
Warioba :Hapana ilikuwa ni hekima tuweze kushughulika kutengeneza katiba hii kwangu ni kwa kweli naona faraja ni heshima kubwa nimepewa kutengeeza katiba kwa mara ya kwanza kutoka wanachi wa kawida nimetumia wakati kutoka utumishi ulitukuka kwa sio sisi wanaotusema wala haina shida ila tunjivunia kwa mara ya kwanza tumetoa utumishi uliotukuka
Mtangazaji:Na unazungumzajehija hii ukuifufua Tanganyika tanznia itakufa
Warioba:Mie nawashangaa watu waliokuwa mstari wa mbele kusema Tanganyika ndo inayofaidika sasa ndo wanaosema ukifufua utavunja Tanzania siwaelewi wanasema Tanganyika ipo na ndo inafaidi.
Tulikwenda Zanzibar wakati tunapata maoni ya wananchi tuakaona tupate na maoni ya taasisi.Hawa sasa wanaosema kwamba ukifufua Tanganyika muungano utakuafa ndio walikuwa wanalalamika jinsi mawaziri wazanzibar wanavyonyayaswa kuapata mikopo na serikali ya muungano inayohudumia Tanganyika.
Mtangazaji:Unazungumzaje kuhusu mwendendo wa bunge la katiba
Warioba:Tatizo ni vyama vyoa kwa hyo unakuta ccm imemua kwamba sisi tujaribu ya kwetu na ndio wengi.wale wenine kwa kuwa hawna wingi kwa kupitisha maamuzi ndo maana wazazuia ili wasipitishe

 
Nimemsikiliza Warioba na kumuelewa sana, Huyu Mzee kweli ni mzalendo asiekuwa na mawaa...Jaji anakata issues tu! Amekiri kuwa wenye kutukana wanatoka CCM na wale wajumbe wa CCM kutoka Zanzibar ni wanafiki wakupitiliza kwani wakati wa kutoa maoni walikuwa wanafunguka sana juu ya umuhimu wa serikali 3 lakini sasa hivi wamefyata mkia!!!... Jaji amesisitiza kuwa CCM wanaweza kuja na katiba yao LAKINI haitadumu! Njia pekee ni maridhiano na kuweka maslahi ya nchi mbele vyama baadae...ameweka wazi kuwa muundo wa serikali 3 hauvunji muungano bali utaimarisha muungano ... Wapayukaji akina Lukuvi , Nchemba, Kigwangalla hawawezi kumsogelea Jaji Warioba hata kwa 0.00000000001%... Akili kubwa siku zote ni akili kubwa Milele daima!!! Lisu Plus Warioba ni zaidi ya akili za magamba wote plus vizazi vyao ambavyo havijazaliwa ....
 
Kazi ya Warioba imekwisha na Kitalu chake cha Tume kimefungwa, huu ni muda wa Bunge la Katiba hana cha kuzuia, kamamvipi ajiunge na UKAWA!
 
Kumbe Wassira ndo alitoa rushwa akafungiwa miaka 5 kushiriiki uchaguzi hivyo jk amemteua waziri mla rushwa na bila shaka na yeye hatakuwa mla rushwa
 
Kazi ya Warioba imekwisha na Kitalu chake cha Tume kimefungwa, huu ni muda wa Bunge la Katiba hana cha kuzuia, kamamvipi ajiunge na UKAWA!

Ndiyo hoja yako hiyo!! Ukiona mtu anaongea pumba huyo lazima ni gamba!
 
Kazi ya Warioba imekwisha na Kitalu chake cha Tume kimefungwa, huu ni muda wa Bunge la Katiba hana cha kuzuia, kamamvipi ajiunge na UKAWA!

Acha ujinga wewe,umekaririshwa na wewe kuonyesha kwamba ndio walewale unapayuka ovyo ovyo,zaidi ya Warioba unataka nani aje afafanue?
 
Nlimwelewa toka zaman sana huyu mzee ccm ikipata watu wanne tu sampuli ya warioba nchi itasongambele kwa haraka sana nimeamini nyerere alikuwa ana nia nzuri na nchi yetu kwan mawazili wake wakuu bado ni moto wa kuotea mbali.
 
Lakin mi cjamwelewa vizuri raisi wangu jk kwan aliwahasa wajumbe kutoweka masilahi ya vyama vyao mbele naye mbona alisimamia maslahi ya chama cha mapinduzi kwenye hotuba yake ya ufunguzi.katiba ya miaka hamsin mbele naona ni kitendawili
 
Back
Top Bottom